Tanzania kutokomeza uagizaji wa Ngano Nje ya Nchi ifikapo 2030. Wilaya ya Makete kuongoza mageuzi ya kilimo cha ngano kibiashara

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,856
Rais Samia anaendelea kujipambanua Kwa kuleta Mageuzi makubwa kwenye Kilimo chenye Tija Nchini.

Tanzania ni Nchi ya 5 Afrika Kwa Kuagiza Ngano nyingi kutoka Nje ya Nchi na ambapo Asilimia 90% ya Ngano inayotumika Nchini hutoka Nje ya Nchi na hasa Ukraine na Urusi na kuigharimi Nchi karibu Bil.700 Kila mwaka.Kwa kuwa Ardhi tunayo na hali ya hewa ni rafiki, Serikali ya awamu ya 6 imekataa aibu hii na kuja na Mpango wa Kilimo Tija almaarufu ajenda 10/30 ambayo Miongoni mwao ni kuhakikisha inatokomeza Uagizaji wa Ngano Nje ya Nchi.

Ili kufikia azma hiyo Serikali imeuteua Mkoa wa Njombe hususani Wilaya ya Makete kuwa kitovu Cha uzalishaji wa Ngano kutosheleza mahitaji ya ndani na kibiashara.Wilaya ya Makete ndio itakuwa kitovu Cha kuzalisha miche ya mbegu kibiashara ambazo zitapandwa maeneo mengine ikiwemo Mkoa wa Manyara..

My Take
Rais Samia na Waziri Bashe wanaendelea kujipambanua kwenye maono makubwa yatakauoleta Tija na mapinduzi kwenye sekta ya Kilimo.
 
Ni fikra nzuri sana ila tujipange haswa kwani kuna nchi 50 duniani zinategemea chakula kutoka Russia- Ukraine

Sisi naona labda tuwe na mashamba makubwa sana sehemu kadhaa na yawe ya umwagiliaji hasa tukizingatia tuna mito na Maziwa pia

Wenzetu wenye mito na maziwa wanaitumia haswa kwani ni neema walizopewa ili wazitumie ila sisi hatujui rasilimali zetu zinatumikaje

Sisi sio wa kuagiza kila kitu nje tupunguze wizi na hela zitaonekana za kufanya mambo makubwa zaidi
 
Ni fikra nzuri sana ila tujipange haswa kwani kuna nchi 50 duniani zinategemea chakula kutoka Russia- Ukraine

Sisi naona labda tuwe na mashamba makubwa sana sehemu kadhaa na yawe ya umwagiliaji hasa tukizingatia tuna mito naawaziwa pia

Wenzetu wenye mito na maziwa wanaitumia haswa kwani ni neema walizopewa ili wazitumie ila sisi hatujui rasilimali zetu zinatumikaje

Sisi sio wa kuagiza kila kitu nje tupunguze wizi na hela zitaonekana za kufanya mambo makubwa zaidi
Tushaanza kujipanga Toka mwaka Jana,ndani ya miaka 3 ijayo nusu ya ngano itatoka Tanzania ,by 2030 tutakuwa tuna exports
 
Kwenye kuanzisha miradi tuko vizuri, akili ya usimamizi haijawahi kuwepo.
Serikali imeajiri mamia ya wahandisi wa Kilimo,imewapeleka wengine Israel na Egypt kujifunza mambo hayo.

On top of that mwaka huu wanatajenga zaidi ya nyumba 4,000 za Maofisa Ugani wakae huko huko.

Mwisho imenunia magari na pikipiki Kwa ajiri ya usimamizi bila kusahau kuwaongezea Bajeti.

Mzee Samia na Bashe wako Serious
 
sawa mkuu, subiri report ya Mkaguzi wa mahesabu ya mwaka 2024/25
 
Kuanzisha miradi ni kitu kingine na kusimamia nayo ni kitu kingine kigumu kwa watanzania,kulikuwa na mashamba makubwa ya ngano huko Basotu wilaya Hanang mkoani Manyara,yakisimamiwa na wakanada leo ni mapori ya kulishia mifugo.
 
Rais Samia anaendelea kujipambanua Kwa kuleta Mageuzi makubwa kwenye Kilimo chenye Tija Nchini.

Tanzania ni Nchi ya 5 Afrika Kwa Kuagiza Ngano nyingi kutoka Nje ya Nchi na ambapo Asilimia 90% ya Ngano inayotumika Nchini hutoka Nje ya Nchi na hasa Ukraine na Urusi.Kwa kuwa Ardhi tunayo na hali ya hewa ni rafiki, Serikali ya awamu ya 6 imekataa aibu hii na kuja na Mpango wa Kilimo Tija almaarufu ajenda 10/30 ambayo Miongoni mwao ni kuhakikisha inatokomeza Uagizaji wa Ngano Nje ya Nchi.

Ili kufikia azma hiyo Serikali imeuteua Mkoa wa Njombe hususani Wilaya ya Makete kuwa kitovu Cha uzalishaji wa Ngano kutosheleza mahitaji ya ndani na kibiashara.Wilaya ya Makete ndio itakuwa kitovu Cha kuzalisha miche ya mbegu kibiashara ambazo zitapandwa maeneo mengine ikiwemo Mkoa wa Manyara..

My Take
Rais Samia na Waziri Bashe wanaendelea kujipambanua kwenye maono makubwa yatakauoleta Tija na mapinduzi kwenye sekta ya Kilimo.

aliyeua kilimo cha ngano tz ni nani? au umezaliwa jana
 
Kuanzisha miradi ni kitu kingine na kusimamia nayo ni kitu kingine kigumu kwa watanzania,kulikuwa na mashamba makubwa ya ngano huko Basotu wilaya Hanang mkoani Manyara,yakisimamiwa na wakanada leo ni mapori ya kulishia mifugo.
Ndio shida ya kuwa na sera za ujamaa,Huwa haziendani na Biashara..

Wawekezaji Wana Imani na sera za Rais Samia
 
hao hao unaowasifia.....ngano ilikuwa inalimwa kwa wingi sana manyara, rukwa na njombe. hata ukienda huko leo, utakuta wakulima wadogowadogo wanajilimie eka chache kwa ajili ya matumizi yao binafsi. walioua kilimo cha ngano ni hao hao unaowasifia, eti wanaanzisha....unaanzishaje kitu kilichokuwepo na ukakiua wewe mwenyewe?
 
Samia na Bashe walikuwepo wapi Hadi wakaua Kilimo? Acha upuuzi wako
 
Nakumbuka uzalishaji wa ngano ulishafanyika wakati wa Nyerere, walikuja wataaalam na vifaa kutoka Canada. Walipokuwepo wao tulikuwa tunazalisha vizuri sana, walipoondoka tu na uzalishaji ukafa.

Hizi project naamini wakifanya wakulima binafsi zitafanikiwa. Kama zitakuwa ama mpango wa BBT kuna uwezekano mkubwa tukafanikiwa.

Lakini, ikiwa ni mpango ambao utasimamiwa na serikali na au vyama vya ushirika, yaani mali ya umma, ujuwe hatutaendelea.

Alah ampe hekima Bashe awe na mpango mzuri wa kuwawezesha wakulima binafsi.
 
Zitafanywa na individuals na Private companies,kazi ya serikali ni kutoa mazingira wezeshi ikiwemo miundombinu ya uwamwagiliaji ambazo zitakuwa zinalipiwa na wakulima hususani kwenye mpunga,chai na mazao ya bustani.
 
kwani wamekuja na chama kipya? chama na wizara havina records? Au huyo samia na bashe wako ndiyo wamepigania uhuru wa nchi hii na wameanza upya kama mwaka 1961?

kwa nini umeruhusu ushabiki wako kwa samia na bashe umegubika ufahamu na elimu yako!??
Wamekuja na.mawazo.mapya ndani ya chama kile kile.
 
hao hao unaowasifia.....ngano ilikuwa inalimwa kwa wingi sana manyara, rukwa na njombe. hata ukienda huko leo, utakuta wakulima wadogowadogo wanajilimie eka chache kwa ajili ya matumizi yao binafsi. walioua kilimo cha ngano ni hao hao unaowasifia, eti wanaanzisha....unaanzishaje kitu kilichokuwepo na ukakiua wewe mwenyewe?
Kwa hiyo unashauri waachane na hilo suala?
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Back
Top Bottom