Tanzania na Burundi kujenga reli ya thamani ya $900m

Hapo unakuwa umeilenga kongo sio burundi kama ilivoanishwa
Kwa sasa ni lazima tupite nchi moja kwa barabara ili tufike Congo, hiyo reli itakuwa haina maana kama bado tutategemea Burundi kufika Congo. Nasikia kuna njia ya barabara huko Rukwa ya kufika Congo moja kwa moja, kwanini isijengwe hio?
 
Burunfi wako chini sana kiuchumi, kielimu na karibu kwenye kila kitu EA, ajabu Tanzania imemkumbatia sana kama ally wake mkubwa.

Mkuu, Paul Kagame haaminiki, ni kigeugeu, huyu anaweza kukugeuka wakati wowote kwa masilahi yake. Kumbuka kisa cha Kagame na Kikwete juu ya DRC kuhusu M23, kumbuka "coalition of willingness" kati ya Rwanda, Uganda na Kenya, wakatutenga sisi.

Washirika wetu wakuaminika ukanda huu ni Burundi, Uganda, (labda na DRC) na SADC.

Kenya na Rwanda ni wakukaa nao macho sana! Majirani zetu ndio , na marafiki zetu ndio, lakini hawaaminiki asilani, wanasema unaweza kuchagua rafiki lakini huwezi kuchagua jirani.
 
Kwa sasa ni lazima tupite nchi moja kwa barabara ili tufike Congo, hiyo reli itakuwa haina maana kama bado tutategemea Burundi kufika Congo. Nasikia kuna njia ya barabara huko Rukwa ya kufika Congo moja kwa moja, kwanini isijengwe hio?

Mkuu, Huwezi kufika Congo kupitia Rukwa bila kwanza kuvuka ziwa Tanganyika, maana Tanzania hatujapakana na Congo kwenye nchi Kavu, Bali kupitia ziwa Tanganyika pekee. Ukitaka kwenda Congo direct kutoka Tanzania bila kupitia nchi nyingine lazima uvuke ziwa Tanganyika, either kupitia ,Kigoma , Katavi na Rukwa.

Lakini kwa njia ya nchi kavu lazima tupitie Zambia, Burundi, Rwanda au Uganda.
 
Mbona serikali ya TZ haina Mpango wa kujenga SGR kwenda Kigoma?.

Sasa hiyo SGR ya Uvinza - Gitega itauunganishwa vipi na bandari ya DSM?
Daraja la Busisis linaendelea vizuri na SGR Mwanza-Kahama iko sawa
 
Burundi kuna biashara gani ya kutulipa
Nanukuu kutoka Wikipedia juu ya yaliyoandikwa kuhusu Reli ya kutoka Uvinza kwenda Msongati, nchini Burundi.
"Emphasis is being placed on minerals,
Emphasis is being placed on minerals, especially nickel, which is found in significant quantities in Burundi. Other mineral deposits in the country include vanadium, gold, rare earth minerals, phosphates, kaolin, quartzite and limestone.
Plan to build a standard gauge railway on this route has been considered, with the possibility of extending the line to Bujumbura and eastern DR Congo"
Burundi inayo hazina ya kutosha ya Madini yaliyotajwa hapo juu.
Madini hayo yapo Musongati.
 
Hiyo hazina inasubili reli hii ndio ichimbwe? Au wawekezaji waligoma kuwekeza Burundi siku zote hizo kwa kuwa kuna barabara pekee
 
Mkuu, Huwezi kufika Congo kupitia Rukwa bila kwanza kuvuka ziwa Tanganyika, maana Tanzania hatujapakana na Congo kwenye nchi Kavu, Bali kupitia ziwa Tanganyika pekee. Ukitaka kwenda Congo direct kutoka Tanzania bila kupitia nchi nyingine lazima uvuke ziwa Tanganyika, either kupitia ,Kigoma , Katavi na Rukwa.

Lakini kwa njia ya nchi kavu lazima tupitie Zambia, Burundi, Rwanda au Uganda.
Sawa kabisa. Lakini kwanini tusinunue vivuko kama lengo ni kufika Congo moja kwa moja
 
Hiyo hazina inasubili reli hii ndio ichimbwe? Au wawekezaji waligoma kuwekeza Burundi siku zote hizo kwa kuwa kuna barabara pekee
Viongozi wenye maono, huweka mipango kwa malengo.
Mwalimu Nyerere alifahamu utajiri wa madini katika nchi yetu, lakini akasema tuyaache kwa kuwa hayaozi, ili Watanzania watakapokuwa na uwezo, wayachimbe wao wenyewe.
Waliotawala baada ya Mwalimu waliruhusu yachimbwe.
Tujiulize, tunafaidika kweli na madini yetu?
Musongati, nchini Burundi ipo deposit kubwa ya Nickel, ambayo matumizi yake makubwa ni kwenye magari ya umeme.
Muda wa kuyachimba ndiyo kwanza umefika.
 
Kwahiyo wakianza kuchimba hayo madini yatakuwa mazito sana kiasi kwamba barabara haiwezi kuhimili? Na pia kwa hoja yako inamaana tunapeleka reli huku tukiwa tunajua hatutopata chochote kwa muda usiojulikana, hii ni akili au matope
 
Burundi na Tanzania zimetia saini mkataba wa $900m kujenga njia ya reli itakayounganisha nchi hizo mbili jirani, tovuti ya Citizen imeripoti.

Reli ya 282km ya standard gauge itaanzia Uvinza mkoani Kigoma nchini Tanzania hadi Gitega, mji mkuu wa kisiasa wa Burundi, ripoti ilisema.

Waziri wa Mipango na Fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba alisema nchi hizo mbili "zitatafuta maeneo ambayo tunaweza kupata fedha za kufadhili mradi huo".

Inatarajiwa kuwa reli hiyo itaunganisha bandari ya Dar es Salaam na nchi kadhaa jirani zisizo na bandari, zikiwemo DR Congo na Rwanda.

Inaweza kusaidia kupunguza gharama za usafirishaji mizigo mkoani humo kwa asilimia 40, Mwananchi ilisema.

Tanzania inalenga kujenga mtandao wa reli wa kilomita 2,561 kwa matumaini ya kukuza biashara Afrika Mashariki na Kati.

Wazo zuri sana.
 
Bilasha bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda litakuwa limesha kamilika mpaka sasa
 
Waziri wa Mipango na Fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba alisema nchi hizo mbili "zitatafuta maeneo ambayo tunaweza kupata fedha za kufadhili mradi huo"....🤣🤣 hakuna kitu hapo ni usanii tuu
 
Au ndio mwanzo wa kuongeza kukopa
 
Back
Top Bottom