Tanzania na Utani wa Makabila: Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti ukaumia nafsi yako?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu wa Tanzania;

Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti (Mfano: Msukuma Vs Mzaramo) kisha ukaumia nafsi yako kimoyomoyo?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, mimi Infantry Soldier kabila langu halisi ni MJALUO, mwenyeji wa mkoa wa MARA katika wilaya ya RORYA. Kuna weekenda moja siku ya jumamosi jioni nilienda Pub moja hivi ipo karibia na huku ninapokaa.

Nilienda kupata beer mbili tatu moja ya moto na nyingine ya baridi kabisa kwa ajili ya kupunguza stress kidogo za hapa na pale za kimaisha. Kwa kawaida nikiendaga kunywa beer huwa ninabebaga 20,000/= kwa maana huwa ninakunywa beer mara moja tu kwa week (Jumamosi Jioni Pekee).

Sasa week hiyo nilikuwa nimechacha vibaya sana. Nina 10,000/= tu kwenye wallet ambayo ingeniwezesha kupata beers labda nne tu zile Lite kisha narudi home. Sasa bwana wakati nimepiga beer yangu ya kwanza ninajiandaa kupiga chupa ya pili akatokea mzee mmoja wa KIHAYA.

Sisi WAJALUO watani zetu huwa ni hawa WAHAYA, WAKEREWE pamoja na WAHA. Huyu mzee wa Kihaya alikuwa amezoeana sana na mzee wangu na anapajua home kwa maana nilipopanga mimi na nyumbani kabisa ni mwendo kama wa 30 minutes tu kwa miguu.

Sasa huyu mzee aliponiona tu akaanza mambo yake kama kawaida, "aaaah mtani nakuona mwanangu. alafu wee mtani huo ukitoka katika shughuli zako huko mkoani huwa haunipigi hata offer kidogo mzee wako nipooze koo langu" mara paaap yule baba akachukua beer yangu akafungua kwa meno kisha akaanza kuinywa.

Daaaah aisee roho iliniuma ile mbaya. Nikiangalia mfukoni nina buku teni tuu la kulipia bill, alafu huyu mzee ndio kanywa beer yangu kisha akavuta kiti akakaa karibu yangu zikaanza story. Roho iliniuma sana. Kumpiga siwezi kwa maana mimi sina hulka za kupigana na huyu ni baba mtu mzima wa miaka kama 50 hivi. Nikasema sawa bwana yote kheri.

Je, wewe mwana JF ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti (mtani wako) kisha ukaumia nafsi yako kimoyomoyo?

ANGALIZO: Ukiachana na utani wa kupitiliza utani una faida kubwa. Wengi tumefanikisha mengi kupitia watani zetu. Ukienda eneo la ugenini na ikatokea ukamkuta mtani wako huko hakika hautakuwa mpweke.

Watani ufanikisha sherehe na hata misiba kwa sababu uhamasishana wenyewe kwa wenyewe na kuhamasisha wengine na kufariji wafiwa.

Yanakera matani ya kikabila ila nasisitiza yaendelezwe maana Yanaleta mshkamano na kuambizana ukweli bila kuoneana haya.

Jamii inapumua kupitia haya matani na kuishi kwa mshikamano. Waliosoma social engineering courses tunaelewa dhima ya hili suala.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Nikiwa kwetu kasulu-BUHA sijuwahi kujua utani ni nini. Siku moja bana nikiwa dsm ukatokea musiba, aliyefariki muha, watani wakaja mfipa tena mwanamke na mkurya mmoja. Wacha waanze kuponda, eti ninyi waha mimi siwaelewi. Leo mnachanga hapa hata hela inayotakiwa haijatimia, kama hamjajiandaa si mngetoa matunzo na matibabu kwa marehemu? Mkurya na mfipa wakatangaza hakuna kuchimba hadi tupate hela yote iliyohitajika. Tulijichanga wala haikufika, ili shughuli ziendelee ilibidi tumfunge kamba mkurya, yule mama wa kifipa yeye tulimdhibiti.

Nikauliza, kwa nini wanafanya hivi, nikajibiwa ni watani na musiba wa juzi tuliwamwagia maji wakiwa wamelala
 
Sisi waarabu wa Tanga tunataniwa sana eti hatuna ndugu Dubai..inauma sana ila basi tu!
Usijali yaa Ak-arab... mie ndg yako asilia.. usiumie njoo UAE hadi huku Saudia ule tende na neema za maziwa ya ngamia na maji ya zamzam...
"Utani na ustaarabu tuliupandikiza Afrika ktk karne ya 14.... Salaam- Salimia-Samahani na Shukuru.. Amani itawale TZ
 
Sina hamu na watani hakyi Nani..walijua kutuchachafya katika msiba wa mshua..Kuna muda nilijiona uvumilivu unanishinda aisee..na walikuwa wengi kinyama..ili wanyamaze wanapewa pesa wanatulia kimya..watani hapana jamani.
 
Usijali yaa Ak-arab... mie ndg yako asilia.. usiumie njoo UAE hadi huku Saudia ule tende na neema za maziwa ya ngamia na maji ya zamzam...
"Utani na ustaarabu tuliupandikiza Afrika ktk karne ya 14.... Salaam- Salimia-Samahani na Shukuru.. Amani itawale TZ
Shukran akhuya...huku naambiwa mwarabu gani unakaa mwananyamala..dah!!
 
Back
Top Bottom