Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,496
- 37,789
Kwanza nikupongeze Kwa hili ulilofanya Jana Kwa Gekul maana alisitahili.
Lakini usiishie hapo maana Gekul hakufanikisha unyama huu Peke yake. Baada ya kumtesa na kujeruhi kijana Hashimu ndani ya Hotel yake alimbeba Hadi Polisi ambako manyanyaso na mateso yaliendelea Kwa siku 4 Hadi alipoonekana kudhoofu na akakabidhiwa Kwa Baba yake na Askari Kwa maelekezo kwamba "utamleta tukimhitaji".
Polisi ndio wapokea malalamiko na kuyaanzishia mashitaka. Katika Hali ya kawaida kosa la kuchota fundo la mchanga karibu na nyumba ya Mtu linakuwaje KUTISHIA KUUA?
Jinai ya kuchota mchanga Kwa kiganja cha mkono ni ipi kwenye tukio hili na linamuweka mtuhumiwa mahabusu siku 4?
Kibaya zaidi RPC Katabazi anaulizwa na waandishi wa habari kuhusu mateso na manyanyaso Kwa mtuhumiwa toka Kwa naibu Waziri anakana na kutaka Wenye ushahidi wapeleke kwake. Ushahidi gani aliotaka wakati anajua Kijana alipelekwa Polisi akiwa na majeraha?
Utendaji wa Polisi kubeba na kuficha maovu ya viongozi wa kisiasa yanaumiza wengi na kukichafua Chama cha mapinduzi kionekane cha watesaji na wanyanyasaji. RPC alikuwa na room kubwa ya kumshauri Gekul aachane na kesi hii mapema maana ushahidi wa ushirikina unathibitishwa kishirikina na siyo Kisheria.
Lakini Hashimu akawekwa ndani siku 4 na RPC akawa anaogopa kumtoa akisubiri Gekul aruhusu. Yaani Jeshi la Polisi linamuweka ndani Mtu Kwa maelekezo ya mwanasiasa na halimtoi mpaka mwanasiasa mwenyewe aruhusu. Sasa hapo Nani Polisi? Gekul au Katabazi?
Tunaomba Mheshimiwa Rais wape funzo la weledi maafisa wa Polisi nchi nzima Kwa kumuonyesha mfano RPC wa Manyara aliyediriki kuficha uhalifu wa Gekul na inawezekana mitandao isingepiga kelele hata wewe usingeambiwa madudu ya mteule wako.