Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,042
- 16,872
Moyo wangu unaniuma,
Najiona mwenye hatia,
Sina raha nalazimisha tabasamu,
Mimi Jack Daniel ni mwanachama wa chama cha mapinduzi Kwa miaka 23 mpaka leo hii.
Nakumbuka nilichukua kadi hii kwasababu kuu mbili,
Kwanza ilikuwa kujihakikishia ajira ya kudumu maana adui akikushinda nguvu mpishe.
Pili ilikuwa ni Sera za kiongozi aliyekuwepo awamu ile ya tatu akiwa kwenye muhula wa mwisho Sera zake nilikuwa nazikubali.
Maisha yanasonga kimtindo,siyo mabaya sana,wala siyo good life kivile,ila sifanani na wengine wengi umri umesogea,nimestaafu Kwa hiyari ili kujikeep busy na biashara zangu zaidi,hii imenipa Uhuru wa kwenda popote,bila bughdha japo serikalini bado nafanya kazi kila nikihitajika.
{Ama kweli UJUZI hauzeeki}
Kwakweli najivunia kuona licha ya kuretire lakini taasisi huniita na kunipa kazi ,haswa kutoa ushauri,kuwa frontline haswa kwenye project kubwa kwani umri wangu unaruhusu na wapo waliolaani Mimi kuacha kazi mapema kabla,lakini Nina sababu zangu binafsi huku ndugu,jamaa na familia yangu wakiridhia Kwa mioyo kunjufu.
all in all Tanzania ni sehemu nzuri ya kuishi kwani Kwa miaka mingi imenipa Uhuru na uwazi huku ikinionesha upendo na mshikamano wa kweli.
Lakini leooo nasikitika kuona,,,,,,,,
1.Waumini wa Kanisa la ufufuo na uzima wakiabudu nje ya Kanisa lao,hili limeniumiza mno
2.Lakini Chama cha demokrasia na maendeleo kukivuruga kwasababu zisizoeleweka ili kukufifisha kisifikie matarajio hili limeniumiza.
3.Taasisi kibao kuingiliwa,mamlaka zao,Leo natangaza hadharani hamtoniona tena nikishangilia Yanga yangu niliyoipenda tangu utotoni sababu nazijua Mimi,kiufupi sitaki mpira wa kibongo.
4.Mimi ni mfuasi wa dini ya kikristo , Roman Catholic na tangu utotoni nilifundishwa kuheshimu taratibu na Sheria za dini na madhehebu mengine.
5.Nakiri wazi Leo hii CCM kuna namna siikubali yaani karibu 40% Imani yangu imeshuka kwenye hiki Chama.
MUNGU ibariki Tanzania,
MUNGU ibariki Africa.