Tanzania tulikosea wapi na Kenya walipatia wapi?

Ulivyo anza mada yako inaonyesha kwamba huijui Tanzania (Tanganyika) kabla ya uhuru na huijui Kenya kabla ya uhuru! Pia hujui Tanganyika na Kenya zilivyopata uhuru. Ukiyajua hayo, hutalinganisha Tanzania na Kenya mpaka unakufa!
Anzisha mada yako na uweke hayo unayosema, sawa? Ni ujinga kuparamia mada za watu huku ukijifanya mjuaji kumbe huna lolote!! Huoni watu wanachangia mawazo yao kwa maana ya kwamba wameelewa kunachozungumzwa? Au wawaona woootee wanachangia ni vilaza kama wewe?
 

Naungana na wewe, kuongezea ni kwamba;

(1)kenya ilikuwa ni settler colony kwamba viwanda vingi vilijengwa kwao na miundombinu,hata social services zilikuwa impoved by that time na hata wazungu wamechangia pakubwa sana ktk uchumi wao

(2)Capitalism as their national ideology na siku zote penye ushindani maendeleo yanakuja haraka ukilinganisha na mwendo wetu slow ila sio kwamba hatutafika waliko ila ni swala la mda tu
 
Daah huu nao ni ukweli mchungu...
 
elimu ipi unayoizungumzia!!

hii ya wakoroni inayotambua maendeleo ya nchi kwa kuangalia GDP,isiyokupa nafasi hata kufikiri nje ya hapo!!!
Elimu ya kuweza kujitegemea, kuvumbua visaidia maisha, ubunifu na uweledi mkubwa kwenye kuanzisha na kuendesha viwanda, makampuni, mashamba makubwa ili kutengeneza ajira. Siyo elimu ya kukariri na kufaulia mitihani... Elimu ambayo unaweza kwenda kufanya kazi popote duniani etc etc
 
Ni Kibra. Zamani ilikuwa yaitwa Kibira. Sina haja ya kusoma utakayoyaandika ikiwa hata jina la mahali lakuchenga. Najua wataka kuandika nini. Watu wengi wanaotoa mfano wa umaskini Kenya wanazungumzia ubaya wa Kibra. Lakini hapa Tanzania tuna Kibra ngapi? Umekwenda vijijini wewe uone Maisha ya watu huko. Kibra ilianza kama mji-tnzu wa Nairobi unaowapokea watu wanaotoka vijijini kuja mjini kutafuta Maisha. Hiyo ni miaka ya 50. Ina historia ndefu ya umaskini na deprivation. Lakini hivi karibuni serikali imetengeneza sana na inazidi kuboreshwa.
Na si kweli kuwa foreigners pekee ndiyo wana Maisha mazuri.
 
Hivi hatuwezi kufanya dua mwezi mzima ili taifa letu liondokane na umasikini na tuingie moja kwa moja kwenye kundi la nchi zinazoongoza kwa uchumi wa juu? Yaani tuingie G8 countries??
 
Huu ni mfano mzuri wa tatizo la elimu la Tanzania, unaweza kukuta huyu ana digrii 2 au 3....
 
Halafu watanzania wakaamua kuharibu green house ya Mtanzania mwenzao aliyekuwa anauza maua na Green beans nje ya nchi na kulipa kodi na kutoa ajira. Kisa tuu tafauti za kisiasa za kijinga. Badala ya kumpiga faini ili waendelee kupata kodi mbalimbali wao wakaamua kumuua ng'ombe wa maziwa.
 
Hata wakenya wenyewe wakiisoma habari hii, watakushangaa sana mwandishi.
 
Matatizo yote ya Tanzania yametokana na Nyerere na misimamo yake ya hovyo isiyokuwa na kichwa wala miguu.
Kimsingi hatutakiwi kujilinganisha na Kenya hata kidogo maana ukiangalia factors zote za kuwezesha maendeleo labour & capitals kwa maana ya resources tunawazidi Kenya kwa mbali sana.

Kama wakenya ndio wangekuwa na nchi yetu ya Tanzania sasa hivi wangekuwa zaidi ya S.A.imagine nyerere alidhinisha katiba yenye mapungufu ili imsaidie katika kipindi chake cha uongozi na alikiri kabisa katiba ina maoungufu na alikuwa na uwezo was kubadilisha lakini akaamua kuiacha hivyo hivyo.

Uoga wa Watanzania ambao unatokana na ujinga ulipitiliza ,kwa sehemu kubwa umesababishwa na nyerere-ambapo alijiona yeye ndio kila kitu.laiti kambona asingefanya upumbavu wake kipind like ambapo tayari dola ilikuwa imisha mponyoka nyerere Leo hii tungekuwa nbali sanauw
 
The education system in the UK is divided into four main parts, primary education, secondary education, further education and higher education. Children in the UK have to legally attend primary and secondary education which runs from about 5 years old until the student is 16 years old.

Education System in Zambia
The Zambian education system has a 7-5-4 structure, namely 7 years at primary school, 2 and 3 years at junior and higher secondary school respectively, and 4 years at university for undergraduate degrees.

The system of education in Uganda has a structure of 7 years of primary education, 6 years of secondary education (divided into 4 years of lower secondary and 2 years of upper secondary school), and 3 to 5 years of post-secondary education, according to Education News Uganda The government of Uganda recognizes
 
Mkuu kama unasema kuwa Kenya siyo foreigners tu ndiyo wana maisha mazuri basi huijui Kenya. Swala la Kibira kuwa ni Kibra hilo silifahamu so yaweza kuwa kweli au si kweli, unajua watu kama waalimu, manesi, drivers and the like kwa Kenya wanaishi wapi? Anyway sipendi kuzungumzia sana hiyo nchi kwani hainihusu lakini ntakuja kuleta story ya niliyoyaona Kibira(wewe waita kibra).
 
Naona umepandwa na wazimu, hizi hapa takwimu za world bank na IMF waliosema nyinyi ni low middle income na mkashangilia.

i) 32% ya Kenya ndio maskini yani wanatumia chini ya $1.9 kwa siku, Tanzania ni 60% kwa sababu hiyo idadi wanaishi chini ya $1.9 kwa siku (IMF).

ii) Kenya raia wana afya nzuri kulingana na world bank na WFP. Tanzania inaongoza eac kwa kuwa na watoto wenye utapia mlo ingawa mnapanda chakula na kuuza mpaka kenya na watoto ambao akili zao hazikui vizuri kwa kukosa lishe bora. (WFP na WHO).

iii) Ikifika kwa elimu hata usitaje ukanda huu ni Uganda tu ndio infata Kenya.(University rankings, IMF na World bank).

iv) Kwa kutimiza malengo ya maisha Kenya ni namba ya tatu afrika ikifata sychelles na mauritius.Yani mtoto akizaliwa na kusoma Kenya ako na 62% chance ya kutimiza malengo yake kwa maisha. (Human capital index report 2020)

v) Mkenya wa kawaida anaishi miaka 4 zaidi kushinda mtanzania (WHO).

v) Kwa inequality Tanzania inashinda Kenya, Tanzania iko na millionaires wengi kushinda kenya lakini pia 60% ya watu Tanzania ni maskini wa kutupwa. (IMF poverty report). Tanzania bado iko katika nchi 28 maskini kabisa duniani.

vi) Kwa miundo mbinu Tanzania iko chini sana, port ya mombasa (2.7 million teus capacity) kwa sahi ni mara 2 ya port zote nne za Tanzania nikiunganishwa na bado inazidi kupanuliwa itafikia 4 million teus mwaka 2022 december. Kenya iko na bara bara kubwa kushinda Tanzania na sahi tunajenga flyover highway ya 27km ikipita kati kati ya jiji la Nairobi kutoka kwa uwanja wa ndege.

vii) Tanzania na burundi zinaongoza eac kwa kuwa na watoto wanaofariki kabla ya kufika miaka 5. Hapa tena lishe bora na usafi iliangaziwa na World bank.

Kwa hivyo najua unataka kujipa consolation lakini hiyo propaganda yenyu yote ni kelele.
 
Salute kwako mkuu [emoji120][emoji120][emoji106][emoji106]... Yaani hapo uliposema kujifunza kwa aliyekuzidi is everything, hata kwenye maisha yetu, nina mifano: katika maisha nimekutana na jamaa mmoja, pamoja na tabia yake ya kujisikia, niliweza kujifunza meengii sana na kujikwamua kiuchumi kutoka kwa huyo jamaa. Mara ya kwanza kwenda abroad kwenye workshop fulani tulikuwa Waafrika 2 tu mimi na Mkenya, the rest ni wazungu na from Asia. It was my first presentation outside, Sasa nikaamua kuonyesha yule Mkenya my presentation kwani ili same field but tofauti ni nchi tuu. Yule Mkenya akaniambia nifanye presentation kwake as if nawasilisha kwenye warsha,na nilipomaliza tukaanza kujadili, aise yaani tuliifumua whole presentation na ikabidi jamaa zangu wanitumie some good and new pics. Yaani niseme kama siyo yule Mkenya kwa kweli ningeadhirika sana kwani maandalizi yangu was very poor na hayakuwa yanajibu objectives za ile workshop. Alinipa many techniques na kufanya many rehearsals mpaka ilipofika siku ya actual presentation it was superb, and eventually project yetu ilipata funds kwenye hiyo component as a result of the presentation. So the guy is one of the family friends todate na tunatembeleana sanaaaaa, kwao ni Nyeri. So mimi mtu aliyefanikiwa ndiye kwa kweli napenda sana kujifunza alifikaje hapo.
 
Hawa ndio top 10 kwa utajiri kenya
i) Vimal shah
ii) Jimnah mbaru
iii) Peter munga
iv) James Mwangi
v) Chris Kirubi
vi) Bhimji Depar shah
vii) Naushad Merali
viii) Mama Ngina Kenyatta
xi) Manu Chandaria
x) Uhuru Kenyatta.

Kwa hio list hakuna foreigner wote ni wakenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…