Tanzania na magrill milangoni na madirishani

Tanzania na magrill milangoni na madirishani

Hii akili ya kuweka magrill kwenye milango na madirisha tumeipatia wapi?
Nyumba nyingi zimejengwa vizuri lakini ukikaa humo ni kama jela.
Ajali ya moto ikitokea ni ngumu sana kupona?
Mbona nchi nyingi hawaweki magrill je hawahofii usalama wa mali zao?
Miaka ya 2000 watu walikuwa wanachonga grills kwenye taa za nje na taa za magari lakini mwisho wameona ni kitu cha kijinga, kwanini kwenye nyumba hawabadiliki?
Nyumba ni ya ghorofa floor ya tatu kuna grill la nini?
Nyimba ina fence ya ukuta na umeme grills za nini?
Kwasababu Alminium haitumii frame..

Weka alminium tupu bila grills utumiwe salamu..
 
Hii akili ya kuweka magrill kwenye milango na madirisha tumeipatia wapi?
Nyumba nyingi zimejengwa vizuri lakini ukikaa humo ni kama jela.
Ajali ya moto ikitokea ni ngumu sana kupona?
Mbona nchi nyingi hawaweki magrill je hawahofii usalama wa mali zao?
Miaka ya 2000 watu walikuwa wanachonga grills kwenye taa za nje na taa za magari lakini mwisho wameona ni kitu cha kijinga, kwanini kwenye nyumba hawabadiliki?
Nyumba ni ya ghorofa floor ya tatu kuna grill la nini?
Nyimba ina fence ya ukuta na umeme grills za nini?
Una hoja ya msingi.
Magrili kwenye nyumba yana faida na hasara zake. Faida zake ni ulinzi na kuthibiti wezi wasiweze kuingia ndani ya nyumba kwa urahisi zaidi, lakini hasara zake ni pale inapotokea ajali kama vile ajali ya moto au jengo kuanguka, inakuwa vigumu kutoka nje.

TAHADHARI KUBWA SANA YA KUZINGATIA KWA WATU WOTE KUHUSU MADIRISHA NA MILANGO YA ALUMINIUM KWENYE NYUMBA ZETU:-
1. Ndio chanzo kikuu kabisa cha vifo vya Wakaazi wa nyumba kutokana na ajali mbaya za majiko ya Gesi yanapolipuka. Mara nyingi husababisha maafa makubwa kwa watu wote wanaoishi ndani ya nyumba husika, milango na madirisha ya aluminium huwa hayaruhusu gesi kutoka nje ya nyumba pale yanapofungwa.
2. Vifo vya Watu/wakaazi kutokana na Bitendo vya Visa vya Maadui zako kuweza kunyunyiza au kupulizia Gesi ya Sumu kwa urahisi ndani ya Chumba unacholala.
Ninayo mifano hai kabisa kuhusu suala hili. Mtu mmoja alikuwa amelala chumbani kwake, usiku alikuja adui yake na kupulizia gesi ya sumu kwa siri kupitia dirishani akiwa nje ya nyumba na Kisha alifunga madirisha yote, mtu huyo Alifia humo humo ndani ya chumba chake kwa kifo cha kutatanisha, lakini baadaye ilikuja kugundulika kwamba alipuliziwa sumu kupitia dirishani wakati yeye akiwa amelala ndani.
Be Very Careful!
 
Back
Top Bottom