Wafanyabiashara wa Tanzania mna ugomvi na usafi wa vyoo?

bikira latifah

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
594
1,351
Tanzania utakuta mtu kafungua biashara kawekeza pesa ya kumwaga kwenye mtaji wa mamilioni ila chooni utakuta panatisha, ni kuchafu vibaya. Utakuta mtu anaingiza mamilioni kwa siku ila huduma ya choo inawashinda, hivi shida huwa ni nini?

Mfanyabiashara pekee ambae nimeona yupo serious na choo chake ni mmiliki wa majengo ya Mlimani City, inshort wale wako serious na biashara yao. Yaani vyoo vya Mlimani City unaweza ukaingia na chakula ukala halafu ndio ukajisaidia! Majamaa wapo makini na usafi sijawahi ona.

Sijajua wafanya biashara wengine wanakwama wapi, hakuna kitu kinachonikeraga kama uchafu wa vyoo. Kwa sasa Uti sugu imekuwa ikisambaa kwa kasi sababu uchafu wa vyoo umezidi ndio maana hata vitoto vidogo vinaugua Uti uchafu wa vyoo ni too much
 
sio wewe tuko wengi tunaoshangazwa na hiyo hali. na kuna wengine unakuta jengo halina choo kujisaidia wanaenda kuomba kwa jirani. mtu anajenga mafremu haweki sehemu ya choo. ajabu sana. lakini sipaswi kushangaa kwa kua bado tuko ktk kubadilika kuwa watu kamili
 
Tatizo hasa linaanzia kwa watumiaji.

Ishakuwa itikadi kwa wengi ya watanzania kuamini vyoo vya halaiki vinapaswa viwe vichafu kukuta mtu anafanya jitihada kabisa kuchafua choo hata akikikuta kisafi.

Kwa macho yangu niliona mtu mzima kabisa na heshima zake kimuonekano akipanda juu ya choo badala kukaa huku akiwa ameacha mlango wazi. Na ilikuwa ni sehemu yenye vyoo visafi kabisa.
Utakuta mwingine anajisaidia na bila ya sababu ya msingi ha flash haja yake.

Akichafua mmoja atakaefuata ataendeleza uchafu. Tuanze kujifunza sisi wenyewe kutumia vyoo kinadhifu, itakuwa rahisi hata wamiliki ku maintain usafi.
 
Tatizo ni mindset za watu tu mkuu,
Watu wengi wamekariri kua Choo ni sehemu chafu,hawaoni umuhimu wa choo kua kisafi,
Mtu mwenye mindset ya hivyo,hata akikuta choo kisafi basi atafanya juu chini akichafue coz kisha chukulia kua hapo ni chooni tu!
Kuna jirani yangu muhaya kaja kufungua hoteli kwenye jengo letu la biashara....kumkabidhi funguo Sasa hivi siwezi hata kwenda hapo haha naenda guest house ya jirani yaani NI wachawi...
 
Back
Top Bottom