Tanzania tuna Rais asiyejua majukumu yake na wajibu wake

kama Marais wastaafu hawatawajibilka kwa utendaji wao au kashfa zilizochomoza wakati wa uongozi wao na kusababisha athari kwa awamu inayofuata kamwe hatutakaa kuendelea na ndio maana kila baya hivi sasa linaonekana ni la kikwete. Kila Rais abebe lake ingawa Rais aliyopo madarakani anawajibika kuziba kasoro za watangulizi wake japo zipo kasoro ambazo haziwezi kuzibwa kwa awamu moja tu.
 
Ha! Ha! Haa! ha ha. Huyo ni chaguo la Mungu mlituaminisha tangu mwaka 2005. Acheni kulialia. Nani analia wakati mlipiga kura wenyewe?

Sasa unabisha?
Mtu huyu ametumwa na MUNGU kuisambaratisha CCM ili ukombozi wa waTZ upatikane!
Kipindi kile sikumuelewa kilaini,lakini sasa nimeanza kumuelewa.
 
Hata kule chadema kuna watu wamemchoka Mbowe ndio maana baadhi wamekihama chama kama David kafulila, Dr Amani Kaborou, na mgogoro wa Wangwe uliibua mengi. Ni matukio tosha kwamba kiongozi huwezi kupendwa na watu wote lakini pia huwezi kuwa mzuri kwa watu wote......huwezi kukubarika na watu wote.
 
CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee JK oyeeeeeeeeeeeeeeeeee mbowe Ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Dr Slaa Ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
kila mtu ana kiongozi aliyemchagua kama wewe ulichagua walioshindwa uchaguzi endelea kuuguza maumivu hadi mwaka 2015 jaribuni tena. Maalim Seif Shariff Hamad aligombea mara 3 akashindwa, Mbowe kagombea mara 2 akashindwa hata Dr Slaa anaweza kugombea mara 4 akashindwa ubaya uko wapi?
 
matusi haya kwa JK ni makovu ya kushindwa kwenye uchaguzi hakuna jingine jipya. waliojeruhiwa kwenye uchaguzi hawachagui silaha za kupigania ili mradi nchi haitawaliki. Kuitetea CCM lazima uwe na roho nguvu kama ilivyo kazi ya kuitetea chadema.....tuvumiliane ndio siasa
 
Hivi ile kashfa ya mbowe ya NSSF na matumizi mabaya ya ruzuku iliishia wapi? huu nao ni ufisadi.
 
mtu mmoja mwenye busara sana alipata kusema walioshindwa kwenye uchaguzi wa kisiasa ni kama nyati aliyejeruhiwa Jk umewajeruhi chadema wako tayari kukusingizia mengi hata ambayo yalitokea awamu zilizopita. hakuna anayetaka kumgusa Mwinyi wala Mkapa kila baya ni wewe tu. Hizi ni dalili za mtu aliyeanza kupoteza kufikiri vema.
 
kama tunaamini kwamba Jk alipendwa sana kashindwa Ikulu kwa nini mnataka tuamini kwamba Dr Slaa anapendwa sana atapaweza Ikulu? kisiasa inakubalika lakini kisayansi haikubaliki
 
Kama ingekuwa ni mahakamani sheria isingebana Jk peke yake na matatizo tunayopata sasa mahakama inaangalia chimbuko/kiini/chanzo na ndipo mlolongo mzima wa wahusika kuwajibika lakini jambo la ajabu hata matatizo yote yaliyosababishwa na awamu zilizopita tunayaona kuwa ni ya JK peke yake.

Ni sheria tuu itakayotekeleza yote haya cha msingi aliyeko juu anapaswa kuhakikisha hakuna mtu anayeipindisha, hapo tutaheshimiana, tutahurumiana, tutawajibishana, tutaogopa kupokea na kutoa rushwa , tutalinda rasrimali zetu, tutaaminiana katika vyama vyote na kupendana, tutajenga nchi yetu, tutaheshimu viongozi wetu na wao watapata Mori wa kutuongoza kwa kufuata taratibu tulizojiwekea.
 
Sasa unabisha?
Kipindi kile sikumuelewa kilaini,lakini sasa nimeanza kumuelewa.
Mtu huyu ametumwa na MUNGU kuisambaratisha CCM ili ukombozi wa waTZ upatikane!

hilo nalo neno umenifurahisha saana kweli watu mnafikiri vizuri
 
Mnamlaumu bure tu, wa kujilaumu ni sisi wenyewe, maana ndio tuliomweka madarakani

Waliomuweka wenyewe wanalia kwani hali hii inatutesa wote haijali wewe ulimpigia kura au la, wanaofaidi ni wateule wake wachache tu.Lakini mi ninaona Jk kwa haya yanayotupata anastahili lawama kubwa sana kama dereva wa gari linaloitwa Tz kwani analiendesha bila ustaarabu.Ndio maana akiwa Uingereza aliulizwa kwanini tz maskini akasema hata yeye hajui kweli huyu ni Rais?
 
hili limeshakuwa taifa la walalamikaji.mtu anakurupuka usingizini na kuja apa na na hoja ya ajabu.mi naona mwny thred ndo hajui majukum ya raiS.anajifanya much know.rais ana watendaj chini yake ambao wanawajibika kwa hayo mambo.kuna mawaziri,makatibu wakuu ndio wanahusika moja kwa moja au mnataka kupandikiza chuki isiyo na maana km KAWAIDA YENU?RAIS ANAJUA MAJUKUM YAKE YALIYOAINISHWA KWNY KATIBA NDO MANA ALIOMBA URAIS.
 
Mnamlaumu bure tu, wa kujilaumu ni sisi wenyewe, maana ndio tuliomweka madarakani

Sema unachokijua na ulichonacho uhakika! Aliyemteua kwenye uwaziri ni sisi? Walibebana wenyewe kipindi cha mwinyi wakahonga watu (nani asiwajua wana mtandao), waandishi wa habari wakampamba, anajilipa na kulipa fadhila.
 
ukisoma hii thred pamoja baadhi ya comments utajua wazi kuwa hawa ni watu wenye gubu mioyoni na sio wazalendo.ni walalamikaji wasiopenda maendeleo ya nchi yetu.tumia mda wako kufanyakazi sio kuleta uzushi apa.
 
hili limeshakuwa taifa la walalamikaji.mtu anakurupuka usingizini na kuja apa na na hoja ya ajabu.mi naona mwny thred ndo hajui majukum ya raiS.anajifanya much know.rais ana watendaj chini yake ambao wanawajibika kwa hayo mambo.kuna mawaziri,makatibu wakuu ndio wanahusika moja kwa moja au mnataka kupandikiza chuki isiyo na maana km KAWAIDA YENU?RAIS ANAJUA MAJUKUM YAKE YALIYOAINISHWA KWNY KATIBA NDO MANA ALIOMBA URAIS.

Kama hauna cha kuchangia si utulie tu.
 
Jk kafanya mambo mazuri makubwa na tutamkumbuka daima.kajenga shule za sekondari kila kata nchi nzima,kajenga chuo cha dodoma,ameendelea kujenga mtandao wa barabara nchi nzima.leo ni lami kila kona ya nchi.mungu mpe maisha mema kikwete muepushe mbali na wabaya wake km hawa wa jf wenye gubu.
 
Ni ukweli ambao unasikitisha na kuumiza sana lakini ndio ukweli wenyewe.

ni kweli aisee ndiyo maana amenyamaza kimya kama vile hayupo. Hivi marais huwa wanalipwa kwa kazi wanayofanya kama ni hivyo, sasa JK huwa analipwa kwa ajili gani? Maana wananchi ambao ndiyo waajiri wake hawamuelewi kabisa. Kila kona wanamlalamikia kuwa siyo mwajibikaji. Sasa kabla kufika 2015 itabidi walau apunguziwe mmshahara isije ikawa analipwa mijihela mingi wakati utendaji wake ni karibu na sifuri!!!
 
Back
Top Bottom