Tanzania ni nchi pekee duniani inayojiendesha yenyewe bila Rais

UMMATI

Member
May 18, 2011
64
13
1.Leo nafunguka kwa kusema hivi ''TANZANIA NI NCHI PEKEE DUNIANI INAYOJIENDESHA YENYEWE BILA RAIS''. Ni muda mrefu sasa mambo mengi yanatokea, watu wanachota rasilimali za nchi bila huruma, mikataba mingi feki inasainiwa tu, wizi mkubwa wa pesa za walipa kodi mfano richmond, dowans, kagoda nk, lakini haya yote yakitokea rahisi yupo kimya wala hashtuki, hatoi onyo lolote japo mkwara tu. Lakini cha ajabu alipotakiwa kuzungunzia DOWANS alijing'atang'ata tu ulimi na kuishia kusema hawajui dowans na wala hana shida ya kuwajuwa.(.......)??????

2.Mawaziri wengi aliowateuwa yeye mwenyewe kwa utashi wake, wameonekana kuboronga kiasi cha kumtia aibu kubwa lakini wala hakuna hatua yeyote ya kuwajibika inayochukuliwa na hamna anayeuliza. (......)?????

3.Ndani ya chama anachokiongoza watendaji wake wakubwa wameonekana kuropokaropoka tu kila mmoja na analoamkanalo ndo hilohilo bila hata kutafakari analisema.(......)?????

4.Shillingi ya nchi yetu dhidi ya dollar ya marekani ndani ya mwezi mmoja imeshuka toka $1/Tsh1540 hadi $1/Tsh1840. Hakuna hatua yoyote ya kuimarisha shillingi yetu inayochukuliwa na kiongozi wetu.(.....)????

5. Na mengineyo mengi tu.(why)?????

Kutokana na haya yote ni sawa na kusema Tanzania inajiendesha yenyewe bila rais.

SOURCE; NI MTAZAMO WANGU.

Naomba kuwakilisha hoja.
 
1:Mzee Mwinyi alishasema kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kwa kila anayejifunza kunyoa(kuongoza) hujifunzia hapo.

somo tumeshapata.tusimlaum rais bali tuwalaum waliomteua (usalama a.k.a uhasama wa taifa na vibaraka wao.
 
Kusema nchi haina rais ni kosa la uhaini kisheria, lakini kwa kuwa nchi haifuati sheria hakuna rais na hakuna serikali.
 
thread yako ina km ka ukweli fulani hivi.......................
 
kweli mkuu. Kuna mifano ya maraisi hapa Afrika ambao wanathubutu na wanasonga mbele, Juzi hapa raisi wa afrika ya kusini kafukuza mawaziri wawili kwa wizi, rais sata anafanya vitu vyake. n.k
 
Nimeshindwa hata kuisoma, imeni "put off", kuanza tu Tanzania haina Rais, kitu ambacho siyo kweli. Unaweza kuwa unazo hoja lakini kuanza na uongo oooh...
 
Ni makosa kusema Tanzania haina Rais, labda ni lugha tu imeyumba lakini ukiangalia mambo yanayofanyika utaona nchi haina kiongozi imara. Ni viongozi wangapi wana tuhuma waziwazi wameachwa bila Rais kuchukua maamuzi? Rais kama JK anatakiwa awe na Waziri Mkuu imara na watendaji wengine wenye akili..yeye awe na kofia ya urais kupitisha kazi za watendaji wake. Tatizo kubwa la siasa ya Tanzania na CCM kwa sasa ni kuwa, wale wanaomsaidia Rais kuingia madarakani wanapewa ahadi hata iwe kuwa aliyekusaidia ni fisadi. Na imani kubwa sana kama JK 2005 angesimama yeye kama yeye wananchi wengi bila kujali upinzani wangempigia kura.
 
Nimeshindwa hata kuisoma, imeni "put off", kuanza tu Tanzania haina Rais, kitu ambacho siyo kweli. Unaweza kuwa unazo hoja lakini kuanza na uongo oooh...

Wewe unayedai kuwa Tz ina rais what has he done in the yrs his reigned? I personally think Nothing! Like the thread says whenever his needed to make serious statements he has nothing to say. Let me add all he does is smile. We need answers. Not his pathetic smiles. We need a president whose gonna be a leader and take action. Nt a person who doesnt know anything coz he sure acts that way. So why he the president?
I agree with the statement we dnt have a President as a country. No system is being followed. Its clear you can do anything and get away with it in Tz.
God bless and protect Tanzania
 
Haina Rais ? Mbona Watanzania mmekuwa walalamishi sana ? Kipindi cha Mkapa mlisema hafai leo hii Kikwete hafai nahic hata akija Dr Slaa naye pia mtamchoka kwa kipindi kifupi.
 
MwanaHalisi juzi niliiona wamesema "nchi ipo kwenye Auto-Pilot...."Siendelei tena alielewa ameelewa!!
 
Tangu kifo cha Yahaya alipoondoka na nyota anazowapa viongozi mambo ni mabaya sana kwa watawala wetu.
 
Ukizani tanzania haina raisi jaribu tia mguu somalia kama kawiki hivi alafu uje utuambie uchambuzi wako.....
 
The thread has a point. The comments lack mwelekeo. My observation is: what now? As per our constitution we put him there albait the numbers do not reflect the reality. Lets come up with tangible solutions not malalaiko day in day out! Maisha ya waTanzania wengi yapo njia panda na wachache wanaelea bila wasiwasi.
 
Kusema nchi haina rais ni kosa la uhaini kisheria, lakini kwa kuwa nchi haifuati sheria hakuna rais na hakuna serikali.
Uhaini wa utumbo wa bata? Hebu kaa kimya kama huna la kuongea
 
Back
Top Bottom