View attachment 838489View attachment 838490View attachment 838491
Kiza Besigye na wafuasi wake wakichezea kichapo huko Uganda,wamarekani kimyaa!!.
Wamarekani Wanasema kwa sababu sisi tulikua tumefikia pazuri sana Kidemokrasia na tulifikia pazuri sana kwenye huduma za jamamii pamoja na kuwa Uhuru mapungufu yalikuwepo.
Ndio maana tulipata misaada mingi ya maendeleo ya afya ,barabara,elimu , Umeme n.k.
....Sasa awamu ya Tano inashindwa nini kuamua siku moja kufanya Uchaguzi wa mfano barani Afrika kwa kulinda kura na maamuzi ya wananchi ili ijue na kujitathimini kama kweli wanakubalika au wana mahali wanakosea au wananchi hawajawaelewa vizuri.
....Mpaka Marekani Sasa wanatuonya mana tunarudi nyuma na kuwa watu wasiojitambua utu wao.
Wananchi wema kabisa wanaenda kupiga kura wakiwa hawajabeba hata Kalamu mfukoni lakini wanazingirwa na mabunduki na mabomu. Aibu kubwa kwa ubaya tunaotendeana wanadamu kama vile tutaondoka na Mali duniani kwenda nazo ahera.
Tunagombania Rasilimali zetu wenyewe kwa kutaka madaraka. Kisa tu huko kuna mishahara minono na heshima kubwa.
Unafikiri tungekiwa wajamaa kweli kama tunavyoudanganya ulimwengu nani angekua na uroho huo wa madaraka?
Uroho upo kwa sababu wanajua ubepari upo kupitia madaraka mana wao ndio wenye mahela mengi na mamlaka makubwa.
DC aliyeteuliwa anakua na madaraka makubwa kuliko Mbunge aliyechaguliwa. Na sio madaraka tu lakini anaweza kutoa tu amri ya ajabu ya kukamatwa mbunge na kuwekwa ndani masaa 48. Haya ni mapungufu ya wazi ya kuonyesha kuwa bado tunahitaji kusikiliza zaidi maoni ya watu wenye akili huru.