kitalolo
JF-Expert Member
- Dec 4, 2006
- 1,827
- 708
usiwaze kodi tunayotoa kumbuka amani inayopatikana inatoka wapi wenzako hawalali wanalinda mipaka kwa ajili yako wewe unaofanya biashara na kupulizwa upepo ikitokea vita watakaofaidi ni wanajeshi pekee wengine ni vilio tu mwanzo mwisho
kwa kuongezea pia sifikiri kuwa uwapo wa majeshi yetu kule ni matumizi ya kodi zetu zaidi sana tanzania italipwa fedha nyingi sana na Un kwa kupeleka majeshi kule ni sawa na mchezo wa pira kwamba wanajeshi wetu tuawauza kwa timu nyingine.
Pia iwao tutafanikiwa katika hiyo mision pamoja na sifa kwa Un wenyewe lakini pia ni sifa kwetu sisi kama taifa, pia tunawaongezea ujuzi wanajeshi wetu wote
mfano mzuri ni wale wanajeshi waliopigana kwenye vita vya Uganda waliijengea heshima nchi na walitizamwa kama wenye uzoefu zaidi kila mara sifa yao kubwa ilikuwa kuwa tulipigana vita ya uganda.
Tunajua kuwa haya ni maswala ya kimataifa zaidi hata South Afrika walipeleka majeshi yao huko Frika ya kati na wameuliwa kwa wingi sana leo hii wako kwenye maombolezo ya kitaifa pamoja na kwamba Raisi Zuma amekuwa akilaumiwa na wananchi wake kwa kupeleka majeshi huko lakini iwapo wangerudi salama na ushindi wa mission iliyowapeleka nafikiri Watu wa AFrika kusini wote wangejivunia hilo kuwa jeshi lao walau limeweza kutekeleza majukumu yao kitaifa na kimataifa na Rank ya S. Afrika kijeshi ingetazamwa kwa namana ya tofauti na sasa.
Yote sawa ikiwa tunaweza kufanya majukumu ya kitaifa na kimataifa basi na tuyafanye kwa maslai ya taifa na dunia kwa ujumla.
Kupatikanba kwa amani ya Congo ni jukumu letu sote na ninafikiri hapa UN wameona ni bora sasa kubadili na kuwa na Offensive Mandateto attack kuliko kujilinda kwakuwa na hawa waasi nao wamekuwa wakitumia njia hiyo kuongeza ujeuri sasa utaona silaa za waasi zitaanza kuwekwa chini kwa haraka sana yaani vikosi vya UN vikiingia tu kwenye nchi itabidi waasi wajisalimishe na kwa njia hii vita itakuwa raisi na haitatumia gharama kubwa na kutakuwa na kipindi cha mpito cha kuhakikisha amani na utulivu