Tanzania Taifa kubwa, Magufuli baba lao

Tanzania Taifa kubwa, Magufuli baba lao

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Mabibi na mabwana kutokea taarifa za habari jana na pia baada ya kujiridhisha:

He! Kumbe yule mgeni wetu mpendwa kabisa, mwalikwa tokea pande za pale Burundi aliingizana nchini kwa kutumia moja ya madege yetu yale mapya mapya ya ATCL chapa ya twiga?

Ikizingatiwa uwanja wa ndege Bujumbura ungali umefungwa kutokana na yale mambo yetu ya kujicoronize, yaonyesha dege letu lile lilifanya safari mahsusi kwa ajili ya kutuletea ugeni ule ugeni wetu.

Kweli mgeni njoo, wenyeji tupone. Tunasubiri.

Ama kwa hakika tunayo sababu ya kutembea kifua mbele kwa kuwa na uwezo wa kuwazukia wageni wetu huko huko waliko na kuanza kuwakaribu tokea makwao.

Hatuko vibaya. Mambo yetu kama uraya uraya vile!

Nani kama sisi?

Naamini yule amekuja kwa hisani yetu.

Hakulipa hata ndururu!
 
Burundi watakuwa ni ndugu zetu wa damu:

1. Wiki ya simba timu mwalikwa toka Burundi.
2. Wiki ya yanga timu mwalikwa toka Burundi.
3. Taifa star kujipima nguvu timu mwalikwa toka Burundi.
4. Kocha taifa star Mrundi.
5. Tufuate wageni na dege letu - Burundi.
6. Simba au yanga mle wachezaji nao imekuwa warundi warundi.
7. Nk, nk.

Kwamba dege hili litafanya safari 4 Tanzania - Burundi kwa ajili ya ugeni huu si bure!

Tutakuwa na vinasaba husika mahali.
 
Burundi tukiwaambia iwe kwenye muungano kama wa Zanzibar na Tanganyika,mbona kesho tu asubuhi na mapema wanakubali.
 
burundi ni nchi rafiki

Labda ungesema ni nchi ndugu au nchi wenye misimamo sawa kuelekea wale wenye mawazo tofauti na watawala.

Nchi kama hizo nadhani watakuwamo pia Uganda, Zimbabwe, Belarus, Ivory Coast na wale jirani zetu wengine.

Hata hivyo: "Kama wageni tumekwama hadi wengine tumewafuata kwa gharama zetu pana kitu fyongo jombi."
 
Burundi tukiwaambia iwe kwenye muungano kama wa Zanzibar na Tanganyika,mbona kesho tu asubuhi na mapema wanakubali.

Zanzibar? Waulize wazanzibari wenye nchi yao.

Kufuata mgeni kwa gharama zetu ni dalili za ukata mkali wa wageni uliopindukia.

Inconceivable!
 
Kuna dhana inajengwa huku ya hovyo lkn inaweza ikawa na kajiukweli ndan yake kwa anayemkumbuka yule mmarekani aloitawala Soviet na kuisambaratisha aweke humu
 
Tupo Uchumi Wa Kati
Tupo Kwenye Light Track
Tembeeni Kifua Mbele
😁😂😅😄😄😄😃😀😁😂🤣🤣😀😀😀
Siri Imefichuka, Nitoboe, Toboa!!
 
Zanzibar? Waulize wazanzibari wenye nchi yao.

Kufuata mgeni kwa gharama zetu ni dalili za ukata mkali wa wageni uliopindukia.

Inconceivable!
Sio kweli, Wazanzibari wamejaza magorofa Kariakoo,Ilala na Magomeni. Wamesambaa Bara na Visiwani wanafanya biashara za used kutoka Zanzibar. Wanafurahia muungano wetu adhim.

Zanzibar ipo salama kwasababu ipo ndani ya muungano. Nje ya muungano Zanzibar haipo salama. Pia Burundi ni hivyohivyo ikiwa kwenye muungano na Tanzania itakuwa salama na amani.
 
Wenye maghorofa na biashara huko ulikotaja unadhani ni wangapi?

Kwani unadhani kuwa Zanzibar hawautaki ni habari mapya?

Unadhani waliouawa kule wameuawa wakiulilia huo unaouita adhim?

Kawaulize kina Jiwe, Bashiri, chaku na hata huko huko Zanzibar kwenyewe. Watakwambia.
 
Napendekeza Burundi ijiunge na JMT, pia comoro maana naona tuna mahusiano nao mazuri.

Sio mbaya tukaongeza watu JMT nako zile zinazoitwa kero za Muungano zipungue.
 
Napendekeza Burundi ijiunge na JMT, pia comoro maana naona tuna mahusiano nao mazuri.

Sio mbaya tukaongeza watu JMT nako zile zinazoitwa kero za Muungano zipungue.
Kuwa serious mkuu Zbar ndugu zetu watoto wa mama mdogo wanatutoa jasho , inasemekana wapo watawala wachache wana vinasaba vya huko tunajuta kwa kusambaratisha umoja wa taifa letu kwa kipindi kifupi kulikoni tukiwafungulia milango??
 
Back
Top Bottom