Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,829
Katika jitihada za kuvutia watalii, hifadhi ya Mikumi ina mpango wa kurejesha faru ambao walotokomezwa na ujangili miaka ya 1980 na 90.
Faru ambao wako kwenye kundi la wanyama watano wakubwa zaidi wanakosekana Mikumi. Faru wawili wa mwisho walionekana mikumi zaidi ya miaka 30 iliyopita upoteaji wake ukichagizwa na ujangili.
Hii sio mara ya kwanza, mwaka 2010, faru walipelekwa mbuga ya Serengeti kutoka Afrika Kusini na mwaka 2019 faru tisa walipelekwa tena Serengeti kutoka Afrika Kusini.