Tanzania tumepigwa bao na Wakenya, Kiswahili is not the official language of EAC!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
25,744
44,112
..hivi Tanzania tuna matatizo gani ktk hii mikataba tunayosaini?

..katika nchi zote za eac Tanzania ndiyo tuna population kubwa, ardhi kubwa na yenye rutuba, na utajiri mwingine wa madini na maliasili kibao.

..sasa katika mazingira hayo does it make sense kwa m-Tanzania yeyote yule, kwamba Kiswahili is not the official language of East African Community?

..for your information my fellow Tanzanians, English is the official language of EAC, and Kiswahili has the status of "lingua-franca"!!!

..kama hivyo ndivyo viongozi wetu waliosaini hiyo makataba waliona inafaa, kwanini mpaka leo hawajabadilisha mitaala ya elimu na kukipa Kingereza uzito uleule kama ilivyo ktk shule za Kenya na Uganda?

..our leaders have known this for more than 20 yrs since these negotiations for East African Community/Federation started. to make matters even worse walitaka Federation ije mwaka 2013!!!

..tukubali tu kwamba wadogo zetu, haswa wale wanaohitimu ktk sekondari za kata, na vyuo vikuu vya yebo-yebo, wataishia kuwa wapagazi tu ktk Shirikisho la Afrika Mashariki.
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,502
Sasa wametupigaje bao mimi nilifikiri Kijaruo kimekuwa official language hapo hata mimi nisingekubali.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
25,744
44,112
Jasusi,Feedback,Gurta,

..thanks for ur responses.

..tatizo ni kwamba viongozi wetu never told us this fact.

..mimi nimejua hili baada ya kusoma kwamba maombi ya Burundi kwamba Kifaransa kiwe moja ya official languages za EAC kukataliwa.

..but it doesnt make any sense kwa kiongozi wa Tanzania kukubali Kiswahili kisiwe official language ya EAC.

..cha kusikitisha zaidi ni kwamba viongozi wameficha suala hilo. zaidi hawajachukua hatua zozote zile za kuwaandaa wa-Tanzania ku-transition toka Kiswahili kuwa official language kwenda kwenye Kiingereza.

..What if tungekubali zile kampeni za Kenya na Uganda ku-fast track East African Federation by 2013???

..halafu wengine tukipinga hii Jumuiya tunaambiwa tunaitwa majina ya kila aina.
 
Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,238
530
JK bwana unang'ang'ania 'viongozi viongozi' -- hao watu wanaoitwa viongozi hawapo katika nji hii bwana. Ila kuna watu wamepewa ofisi ili wapige madili ya kimjinimjini, miayo na kufaidi bites and VIP treatment basi. Wanajikusanya vizuri halafu wanaritaya wakiwa na hati za utumishi uliotukuka!
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
25,744
44,112
Gurta said:
JK bwana unang'ang'ania 'viongozi viongozi' -- hao watu wanaoitwa viongozi hawapo katika nji hii bwana. Ila kuna watu wamepewa ofisi ili wapige madili ya kimjinimjini, miayo na kufaidi bites and VIP treatment basi. Wanajikusanya vizuri halafu wanaritaya wakiwa na hati za utumishi uliotukuka!

Gurta,

..sasa ndugu yangu suala hili tumuulize nani?

..Raisi, Mawaziri, na Wabunge wetu wanafanya nini?

..wa-Tanzania ktk ujumla wetu tunafanya nini ili kuweza ku-compete ktk EAC??
 
mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
wangeweka hata kikamba ndo lugha ya taifa..................mana ssi ni ka gurudumu kwenye baiskeli
 
only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
..hivi Tanzania tuna matatizo gani ktk hii mikataba tunayosaini?

..katika nchi zote za eac Tanzania ndiyo tuna population kubwa, ardhi kubwa na yenye rutuba, na utajiri mwingine wa madini na maliasili kibao.

..sasa katika mazingira hayo does it make sense kwa m-Tanzania yeyote yule, kwamba Kiswahili is not the official language of East African Community?

..for your information my fellow Tanzanians, English is the official language of EAC, and Kiswahili has the status of "lingua-franca"!!!

..kama hivyo ndivyo viongozi wetu waliosaini hiyo makataba waliona inafaa, kwanini mpaka leo hawajabadilisha mitaala ya elimu na kukipa Kingereza uzito uleule kama ilivyo ktk shule za Kenya na Uganda?

..our leaders have known this for more than 20 yrs since these negotiations for East African Community/Federation started. to make matters even worse walitaka Federation ije mwaka 2013!!!

..tukubali tu kwamba wadogo zetu, haswa wale wanaohitimu ktk sekondari za kata, na vyuo vikuu vya yebo-yebo, wataishia kuwa wapagazi tu ktk Shirikisho la Afrika Mashariki.

Imenenwa sana hapa JF kuwa Tanzania haina serikali,inajiongoza...sasa kama viongozi wenyewe ndio sapuli ya Nape,JK,Wasira,mnafiki Sitta nk unategemea nini? Mimi nategemea maafa makubwa kwa taifa hili katika kila nyanja....hawa watu tunaowaita viongozi wanajau fika wanachofanya huko EAC,isipokuwa kila kitu wanaangalia maslahi ya familia zao,hawana huruma na Taifa hili na sisi masikini...Wanatuziba macho kwa kutuambia tusiogope shirikisho la EAC ni kweli hatupaswi kuogopa,lakini Je,tunaendaje huko? suala sio kuogopa aua kutoogopa.Ishu ni kuwa tumeandaliwa katika kila nyanja?
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Sasa wametupigaje bao mimi nilifikiri Kijaruo kimekuwa official language hapo hata mimi nisingekubali.

Mimi nakwambia kiwango cha kulalamika nchi hii kimefikia kwenye alarming stage. Kuna tatizo gani Kiingereza kuwa official language wakati population ya Kenya, Uganda na hapo baadae South Sudan hiyo ndiyo official language yao. Kwa nini tudhani kwamba Tanzania tuna haki ya ku-impose kile tunachokitaka? Kwanza kwa kusema official language kunabadilisha nini? Watu wa jumuiya watakuwa na uhuru wa kuwasiliana kwa lugha wanayoihitaji na kuelewana lakini majadiliano katika mijadala na mikusanyiko maalum itafanywa kwa kiingereza, kitu ambacho hata hapa Tanzania tunakifanya.

Hivi ni lazima mtu ulie lie hata kwa kitu ambacho siyo issue? Tumewachoka sasa!
 
Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
16,213
22,393
Hatari kubwa Tanzania lazima ibadili mitaala lugha ya kiingereza ichukue nafasi yake.
 
Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
4,112
2,074
Na bado hapo ni lugha tu subirini amabo mengine yataibuka baada ya jumuia hii kuanza kufanya kazi effectivelly
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
I am shocked after this revealations hakika .Tanzania hii hii tunapiga kelele kila siku na waoenda mbali wanataka kiswahili kizagae kila kona ya Nchi kumbe huko EAC hakuna kitu ?
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Hakuna la ajabu hapa. Kama mnataka kudumisha kiswahili basi msikubali miungano ili mbaki peke yenu na mkienzi kiswahili mtakavyo nyie. Ni udikteta kulazimisha mnachokitaka nyie bila kuangalia maslahi ya wengine.
 
Habdavi

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
618
413
tutakuwaje regional market kwa kutumia kiswahili wakati lugha ya biashara ni kingereza? Mimi nijuavyo the official language, yaani lugha itakayotumika kwa maandishi ni kingereza, ila lugha ya itumikayo kwa interaction, kati ya wanajumuiya ndiyo itatumika kiswahili.
 
lina Mongi

Member
May 31, 2011
34
6
Ndugu zangu Watanzania, sawa tukienzi kiswahili ndio Lugha ya Taifa letu. Lakini je tunaangalia upande wa pili? kiswahili kinatupeleka wapi? Hoteli zinafunguliwa nyingi tu,je kama watanzania hawajui Kiingereza itakuwaje?
 
M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
Official languages zinaweza kuwa hata zaidi ya mbili! South Africa wana 11 Official languages.
Tatizo tunakumbatia lugha ambayo hata haitoi fursa za sisi kujumuika na ulimwengu wa nje......achilia mbali kutojitosheleza!
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
tutakuwaje regional market kwa kutumia kiswahili wakati lugha ya biashara ni kingereza? Mimi nijuavyo the official language, yaani lugha itakayotumika kwa maandishi ni kingereza, ila lugha ya itumikayo kwa interaction, kati ya wanajumuiya ndiyo itatumika kiswahili.

Walalamishi hawajui hilo kaka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

7 Reactions
Reply
Top Bottom