1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,304
Kwa hiyo majeshi yetu yako Kongo kwa ajili ya Kulinda wezi toka Marekani ?Wanaochukua madini ya kongo unawajua?
.....Kama tatizo ni hao wezi tena wazungu wa Magharibi ,kwa nini Majeshi yetu yasiwachakaze hao wezi mchezo ukaisha?
Acheni utani bhana.
.....Vita za Afrika zinatokana na viongozi waroho wa madaraka wanaotumia majeshi kuua watu na kutesa watu kwa sababu ya kupenda kufia madarakani na rafiki na ndugu zao.
Demokrasia ya kweli na haki sawa itaondoa vita dunia. Mana kila MTU ataipenda nchi yake kwa moyo wote.
Jiongeze acha siasa za kujenga chuki dhidi ya binadamu wenzako.
Dunia ilishaondoka huko kwenye hizo siasa ndio maana Ufaransa inageuka kuwa Tawi la Bara la Afrika.
Watu wanaishi popote alimradi kuna Uhuru na kujali haki na utu wa wanadamu.
Hii mambo ya kuona kuwa wazungu ni wezi tu ni ujinga na Propaganda za kijinga za kuhalalisha uhalifu dhidi ya binadamu.
Watu wanatuonya kuwa hayo tunayoyafanya yatapoteza amani ya nchi yetu na kuruhusu wezi kuvamia nchi yetu badala yake tunakua wakali badala ya kurekwbisha makosa ili tuwe na amani zaidi.
Ukweli ni kwamba Watanzania tukipendana na kuungana bila kubaguana hakuna Muzungu wala Muchina atakayeivamia nchi yatu na kuiba rasilimali zetu milele. Lakini tukichukiana na kulazimisha watu wanaovaa nguo za rangi Fulani tu ndio wafaidi mema ya nchi sidhani kama tutafikia kuzuri.
Sioni sababu ya kutisha ,kuteka ,kutesa ,kujeruhi na kuua ndugu wa jamaa moja kwa sababu tu ya madaraka ya kulazimisha mtu mmoja kushinda uchaguzi kwenye Kata au jimbo.
Mchawi wa Afrika ni Waafrika wenyewe wala sio nchi za Magharibi.