Tanzania: Serikali yaagiza faru toka Uingereza!

iweje tuwakodishe wakati hawa wanyama ni adimu?huoni serikali ilikosa mapato kwa wanyama hao kukaa uk?nani aliidhinisha ukodishaji huo?je wanyama wangapi tumewakodisha nje ya nchi na kwa idhini/maslahi ya nani?
Hii hapa nukuu kutoka kwa mmojawapo aliyekuwepo kwenye sherehe hizo za kuwarudisha vifaru:

Waheshimiwa: jana tulikuwa Mkomazi National Park kupokea vifaru watatu kutoka Uingereza walikokuwa wamepelekwa kuzaliana kwenye mazingira salama. Hapo mtaona Balozi wa Grt Britain na Waziri wetu Balozi Kagasheki na baadhi yetu waalikwa. DHL walichangia Boeing 757 kuwaleta kwenye macontainer matatu hadi KIA. Kuna ujangiri wa kutisha sasa hivi juhudi zisipofanyika tutajikuta hatuna wanyama wote wameuliwa. Tunaomba mchango wenu wa hali na mali, yakiwamo mawazo.
Nadhani hiyo itakupa jibu kwa swali lako.
 
faru

SGR_Jan11_hero.jpg

Vifaru

vifaruvyakijeshi.jpg
mkuu kiswahili changu kinaniambia kuwa wingi wa faru ni vifaru.hebu weka majina ya kizungu tutaelewana.
 
Mkuu meningitis Usijali .. huko ndio tunakoelekea ...

Baadae watoto wetu watakuwa wanapanda ndege kwenda Ulaya kwa ajili ya kuangalia Twiga maana watakuwa wameshaisha kabisa Tanzania. Maana viongozi wetu wanauza kila kitu (Twiga, Madini, Gesi, Ardhi) mpaka sisi wote wameshatuuza na pia tuna madeni ya hatari na hata watoto wetu ambao bado hawajazaliwa na wenyewe wanadaiwa.

Kwa hiyo Mkuu usijali ndio mwanzo huo! & ndio faida ya kuwa na Viongozi wasiokuwa na Uchungu na Nchi yao.
 
Je ndege iliyowaleta inarudi na nini uk? Jiulize kwa makini
 
Hii hapa nukuu kutoka kwa mmojawapo aliyekuwepo kwenye sherehe hizo za kuwarudisha vifaru:
mkuu!kuna Waheshimiwa: jana tulikuwa Mkomazi National Park kupokea vifaru watatu kutoka Uingereza walikokuwa wamepelekwa kuzaliana kwenye mazingira salama. Hapo mtaona Balozi wa Grt Britain na Waziri wetu Balozi Kagasheki na baadhi yetu waalikwa. DHL walichangia Boeing 757 kuwaleta kwenye macontainer matatu hadi KIA. Kuna ujangiri wa kutisha sasa hivi juhudi zisipofanyika tutajikuta hatuna wanyama wote wameuliwa. Tunaomba mchango wenu wa hali na mali, yakiwamo mawazo.
Nadhani hiyo itakupa jibu kwa swali lako.

mkuu!heshima sana!kuna baadhi ya maswali hujajibu.mfano,nani aliidhinisha wanyama hawa adimu kupelekwa uk?
Unataka kuniambia uingereza ndio sehemu salama ya kutunzia wadudu hawa?why not kenya au SA au zimbabwe?usalama unaosema ni dhidi ya majangili tu au mazingira?
This is too low!!kwa hiyo tumeshindwa kulinda wanyama wetu,ndivyo unavyotakaniamini!
 
mkuu kiswahili changu kinaniambia kuwa wingi wa faru ni vifaru.hebu weka majina ya kizungu tutaelewana.

ninavyofahamu mimi majina ya vitu umoja wake huanzia na "ki" na wingi wake na "vi" mfano;

kiatu-viatu
kisu-visu
kifaru-vifaru
kituo-vituo
kiwanja -viwanja

n.k

hao wanyama hujulikana kama "FARU" na "KIFARU" ni zana ya kijeshi
 
mkuu!heshima sana!kuna baadhi ya maswali hujajibu.mfano,nani aliidhinisha wanyama hawa adimu kupelekwa uk?
Unataka kuniambia uingereza ndio sehemu salama ya kutunzia wadudu hawa?why not kenya au SA au zimbabwe?usalama unaosema ni dhidi ya majangili tu au mazingira?
This is too low!!kwa hiyo tumeshindwa kulinda wanyama wetu,ndivyo unavyotakaniamini!
Mkuu Meningitis,
Kwa sasa naweza tu kujibu baadhi ya maswali yako. Kenya, Afrika Kusini na Zimbabwe zote zina matatizo yale yale tuliyo nayo sisi Tanzania: poaching. Sasa kama ni nani aliyeidhinisha hawa wanyama wapelekwe Uingereza sijui. Ngoja nimtafute jamaa niliyewaletea nukuu yake hapo juu kwa sababu yeye alikuwepo kwenye sherehe hizo, nimuulize kama ana ufafanuzi zaidi kwa nini waliwapeleka Uingereza. Ndio maana naipenda JF. Ni hazina ya hekima.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Je ndege iliyowaleta inarudi na nini uk? Jiulize kwa makini

Itarudi na Vinyonga adimu wenye pembe moja wa pale Uluguruni Morogoro ili wakazaliane huko,maana majangiri wanawamaliza wale vinyonga. UK wanatunza hata wale Mbega wekundu pale kilombero milima ya Udzungwa. Kuna mijitu inakula kila kitu kitambaacho juu ya nchi,hadi hawa nyani (mbega wekundu) wanakaribia kupotea Tanzania.
 
Mkuu imenishitua nikabaki kucheka, ndio maana nahisi huenda ni vifaru wa kizungu!

Kiongozi, kuna mdau anasema kuwa vifaru walikuwa Uingereza kwa muda ambapo walipelekwa huko kujufungua kwenye "mazingira salama". Nadhani hapa tumekwisha maana wakubwa wakishikwa na mafua wanaamkia Apollo India, na sasa vifaru wakifikia muda wa kujufunguwa wanapelekwa Uingereza!
 
Mkuu Meningitis,
Kwa sasa naweza tu kujibu baadhi ya maswali yako. Kenya, Afrika Kusini na Zimbabwe zote zina matatizo yale yale tuliyo nayo sisi Tanzania: poaching. Sasa kama ni nani aliyeidhinisha hawa wanyama wapelekwe Uingereza sijui. Ngoja nimtafute jamaa niliyewaletea nukuu yake hapo juu kwa sababu yeye alikuwepo kwenye sherehe hizo, nimuulize kama ana ufafanuzi zaidi kwa nini waliwapeleka Uingereza. Ndio maana naipenda JF. Ni hazina ya hekima.

naamini poaching hufuata pale wanyama walipo.sidhani kama uingereza nifree from poaching!
 
Wale walioitwa faru wa Jk walionunuliwa bil 7, wawili kati ya watano wamekwisha uliwa
 
naamini poaching hufuata pale wanyama walipo.sidhani kama uingereza nifree from poaching!

Meningitis,
Think again. Uingereza hawana mbuga za wanyama. Hawa faru waliwekwa kwenye controlled environment kama vile zoo.
'They were much safer there than in South Africa, Kenya or Zimbabwe.
 
Duuuh aiseee kua uyaone. Hawa jamaa sijui wanatuonaje miAfrica!!!!! Kesho usishangae kusikia serikali inalipa bilioni 200 kukodi mlima Kilimanjaro kutoka kwa Waingereza. Kwa uchungu nilionao kwa haya mauzauza natamani niwe najichapa viboko 6 asubuhi nikiamka na 6 wakati wa kulala, mpaka hapo tutakapokombelewa kutoka kwa hawa mabwanyenye.
 
Taarifa zaidi kuhusu kwa nini vifaru walipelekwa London:
Walipelekwa London kuzaliana, huku they are really endangered. Sasa hivi wamebaki sabini na ambapo wakati wa uhuru walikuwa alfu 9. Mwaka jana walikuja wanne toka Prague na kabla ya hapo walikuja watatu toka Kruger. Yes, originally walitoka hapa, ema Tarangire au Mkomazi kwenyewe.

cleardot.gif
 
ujangili dhidi ya tembo ni mkubwa sana!sasa nataka kujua tuna tembo wangapi nje ya nchi?
 
Back
Top Bottom