Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,337
Burundi na Tanzania zimetia saini mkataba wa $900m kujenga njia ya reli itakayounganisha nchi hizo mbili jirani, tovuti ya Citizen imeripoti.
Reli ya 282km ya standard gauge itaanzia Uvinza mkoani Kigoma nchini Tanzania hadi Gitega, mji mkuu wa kisiasa wa Burundi, ripoti ilisema.
Waziri wa Mipango na Fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba alisema nchi hizo mbili "zitatafuta maeneo ambayo tunaweza kupata fedha za kufadhili mradi huo".
Inatarajiwa kuwa reli hiyo itaunganisha bandari ya Dar es Salaam na nchi kadhaa jirani zisizo na bandari, zikiwemo DR Congo na Rwanda.
Inaweza kusaidia kupunguza gharama za usafirishaji mizigo mkoani humo kwa asilimia 40, Mwananchi ilisema.
Tanzania inalenga kujenga mtandao wa reli wa kilomita 2,561 kwa matumaini ya kukuza biashara Afrika Mashariki na Kati.