Tanzania kushirikiana kijeshi na Iran | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kushirikiana kijeshi na Iran

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 21, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kati ya Waziri wa Tanzania au wa Iran mmoja wao amelidanganya taifa lake:

  Hivi ndivyo imeripotiwa:

  Lakini vyombo vya Iran na vingine vya kimataifa viliripoti hivi:

  more News:
  So:

  Yawezekana:

  a. Waziri wa Iran alikuwa anadanganya
  b. Waziri wa Tanzania alikuwa anadanganya
  c. Hawa wote hawajui walichokubaliana
  d. Hawa hawakukutana kabisa na hawaakuzungumza lolote!

  Vyovyote vile ilivyo; Kama Mwinyi kadanganya basi na yeye ajiandae kuomba msamaha tumsamehe.
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  God is faithful na amesema mwenye haki wake hataangamia wacha washirikiane wakitaka waanze ushirika na Lucifa mwenyewe tumechoka
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mwinyi alisoma Medicine kule ndo maana ana interest!
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Jan 21, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  wandugu,

  ..Irani ndiyo wakufunzi wa Hamas na Hezbollah.

  ..nina wasiwasi sana na hawa wa-Irani wasijelivuruga jeshi letu kwa kutumbukiza mambo yao ya ajabu-ajabu.
   
 5. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kwa vile mou ilikuwa inafanywa baina ya iran na nchi ambayo serikali yake haifungamani ni dini yoyote basi naamini ni vyema huyu waziri wa iran angehimiza nchi zote wapenda haki na amani kusaidia katika kusitisha unyama wa israeli kwa wapelestina huko gaza.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  hawa jamaa si ndio alfitina wakubwa kwa sasa hapo mashariki ya kati?
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  As much as napenda urafiki na mataifa mbalimbali duniani nisingekimbilia kuunda uhusiano wa kijeshi na Iran.
   
 8. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ...Lakini Tanzania kama Nchi haina Dini!!!!!!!.....hapa kuna mushkili kidogo ktk kutetea/kulinda 'mataifa ya kiisilamu'.
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Tunafichwa nini? Yaani habari twazipata kupitia ISNA!
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Inasemekena Tz kuna Uranium na Iran anahitaji sana hiyo resource

  Inaoenkana kila anayetaka kuwa Rais Tz ni muhimu kuwa karibu na Iran

  ......of all the countries!!!.....Iran!!.......give me a break!!......damn
   
 11. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Hatua ya kuingia mkataba wa ushirikiano wa kijeshi na nchi nyingine inaamuliwa na CABINET au anajitokea waziri tu na anatuingiza?

  Tunatakiwa kuingia ushirikiano na nchi ambazo zinajali haki za binadamu. Kwenye sheria zake, Iran ina adhabu ya kifo kwa raia wake yoyote anayebadilisha dini kutoka Uislamu kwenda Ukristo. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

  Wakati wa kampeni za Urais, kuna gazeti la Uingereza lilidai JK alipewa US$20 million na Iran. JK aling'aka akatishia kulishtaki gazeti, lakini akaogopa. Labda ilikuwa kweli, na sasa anawalipa.
   
 12. H

  Haki JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna nchi inayojali haki za binadamu duniani, mbona usemi kuhusu mauaji ya watu wa Iraq yaliyofanywa na Bush. Nyie mkiona nchi ya kiislamu inaingia mkataba na Tanzania mnapiga kelele, lakini Kikwete akienda Vatican mnasherehekea.
   
 13. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Haki,

  Two wrongs don't make a right. Kutokujaliwa kwa haki za binadamu Iran hakukubaliki eti kwa vile ziko na nchi nyingine za aina hiyo.

  Vatican haina tatizo la kukiuka haki za binadamau. Na hatuna ushirikiano wa kijeshi na Vatican. Haina jeshi wala. Nchi ya Vatican inajishughulisha kujenga mashule na mahospitali Tanzania. Iran inakaribishwa kufanya hayo.

  Hatukatai kuwa na uhusiano wa karibu na nchi za Kiislamu kama Algeria na Misri ambazo si za hatari. Iran is a dangerous country that supports terrorist groups. How can we cooperate militarily with sponsors of terrorists?
   
 14. M

  Mchapakazi Member

  #14
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona baada ya Bush mshkaji wake na Kikwete kuondoka jamaa ameamua kugeukia IRAN!
  Haya we lets see ni ushirikiano gani wanataka kufanya..
   
 15. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  tutatengwa
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu Moshi,

  In the first place Augustine Moshi ninayemjua mimi ana upeo mkubwa wa mambo na ANAPASWA kuweka uwiano katika katika maandiko yake. Unasema kuwa Iran ina sponsor terrorist groups,
  Je, habari hizi wewe umezipata kutoka wapi (source)?
  Je, ni kwanini Marekani kupitia Shirika la Ujasusi lina wa-sponsor wairan against nchi yao?
  Je, unakubaliana na mimi kuwa wafuatao walikuwa ni vipenzi wa wamarekani na walikuwa wanapata sponsorship toka kwao?
  Osama bin Laden,
  Jonas Savimbi,
  Renamo
  Mobutu
  Mimi siungi mkono namna yeyote ile ya ugaidi iwe ni kwa wanaodai haki hadi kwa wanaonesha ubabe.
  Iko haja ya kukaa chini na kufikiri matatizo ya yanayowakuta wananchi wa paletine as well as Israel. Hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa aidha mpalestina au muisraeli kwa namna yeyote ile.
  Nikirudi kwenye uhusiano wetu na Iran, ninamkumbuka sana Mwalimu ambaye mara kwa mara alikuwa anasisitiza umuhimu wa kutofungamana na 'mkubwa yeyote kwa vile ni hatari kwa uhuru wa nchi. Alisistiza kuwa nchi yetu haiwezi kuchaguliwa rafiki, ni nchi huru ambayo inaweza kujiamulia mambo yake kwa vile inavyoona inafaa. Tumekuwa na uhusiano na Iran kwa kipindi kirefu sana, tumekuwa na Uhusiano na China kwa kipindi kirefu sanambona hatujahoji kuvunja uhusiano na China kama kigezo ni madai ya 'mkubwa' kwamba kuna uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu? Tunadanganywa, na tunakubali. Lakini sijasikia tukitaka tuvunje uhusiano na Marekani kwa kuvunja haki za binadamu, ni leo hii serikali ya Marekani imetangaza kusitishwa kwa process za kuwashitaki wale waliowekwa kizuizini Guantenamo bila ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
  Ninarudia kama tunataka kujadili masuala ya mahusiano kati ya Tanzania na nchi nyingine si vema tuaangalie matatizo kati ya 'mkubwa' na huyo tunayetaka kushirikiana nae kigezo kiwe ni mahusianao yao.
   
 17. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Pundamilia07,

  Umeona nani kasema tuvunje uhusiano na Iran? Hatusemi hivyo. Tunachozungumzia hapa ni Waziri wa Ulinzi kwenda Iran na kutuingiza kweye ushirikiano wa Kijeshi na nchi hiyo.

  Hizbulla (or Hezbullah, or whatever) ni kikundi cha kigaidi. Why? Hivyo ndivyo ulimwengu unavyotamka. Naamini ni kikundi ambacho kiko kwenye orodha ya UN ya magaidi. Sasa Hizbullah kinafadhiliwa na Iran. Hata mkuu wake anakaa Iran. Thus, Iran inasaidia ujangili duniani.

  Sijasema Iran pekee ndio inasaidia ujangili duniani. Hata hivyo, niseme tena kwamba two wrongs do not make a right.

  Sababu yangu ya msingi ya kusema hatupashwi kuwa na uhusiano wa kijeshi na Iran ni kwamba nchi hiyo ina sheria ambazo zina adhabu ya kifo kwa raia wake yoyote anayebadili dini toka Uislamu hadi Ukristu.
   
 18. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu Moshi,

  Kwa hiyo unahoji uhusiano wetu na Iran kama nchi kwa sababu za kidini?
   
 19. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  It is open and clear, the reason is Muhammadic to incentive Muhammadans beneficiaries fanatics.
   
 20. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Nahoji uhusiano wetu nao kwa sababu sheria za nchi yao zinasema auawe raia yoyote anayebadilisha dini toka Uislamu kwenda Ukristo. Inaelekea wametumia dini vibaya, na matokea yake wakapitisha sheria ambazo hatuwezi kukubalina nazo.

  Kutaka uhusiano wa karibu na nchi ni kuunga mkono values zake. Hatuwezi tukakubaliana na ukandamizaji wa kidini wa Iran. Kama Waziri Mwinyi anakubaliana nao, asilazimishe taifa letu kufanya hivyo hivyo.
   
Loading...