Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji wa gesi ya hellium duniani

Ngamanya Kitangalala

Verified Member
Sep 24, 2012
461
1,000
TANZANIA KUWA MOJA YA WAZALISHAJI MUHIMU WA GESI YA HELLIUM DUNIANI

Gesi ya hellium ni moja ya gesi adimu kabisa hapa duniani, ni gesi yenye sifa ya kipekee kabisa, ambayo inaifanya gesi hiyo kuwa na umuhimu mkubwa kabisa katika matumizi mbalimbali hapa duniani

Moja ya sifa kubwa kabisa inayoifanya gesi hii kuwa na upekee, ni kwamba hellium huwa haiyeyuki wala kuganda kwa urahisi, mara zote huwa katika hali ya gesi hata katika joto au baridi kali kabisa

hellium ina sifa nyingine kubwa, ni moja ya gesi nyepesi kabisa, sifa inayoifanya iweze kutumika kwenye maeneo mengi muhimu hapa duniani

Kwa sababu ya upekee wake huo, gesi hii imekuwa ikitumika kwenye maeneo mbalimbali hapa duniani, kama vile kwenye vifaa vya kimaabara na utabibu(laboratory &medical equipments), kwenye vyombo vya kwenda kwenye safari za juu angani( spacecraft) kama roketi( rocket), ambapo inatumika kama mafuta ambayo husaidia chombo hicho kusafiri kwenda kwenye anga za juu, vile vile gesi hiyo inekuwa ikitumika kwenye mitambo ya kinyuklia na kwenye vifaa ya kieletroniki

Kwa mujibu wa ripoti ya Hellium Global Market Report 2020, inaonyesha kuwa biashara ya gesi ya hellium duniani, kwa mwaka 2019 pekee,ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 10.6( zaidi ya shilingi trilioni 21), na kwamba thamani hiyo itakuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 11 kila mwaka,na inakadiriwa kufikia thamani ya dola za kimarekani 15.73 bilioni ( zaidi ya shilingi trilioni 32) ifikapo mwaka 2023

Moja ya eneo muhimu kabisa kwenye matumizi ya hellium gesi duniani, ni kwenye sekta ya afya, ambapo gesi hiyo imekuwa ikitumiwa na wataalamu wa afya kwenye mashine za MRI scanners( Magnetic Resonance Imaging) , ambapo inakadiriwa mpaka sasa kuna mashine hizo takribani 36,000 duniani kote zinatumika

Kwa mujibu wa taasisi ya Statista kutoka Ujerumani ambayo imebobea kwenye kutunza kumbukumbu za masoko na watumiaji( marketing and consumer data) taasisi hiyo inaonyesha kuwa MRI scanners ndio zinatumia zaidi gesi hiyo ya hellium, ambapo asilimia 20 ya hellium inayozalishwa duniani, inatumika katika mashine hizo za kiuchunguzi kwenye utabibu

Tangu mwaka 1925 Marekani (United States of America),ndio inekuwa mzalishaji mkubwa wa gesi hiyo( hellium), ambapo kuna machimbo( gas field) kwenye majimbo ya Texaa, Kansas na Oklahoma na gesi hiyo imekuwa ikihifadhiwa kwenye hifadhi kubwa ya Kimkakati( Strategic reserve) nchini humo, chini ya Federal Hellium Reserves katika jiji la Amarillo, jiji maarufu kama kitovu cha gesi ya hellium duniani( The hellium capital of the world)huko katika jimbo la Texas, ambapo inakadiriwa kuwa takribani futi za ujazo( cubic feet) bilioni 24.2zimehifadhiwa hapo

Kwa mujibu wa United States Geological Surrey , inaonyesha nchi ya Marekani wanazalisha asilimia 55 ya gesi hiyo hapa duniani, wakifuatiwa na nchi ya Qatar ambayo inazalisha asilimia 32 , na nchi ya Algeria wao wanazalisha asilimia 6, ambapo kwa mwaka 2018 pekee Marekani walizalisha hellium kiasi cha mita za ujazo( cubic metre)millioni 64, na nchi ya Qatar wao walizalisha mita za ujazo milioni 45

Lakini katika miaka ya karibuni, kumekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maeneo mapya ya uhakika kwa upatikanaji wa gesi hiyo adimu, ambapo kwa Marekani wanategemea kuacha uzalishaji wa gesi hiyo, kwenye machimbo yao, hiyo ni baada ya bunge lao( US congress) kupitisha sheria mwaka 1996, kuwa ifikapo Septemba mwaka 2021,machinbo hayo yawe yamefungwa na kufanya Marekani kuachana na biashara hiyo, ambapo baada ya hatua hiyo bei ya hellium gesi dunisni imepanda kutoka dola tano( $5 per litre) za Lskini kwa lita moja,miaka kumi iliyopita mpaka dola elfu moja( $ 1000 per litre) kwa lita moja kwa sasa, kwa wakati huu wa sasa, mahitaji ya gesi ya hellium ni futi za ujazo milioni nane( cubic feet 8 milion)kwa mwaka duniani kote

Mwaka 2016 nchini kwetu Tanzania, iligundulika hifadhi kubwa kabisa duniani ya gesi hiyo kwenye bonde la ufa ndani ya ziwa Rukwa, mkoani Rukwa

Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Oxford na Durham nchini Uingereza kwa kushirikiana na kampuni kutoka nchini Norway, iitwayo Hellium One, moja ya kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa gesi ya hellium hapa duniani, walifanikiwa kugundua hifadhi ya gesi hiyo, inayokadiliwa kufikia futi za ujazo bilioni 54,mara saba ya mahitaji ya saaa ya gesi hiyo duniani, na mara mbili zaidi ya nchi ya Marekani( 24.2 bilioni futi za ujazo) ambayo ndio mzalishaji mkubwa zaidi duniani

Hifadhi hiyo ya gesi hapa nchini kwetu( 54 billion cubic feet) inakadiriwa inaweza kuhudumia mahitaji ya hellium duniani kwa miaka takribani 20,pia kutumika kwenye mashine za MRI scanners 1.2 milioni duniani kote

Akiongea katika mtandao maarufu duniani wa masuala ya sayansi( live science) mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Hellium one, Thomas Abrahaman, alisema kampuni yake wanaamini Tanzania wana hifadhi ya hellium inayofikia futi za ujazo bilioni 98.6 mara mbili zaidi ya makadirio yao ya awali

Hii ni habari njema sana kwa nchi ya Tanzania, ambapo endapo uwekezaji huo utaanza, utaifanya nchi yetu kuwa muhimu sana kwenye uzalishaji wa gesi hiyo adimu yenye kuhitajika sana kwenye maeneo mbalimbali ya teknolojia

Wakubwa duniani, wanaitazama Tanzania kama tegemeo kwenye uzalishaji wa gesi hiyo kwa siku za usoni

Ni wakati sasa kwa watanzania sote kwa umoja wetu kuelewa ni namna gani wakubwa hawa wa dunia wanaitazama nchi yetu

Ngamanya Kitangalala Mwaswala
0756 669494
kngamanya@yahoo.com
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,820
2,000
Uwezo ,vifaa na teknolojia wa kuizalisha mnao,au Hadi muwapigie magoti Mabebelu?
 
Attachments

 • 20201124_182411.jpg
  File size
  34.6 KB
  Views
  0
 • 20201122_161633.jpg
  File size
  91.8 KB
  Views
  0

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,800
2,000
Ugunduzi wowote hapa ni sawa na Kichwa cha mwendawazimu hapa,tutegee watatunyoa tu km ile gesi ya mtwara

70% kwao, 30 kwetu huu si uwenda wazimu?
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
8,216
2,000
Tanzania ni tajiri - Rais John Pombe Magufuli
Mpango madhubuti ni muhimu kwa ustawi wa nchi yetu
Mungu ibariki Tanzania
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,275
2,000
TANZANIA KUWA MOJA YA WAZALISHAJI MUHIMU WA GESI YA HELLIUM DUNIANI

Gesi ya hellium ni moja ya gesi adimu kabisa hapa duniani, ni gesi yenye sifa ya kipekee kabisa, ambayo inaifanya gesi hiyo kuwa na umuhimu mkubwa kabisa katika matumizi mbalimbali hapa duniani

Moja ya sifa kubwa kabisa inayoifanya gesi hii kuwa na upekee, ni kwamba hellium huwa haiyeyuki wala kuganda kwa urahisi, mara zote huwa katika hali ya gesi hata katika joto au baridi kali kabisa

hellium ina sifa nyingine kubwa, ni moja ya gesi nyepesi kabisa, sifa inayoifanya iweze kutumika kwenye maeneo mengi muhimu hapa duniani

Kwa sababu ya upekee wake huo, gesi hii imekuwa ikitumika kwenye maeneo mbalimbali hapa duniani, kama vile kwenye vifaa vya kimaabara na utabibu(laboratory &medical equipments), kwenye vyombo vya kwenda kwenye safari za juu angani( spacecraft) kama roketi( rocket), ambapo inatumika kama mafuta ambayo husaidia chombo hicho kusafiri kwenda kwenye anga za juu, vile vile gesi hiyo inekuwa ikitumika kwenye mitambo ya kinyuklia na kwenye vifaa ya kieletroniki

Kwa mujibu wa ripoti ya Hellium Global Market Report 2020, inaonyesha kuwa biashara ya gesi ya hellium duniani, kwa mwaka 2019 pekee,ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 10.6( zaidi ya shilingi trilioni 21), na kwamba thamani hiyo itakuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 11 kila mwaka,na inakadiriwa kufikia thamani ya dola za kimarekani 15.73 bilioni ( zaidi ya shilingi trilioni 32) ifikapo mwaka 2023

Moja ya eneo muhimu kabisa kwenye matumizi ya hellium gesi duniani, ni kwenye sekta ya afya, ambapo gesi hiyo imekuwa ikitumiwa na wataalamu wa afya kwenye mashine za MRI scanners( Magnetic Resonance Imaging) , ambapo inakadiriwa mpaka sasa kuna mashine hizo takribani 36,000 duniani kote zinatumika

Kwa mujibu wa taasisi ya Statista kutoka Ujerumani ambayo imebobea kwenye kutunza kumbukumbu za masoko na watumiaji( marketing and consumer data) taasisi hiyo inaonyesha kuwa MRI scanners ndio zinatumia zaidi gesi hiyo ya hellium, ambapo asilimia 20 ya hellium inayozalishwa duniani, inatumika katika mashine hizo za kiuchunguzi kwenye utabibu

Tangu mwaka 1925 Marekani (United States of America),ndio inekuwa mzalishaji mkubwa wa gesi hiyo( hellium), ambapo kuna machimbo( gas field) kwenye majimbo ya Texaa, Kansas na Oklahoma na gesi hiyo imekuwa ikihifadhiwa kwenye hifadhi kubwa ya Kimkakati( Strategic reserve) nchini humo, chini ya Federal Hellium Reserves katika jiji la Amarillo, jiji maarufu kama kitovu cha gesi ya hellium duniani( The hellium capital of the world)huko katika jimbo la Texas, ambapo inakadiriwa kuwa takribani futi za ujazo( cubic feet) bilioni 24.2zimehifadhiwa hapo

Kwa mujibu wa United States Geological Surrey , inaonyesha nchi ya Marekani wanazalisha asilimia 55 ya gesi hiyo hapa duniani, wakifuatiwa na nchi ya Qatar ambayo inazalisha asilimia 32 , na nchi ya Algeria wao wanazalisha asilimia 6, ambapo kwa mwaka 2018 pekee Marekani walizalisha hellium kiasi cha mita za ujazo( cubic metre)millioni 64, na nchi ya Qatar wao walizalisha mita za ujazo milioni 45

Lakini katika miaka ya karibuni, kumekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maeneo mapya ya uhakika kwa upatikanaji wa gesi hiyo adimu, ambapo kwa Marekani wanategemea kuacha uzalishaji wa gesi hiyo, kwenye machimbo yao, hiyo ni baada ya bunge lao( US congress) kupitisha sheria mwaka 1996, kuwa ifikapo Septemba mwaka 2021,machinbo hayo yawe yamefungwa na kufanya Marekani kuachana na biashara hiyo, ambapo baada ya hatua hiyo bei ya hellium gesi dunisni imepanda kutoka dola tano( $5 per litre) za Lskini kwa lita moja,miaka kumi iliyopita mpaka dola elfu moja( $ 1000 per litre) kwa lita moja kwa sasa, kwa wakati huu wa sasa, mahitaji ya gesi ya hellium ni futi za ujazo milioni nane( cubic feet 8 milion)kwa mwaka duniani kote

Mwaka 2016 nchini kwetu Tanzania, iligundulika hifadhi kubwa kabisa duniani ya gesi hiyo kwenye bonde la ufa ndani ya ziwa Rukwa, mkoani Rukwa

Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Oxford na Durham nchini Uingereza kwa kushirikiana na kampuni kutoka nchini Norway, iitwayo Hellium One, moja ya kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa gesi ya hellium hapa duniani, walifanikiwa kugundua hifadhi ya gesi hiyo, inayokadiliwa kufikia futi za ujazo bilioni 54,mara saba ya mahitaji ya saaa ya gesi hiyo duniani, na mara mbili zaidi ya nchi ya Marekani( 24.2 bilioni futi za ujazo) ambayo ndio mzalishaji mkubwa zaidi duniani

Hifadhi hiyo ya gesi hapa nchini kwetu( 54 billion cubic feet) inakadiriwa inaweza kuhudumia mahitaji ya hellium duniani kwa miaka takribani 20,pia kutumika kwenye mashine za MRI scanners 1.2 milioni duniani kote

Akiongea katika mtandao maarufu duniani wa masuala ya sayansi( live science) mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Hellium one, Thomas Abrahaman, alisema kampuni yake wanaamini Tanzania wana hifadhi ya hellium inayofikia futi za ujazo bilioni 98.6 mara mbili zaidi ya makadirio yao ya awali

Hii ni habari njema sana kwa nchi ya Tanzania, ambapo endapo uwekezaji huo utaanza, utaifanya nchi yetu kuwa muhimu sana kwenye uzalishaji wa gesi hiyo adimu yenye kuhitajika sana kwenye maeneo mbalimbali ya teknolojia

Wakubwa duniani, wanaitazama Tanzania kama tegemeo kwenye uzalishaji wa gesi hiyo kwa siku za usoni

Ni wakati sasa kwa watanzania sote kwa umoja wetu kuelewa ni namna gani wakubwa hawa wa dunia wanaitazama nchi yetu

Ngamanya Kitangalala Mwaswala
0756 669494
kngamanya@yahoo.com
Kutokuweka “source” au hata “citations” ndiyo ujinga wako.

Unaandika habari za kitafiti kama zile ni tafiti zako, halafu unaweka na namba ya simu kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom