#COVID19 Tanzania kupokea dozi 500,000 za chanjo ya Pfizer

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Tanzania inatarajia kupokea Dozi 500,000 za Chanjo dhidi ya COVID19 ya Pfizer kupitia Mpango wa COVAX. Imeelezwa, Dozi hizo zitachanjwa mara mbili

Akitoa Taarifa ya Wiki Jijini Mwanza amesema, "Hizi Pfizer ni sehemu ya Chanjo Dozi 3,700,000 ambazo zitaletwa na COVAX Facility. Mwisho wa mwezi huu zitakuja hizo laki tano, lakini awamu kwa awamu zitaendelea kuja zingine"

Aidha, amesema hadi kufikia Oktoba 15, 2021 Watanzania zaidi ya 940,000 walishapata Chanjo
 
Jaman almost 1 million ya watanzania wako vaccinated mimi ni nani nipinge

Em soon in shaa Allah
 
Kwa miezi mitatu tunahangayika na dozi milioni 1 iliyoletwa na wamarekanina bado haijaisha. Juzi tu tumepokea SINOFARM karibu dozi milioni 1 pia ambazo kuzimaliza itachukua kama miezi 5. sasa hiozo laki 5 si zitakuja ku expy kabla ya kutumika? Policy ya chanjo ya Covid tanzania lazima ibadilike na serikali wawe wakali kidogo vinginevyo.
 
😂😂😂😂😂 Kama kawaida Watanzania ni watu wa kujaribu jaribu kama laini za simu tunamiliki zaidi ya laini tano nini chanjooo. Tozo zitalipa
 
Ni jambo jema sana ila lazima kasi ya kuchanja iongezwe.

Ila kuwaambia raia wachanje mara mbili inaweza kuwa changamoto ni vyema raia wajitokeze wakachanje hizi za Janseen kabla hazijaisha ili kuepuka usumbufu wa kuchanja mara mbili.
 
Kwa miezi mitatu tunahangayika na dozi milioni 1 iliyoletwa na wamarekanina bado haijaisha.. Juzi tu tumepokea SINOFARM karibu dozi milioni 1 pia ambazo kuzimaliza itachukua kama miezi 5. sasa hiozo laki 5 si zitakuja ku expy kabla ya kutumika? Policy ya chanjo ya Covid tanzania lazima ibadilike na serikali wawe wakali kidogo vinginevyo.
Wamkalie nani?🙄
 
Ni jambo jema sana ila lazima kasi ya kuchanja iongezwe.

Ila kuwaambia raia wachanje mara mbili inaweza kuwa changamoto ni vyema raia wajitokeze wakachanje hizi za Janseen kabla hazijaisha ili kuepuka usumbufu wa kuchanja mara mbili.
Magufuli aliwakoroga watanzania wetu wajinga, akawajaza mambo ya ajabu kabisa, mama ana shida sana kuwabadili hawa watanzania maskini kwa sasa, ila tunaamini ataweza
 
Magufuli aliwakoroga watanzania wetu wajinga, akawajaza mambo ya ajabu kabisa, mama ana shida sana kuwabadili hawa watanzania maskini kwa sasa, ila tunaamini ataweza
Ni ukweli mkuu...ule utawala uliendesha propaganda kubwa sana ya uongo kuhusu ugonjwa wa Corona na hata chanjo, ambayo imekua ngumu kuiondoa vichwani mwa Watanzania wengi.
 
K
Ni ukweli mkuu...ule utawala uliendesha propaganda kubwa sana ya uongo kuhusu ugonjwa wa Corona na hata chanjo, ambayo imekua ngumu kuiondoa vichwani mwa Watanzania wengi.
Kwa hiyo ukweli kuhusu chanjo ya corona ni upi? Ulaya wanasema hawatambui chanjo zilizopelekwa Africa, jana kupitia BBC na aljazeera marekani wanasema tutapokea foreigner yeyote mwenye chanjo mchanganyiko. Hebu tupe ukweli kuhusu chanjo.
 
Back
Top Bottom