Tanzania tumepigwa bao na Wakenya, Kiswahili is not the official language of EAC!

Kiswahili ni kizuri lakini kimedumaza sana watanzania to the outside world. Leo hii watu wanahitimu shahada zao hata kuandika barua ya kuomba kazi kwa kiingereza kilicho nyooka hapana. Nenda kawaweke wahitimu wetu na wa Ug na Kenya kwenye labour market wafanyiwe usaili utaona tunashindwa badly. Let us be honest jamani, achilia mbali EAC! Ni lini humu nchini watu wameomba kazi kwa Kiswahili? Ama umeenda usaili unaofanywa kwa kiswahili kwenye nyadhifa muhimu? Jibu hapana!
Mimi nafikiri, kama tayari tunakifahamu Kiswahili kwa ustadi kabisa kwanini basi tusihamie kujifunza lugha nyingine na kuitumia? Kwanini tung'ang'anie tu Kiswahili na tunakijua?
Kwa wale wanaotembea na kutafuta ajira ng'ambo wanaweza kukubaliana nami kuwa Nchi zote za kiarabu hususan U.A.E ( Umoja wa Falme za Kiarabu yenye Dubai na Abudhabi----), Qatar na nyinginezo zimetoa ajira sana kwa waafrika wengi wao wakiwa wakenya.
Hawa jamaa wako kila mahari mpaka karibuni wanafanya kazi kama walinzi ama security guard wakiwareplace wahindi na wapakistan, lakini kwanini waajiri wanawataka? Jibu kiingereza sababu kazi nyingine haziitaji elimu kubwa huko middle east bali ufahamu tu wakiingereza na wanaajiriwa. Sasa sisi bado tunalalamika - ni ujinga tu.
Jamaa wanaenda na wanaita ndugu zao, wako mahotelini mpaka top hotels in town wapo! Sisi twang'ang'ana na Kiswahili, jamaa wanaanza na security guard kesho unamuona ameingia sales keshokutwa anafanya jambo lingine! Tukisubiri serikali itufanyie tutabaki kulalama pasipo msaada!
Anyway let us wake up and run badala ya kuendelea kupiga mayowe ya usingizi wakati mda umeshasogea!!!
Mkuu wangu sijui kama wewe ni mtaalam wa ELIMU yenyewe... Kiswahili sio sababu ya kudumaza watu bali kiingereza chenyewe ndio kimedumaza ELIMU ya Watanzania na nitakwambia kwa nini:-

Nijuavyo mimi vijana wengi wanaoandika kiintgereza vizuri na hata kukisoma ni wale waliosoma wakati wa Nyerere, wakati ambao kiingereza kilikuwa lugha hivyo wanafunzi tulijifunza kuongea kiingereza, kusoma na kuandika..Sasa maadam hawa watoto waliisha ielewa lugha ya kiingereza wameweza kujenga uwezo wa kuandika kutokana na Elimu yao..Tofauti kabisa na vijana wa leo wanaokwenda shule kujifunza elimu wakati lugha ya kiingereza hawaijui..

Labda unasahau tu ya kwamba hakuna nchi yoyote duniani (nchi zilizoendelea) inafundisha wanafunzi wake kwa lugha ya Kigeni - HAKUNA isipokuwa nchi maskini tulotawaliwa....Na nchi zote hizi zipo chini sana ktk kiwango cha elimu (Literacy - ability to read for knowledge and write coherently and think critically about the written word)..
Leo hii tazama South Korea inaongoza duniani kwa masomo ya hesabu, na sayansi hawa wanasoma kwa lugha yao lakini wanafundishwa kiingereza kama lugha hivyo ni rahisi kwao kutafsiri swala toka lugha ywaliyosomea kwenda kiingereza na hata yule alojifunza Kiswahili anaweza kukupa majibu yaleyale kwa sababu anakijua kiswahili na elimu yake haipotea hata kama kasoma kwa Kikorea.

Kwa hiyo sababu za watu kuajiririwa ni za makosa kabisa kwani elimu ya mhusika haitumiki bali lugha. Na ndio maana nchi zetu maskini kwa sababu hata hizo ajira ulizozisema zinapatikana Dubai na UAE ni za security au salesmen ambazo hazihitaji elimu bali kuwasiliana na wateja..Sasa wewe Mtanzania wananchi wako asilimia 80 hawajui kiingereza unamwajiri mtu anayezungumza kiingereza kwa sababu gani?.

Na tazama kwa makini sehemu zote ambazo wanazotoa ajira kwa sababu ya lugha ni kwa sababu kuna matabaka ya wajamii wenyewe. Mtu mwenye Hotel ya Kempiski hategemei mtanzania toka kundi la asilimi 80 kuja kuwa mteja pale na hatakiwi isipokuwa wanalenga asilimia 1 ya wateja matajiri wenye uwezo mkubwa na ulimbukeni wa lugha kuja kualala pale. Vivyo hivyo tunagawanywa kwa lugha tukifikiria ni elimu ama maendeleo lakini mbona umaskini wetu hauondoki kutokana na matumizi ya lugha...

Kenya walikuwa wakitumia kiingereza kabla hata ya Uhuru, Nigeria, Ghana yaani kote huko lakini nenda kaa nao karibu uzungumze nao kiingereza.. Ni vichekesho, Accent nzito hata maneno mengine inabidi ufikirie sana wana maana gani?..Na kikubwa zaidi kiingereza hakikuboresha maisha yao bali kuwaweka ktk nafasi za utumwa zaidi (security na salesmen) kwa sababu hawakuweza kuelimika bali wanaijua lugha.

Mkuu kama umewahi kunisoma vizuri mimi sipendi kabisa kutumia kiingereza ktk mabandiko yangu kwa sababu nawalenga Watanzania walio wengi na kama mtu anataka tuongee kiingereza basi kuna wakati wake lakini sio wakati nazungumza na Watanzania wenzangu. Kusema kweli hua inanikera sana kukutana na Mtanzania anataka tuongee kiingereza baina yetu..Kwangu huu ni Ulimbukeni na kutofahamu thamani ya lugha yako..
 
Asante mkuu! Umeiweka vizuri hii, mwenye kutaka kuelewa ataelewa..
 
Hivi JF ni Jamii Forums ? Sasa hiki sindio KISWA-KINGE?
Naaam ndio ulevi wa lugha za watu kaka, huoni sinema zetu zote zina title ya kiingereza lakini lakini sinema nzima wanazungumza kiswahili halafu sinema zote za nyumbani zinazoongea kiingereza zaidi hazina soko kubwa. Muuzaji wa juu ktk soko ambaye yuko juu ni mzee Majuto - sababu?
 
Mkandara,....

..kwanza, Watanganyika tuna nafasi gani ktk ushiriki wetu ktk Jumuiya ya EAC ikiwa lugha yetu ya taifa imepuuzwa na kupewa hadhi ya chini yaani "lingua franco"?

..pili, Kiingereza ni lugha ya mawasiliano ya dunia nzima. sasa sijui kwanini sisi Watanganyika hatuipi lugha hiyo umuhimu inaostahili.

..tatu, kwanini suala hili la KIINGEREZA na siyo KISWAHILI kuwa ndiyo lugha rasmi ya EAC limefanywa siri kwa Watanyika wa kawaida?

..nne, tangu uamuzi huo umechukuliwa kumefanyika juhudi gani kuhakikisha kwamba Watanganyika wataweza kushiriki kikamilifu ktk mazingira mapya ambapo lugha ya taifa itakuwa ni Kiingereza???
 
..hivi Tanzania tuna matatizo gani ktk hii mikataba tunayosaini?

..katika nchi zote za eac Tanzania ndiyo tuna population kubwa, ardhi kubwa na yenye rutuba, na utajiri mwingine wa madini na maliasili kibao.

..sasa katika mazingira hayo does it make sense kwa m-Tanzania yeyote yule, kwamba Kiswahili is not the official language of East African Community?

..for your information my fellow Tanzanians, English is the official language of EAC, and Kiswahili has the status of "lingua-franca"!!!

..kama hivyo ndivyo viongozi wetu waliosaini hiyo makataba waliona inafaa, kwanini mpaka leo hawajabadilisha mitaala ya elimu na kukipa Kingereza uzito uleule kama ilivyo ktk shule za Kenya na Uganda?

..our leaders have known this for more than 20 yrs since these negotiations for East African Community/Federation started. to make matters even worse walitaka Federation ije mwaka 2013!!!

..tukubali tu kwamba wadogo zetu, haswa wale wanaohitimu ktk sekondari za kata, na vyuo vikuu vya yebo-yebo, wataishia kuwa wapagazi tu ktk Shirikisho la Afrika Mashariki.

kalaga bao, watoto wa wakubwa wachoma kimombo kama kawa. Mimi sidanganyiki, viva EAC for selecting english.
 
..hivi Tanzania tuna matatizo gani ktk hii mikataba tunayosaini?

..katika nchi zote za eac Tanzania ndiyo tuna population kubwa, ardhi kubwa na yenye rutuba, na utajiri mwingine wa madini na maliasili kibao.

..sasa katika mazingira hayo does it make sense kwa m-Tanzania yeyote yule, kwamba Kiswahili is not the official language of East African Community?

..for your information my fellow Tanzanians, English is the official language of EAC, and Kiswahili has the status of "lingua-franca"!!!

..kama hivyo ndivyo viongozi wetu waliosaini hiyo makataba waliona inafaa, kwanini mpaka leo hawajabadilisha mitaala ya elimu na kukipa Kingereza uzito uleule kama ilivyo ktk shule za Kenya na Uganda?

..our leaders have known this for more than 20 yrs since these negotiations for East African Community/Federation started. to make matters even worse walitaka Federation ije mwaka 2013!!!

..tukubali tu kwamba wadogo zetu, haswa wale wanaohitimu ktk sekondari za kata, na vyuo vikuu vya yebo-yebo, wataishia kuwa wapagazi tu ktk Shirikisho la Afrika Mashariki.

For your information Mh Jokakuu Kiswahili sio official language ingekuwa kishahili ni official language basi hata katiba ya Muungano isingali andikwa kwa lugha ya kiengereza ingeandikwa kwa lugha ya kishwahili kwa vile asilimia %80 ya Watanzania wanazungumza kishwahili safi hususani Zenj.
 
Mimi nakwambia kiwango cha kulalamika nchi hii kimefikia kwenye alarming stage. Kuna tatizo gani Kiingereza kuwa official language wakati population ya Kenya, Uganda na hapo baadae South Sudan hiyo ndiyo official language yao. Kwa nini tudhani kwamba Tanzania tuna haki ya ku-impose kile tunachokitaka? Kwanza kwa kusema official language kunabadilisha nini? Watu wa jumuiya watakuwa na uhuru wa kuwasiliana kwa lugha wanayoihitaji na kuelewana lakini majadiliano katika mijadala na mikusanyiko maalum itafanywa kwa kiingereza, kitu ambacho hata hapa Tanzania tunakifanya.

Hivi ni lazima mtu ulie lie hata kwa kitu ambacho siyo issue? Tumewachoka sasa!
Inamaana huelewi umuhimu wa lugha kuwa official? kuna tatizo gani kuwa na lugha mbili official? mbona kuna nchi nyingi tu zina official language zaidi ya moja?
Halafu ni mijadala ktk mikusanyiko gani TZ inafanywa kwa kiingereza? au huijui vizuri TZ.
 
Ndugu zangu Watanzania, sawa tukienzi kiswahili ndio Lugha ya Taifa letu. Lakini je tunaangalia upande wa pili? kiswahili kinatupeleka wapi? Hoteli zinafunguliwa nyingi tu,je kama watanzania hawajui Kiingereza itakuwaje?
Kama hatuoni umuhimu wa kiswahili, basi tusione pia umuhimu wa sarafu yetu ya shilingi, mbona kuna baadhi ya nchi zimeamua kutumia US dollar baada ya kukuta sarafu zao zinayumba kama ilivyo yetu.
 
Inamaana huelewi umuhimu wa lugha kuwa official? kuna tatizo gani kuwa na lugha mbili official? mbona kuna nchi nyingi tu zina official language zaidi ya moja?
Halafu ni mijadala ktk mikusanyiko gani TZ inafanywa kwa kiingereza? au huijui vizuri TZ.
Nchi gani hizo zenye lugha mbili Official?
A hint ni WATU wanaojenga lugha na sio Lugha kujenga watu...ukinielewa hapo hutaipata nchi unayotaka kusema.
 
I am shocked after this revealations hakika .Tanzania hii hii tunapiga kelele kila siku na waoenda mbali wanataka kiswahili kizagae kila kona ya Nchi kumbe huko EAC hakuna kitu ?
Unashangaa nini wakati hata hapa TZ kiswahili sio official language? Hapa kiswahili ni lugha ya taifa lakini official language ni English.
 
Official languages zinaweza kuwa hata zaidi ya mbili! South Africa wana 11 Official languages.
Tatizo tunakumbatia lugha ambayo hata haitoi fursa za sisi kujumuika na ulimwengu wa nje......achilia mbali kutojitosheleza!
Wewe unataka ulimwengu wa nje upi? kama ishu ni ulimwengu wa nje basi tukubali pia kuwa tukubaliane kwanza tunataka kuelekea kwenye ulimwengu upi? wa kiingereza, kifaransa, kiarabu, kireno au kihispania?
 
Kenya wanazungumza Kiswahili. Tena wamekishupalia sana siku za karibuni. Jeshi la Uganda tangu enzi za ukoloni limekuwa la Kiswahili. Tunaona aibu gani kupendekeza Kiswahili kiwe lingua franca na Kiingereza kishike nafasi ya pili. Siyo udikiteta. Kote Rwanda na Burundi kuna Waswahili. Tatizo liko wapi? Waache Wanigeria, Ghana, Sierra Leone, na ECOWAS yao watumie Kiingereza. Sisi tulikuwa na nafasi ya kipekee kukuza lugha yetu ambayo mpaka AU inatambuliwa leo wewe unatuambia ni udikteta? Achana na kasumba hii ya ukoloni mamboleo.
Safi sana! napenda watu ambao wana ufahamu usiokuwa na shaka ktk mambo muhimu. Achana na hao wenye upeo wa kuunga hawajui nini maana ya lugha.
 
Mbopo,kitu kuwa official kina implication kubwa sana,unajua mfumo tulionao sasa mpaka tuje tubadilike na official language mpya? Duh kiingereza kuwa lugha ya taifa rasmi! Umefikiria vizuri matokeo yake Mbopo?
Kweli mkuu, Mwambie huyo!!! kuna watu wanatumia taarifa za magazetini kuamua mambo. Hajui anaongea nini, yeye anadhani watz wakiongea kiingereza kila mahali basi watakua wameelimika na hivyo wataweza kushindana vizuri ktk EAC.
 
Nakumbuka mwaka jana serikali ya Tanzania ilitangaza kwamba lugha rasmi ya mawasiliano serikalini itakuwa kiswahili lakini siku chache baadae tulishuhudia kwenye vyombo vya habari watumishi wa serikali wakiendesha makongamano na warsha kwa lugha ya kiingereza na mkuchika hakutoa kauli yoyote hadi leo na mawasiliano yanaendelea kuandikwa kwa kiinglish.

Viongozi wetu hawajawahi kuishi kwenye maneno yao. Hata kama si lazima kiswahili kuwa lugha rasmi ya mawasiliano lakini serikali ilipaswa kuwaandaa watanzania kukabiliana na makubaliano hayo. Serikali inaona shida gani kuruhusu kiinglish kutumika kuanzia shule za awali kama lugha ya kufundishia ili kuondoa hili zogo? au kwakuwa watoto wao wanasoma st.academia na kisha ulaya na marekani!
Kwani inaona shida gani kutumia kiswahili mpaka elimu ya juu halafu na kupiga marufuku matumizi ya kiingereza ktk ofisi za serikali?
 
We should dare face it once and for all ... Kazi ya kiswahili kama lugha moja ya Taifa ... Imeshafanyika .... imemalizika na kutufikisha mahali ..hatuwezi kuendelaea bila lugha ya kiingereza kupewa umuhimu sawa na Kiswahili...!!
Mbona nchi kama Ivory coast, Morocco na Cape verde zimeendelea sana kutuzidi japo hawajui kabisa kiingereza? Huwezi kusema hatuwezi endelea bila kiingereza bwana! unless ututhibitishie kuwa nchi zote zinazopiga hatua wanafahamu kiingereza.
 
Nchi gani hizo zenye lugha mbili Official?
A hint ni WATU wanaojenga lugha na sio Lugha kujenga watu...ukinielewa hapo hutaipata nchi unayotaka kusema.
Kwa nilivyosoma post zako nadhani hujanielewa, kimsingi niko pamoja nawe kimtazamo. Nilimaanisha kwanini sasa EAC isiwe na lugha official mbili kwa maana ya kiswahili na kiingereza. Hata hivyo nchi zenye lugha official zaidi ya moja ninazozifahamu ni: Cameroon, South Africa, Canada,Eritrea na DRC
 
Mkuu Mkandara ..

Kiswahili kinahitaji ... Wa Kukisimamia ... Kukitetea... Kukisimamia si kama Lugha tu ..lakini na tamaduni zote za nidhamu na mausiano sahihi ya kijamii ..kwa sasa hayupo...
Tunatakiwa tumtafute wa kukisimamia na sio kuamua kukiua. Mbona alama zingine za utaifa kama wimbo, bendera na Twiga hamuongelei kuzifuta ila mnona sawa kuua kiswahili? Kama vipi acheni hata huo mchakato wa vazi la taifa maana kwenu halina maana.
 
hapa tumeshindwa,sasa sijui ile kampeni ya umoja wa Afrika (AU) tutaweza kukifanya kiswahili ndio lugha ya Afrika.?
Kiswahili kilishaingizwa kwenye lugha za Africa zamani mno na aliyekuwa wa kwanza kukiongea kwenye mkuatano wa AU alikuwa rais wa msumbiji wa wakati huo Joachim Chissano, kama sijakosea ilikuwa mwaka 2003.
 
Mbona nchi kama Ivory coast, Morocco na Cape verde zimeendelea sana kutuzidi japo hawajui kabisa kiingereza? Huwezi kusema hatuwezi endelea bila kiingereza bwana! unless ututhibitishie kuwa nchi zote zinazopiga hatua wanafahamu kiingereza.

Pia muulize China, Korea ya Kusini na Japan wanatumia lugha gani vile? Na maendeleo yao yakoje vile?
 
Back
Top Bottom