Je, Tanzania itapeleka majeshi DRC?

Mr Chromium

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
2,088
2,703
Kufuatiwa mgogoro wa DRC/Congo dhidi ya M23 ambao umepelekea nchi wanachama wa Africa mashariki kupeleka vikosi vyake kupambana na kundi hilo la kiasi ambalo DRC inaishutumu Rwanda kulisupport kifedha, kiinteligencia na kijeshi.

Mpaka sasa nchi 5 kati ya 7 zimepeleka majeshi yake DRC /Nchi zote kasoro Tanzania na Rwanda ambayo imekataliwa isipeleke majeshi nchini humo.

Nchi zilizopeleka majeshi
1.Burundi
2.South Sudan
3.Kenya
4.Uganda

Nchi ambazo hazijapeleka
1.Tanzania
2.Rwanda (Imekataliwa)
C79A0DE8-EC06-4442-96BA-BE916157DD05.jpeg

Nini kinazuia Nchi hii kubwa kupeleka majeshi yake huko?

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

BURUNDI KUPELEKA WANAJESHI 100 DRC
Nchi ya Burundi imepeleka wanajeshi wake nchini DRC kwa ajili ya kukabiliana na mzozo wa waasi wa m23

Majeshi hayo ya burundi yanategemewa kwenda kuweka kambi maeneo ya Kitshanga na Kilorirwe.

SWALI LA KUJIULIZA ??
Kwanini maeneo hayo na si karibu na Goma au mpakani mwa Rwanda na Kongo.

Imefanya hivo kuepuka kushambuliwa na jeshi la Rwanda kwa mwavuli wa M23. Ikumbukwe kwamba Majeshi ya rwanda na Burundi hayapatani kutokana na tofauti za kisiasa na utawala. Rwanda inaongozwa na chama cha kitutsi wakati Burundi inaongozwa na chama cha Kihutu.

View attachment 2541035
View attachment 2541036
 
Kufuatiwa mgogoro wa DRC/Congo dhidi ya M23 ambao umepelekea nchi wanachama wa Africa mashariki kupeleka vikosi vyake kupambana na kundi hilo la kiasi ambalo DRC inaishutumu Rwanda kulisupport kifedha, kiinteligencia na kijeshi.
Mpaka sasa nchi 5 kati ya 7 zimepeleka majeshi yake DRC /Nchi zote kasoro Tanzania na Rwanda ambayo imekataliwa isipeleke majeshi nchini humo.
Nchi zilivopeleka majeshi
1.Burundi
2.South Sudan
3.Kenya
4.Uganda

Nchi ambazo hazijapeleka
1.Tanzania
2.Rwanda (Imekataliwa)
View attachment 2506851
Nini kinazuia Nchi hii kubwa kupeleka majeshi yake huko?
Jamani wacheni vijana wetu wapumziswe hata kidogo.

Si wametokako mwaka jana?

Wacha na wengine wakalinde bhana!
 
Kufuatiwa mgogoro wa DRC/Congo dhidi ya M23 ambao umepelekea nchi wanachama wa Africa mashariki kupeleka vikosi vyake kupambana na kundi hilo la kiasi ambalo DRC inaishutumu Rwanda kulisupport kifedha, kiinteligencia na kijeshi.

Mpaka sasa nchi 5 kati ya 7 zimepeleka majeshi yake DRC /Nchi zote kasoro Tanzania na Rwanda ambayo imekataliwa isipeleke majeshi nchini humo.

Nchi zilizopeleka majeshi
1.Burundi
2.South Sudan
3.Kenya
4.Uganda

Nchi ambazo hazijapeleka
1.Tanzania
2.Rwanda (Imekataliwa)
View attachment 2506851
Nini kinazuia Nchi hii kubwa kupeleka majeshi yake huko?
Tanzania imepeleka kupitia sadc
 
Tuna tatizo kubwa zaidi hapa mlangoni kwetu, Mozambique ndio tuelekeze nguvu zaidi
Kenya ina tishio la Al shababu kubwa kuliko hata lilo la wahuni wa msumbijii??

Kuna namna Tz inajitoa East africa
 
Kenya ina tishio la Al shababu kubwa kuliko hata lilo la wahuni wa msumbijii??

Kuna namna Tz inajitoa East africa
Mkuu with respect wale ISIS sio wahuni and don't undermine them, pata informations zao on the ground sio hizo politics, kule kuna tatizo zaidi ya uhuni!
 
Walipelekwa mwaka 2013 na mkataba wao umeisha mwaka jana.
Walikuwa chini ya UN na kikundi chao kilikuwa mchanganyiko pamoja na wanajeshi wengine kutoka nchi za Sadc kikundi hicho kilijulikana kama "Monusco"
Hujui maana ya munusco tulia upewe ukweli

USSR
 
Hujui maana ya munusco tulia upewe ukweli

USSR
Sasa jambo unapomueleza mwenzako halijui, si unalieleza wewe sasa kuliweka sawa?
Au na wewe unabishi tu huku haulewi chochote?
Kwanza eleza, Wanajeshi wa Tz, walikuweko Congo Drc ama hawakuwako?
 
Sasa jambo unapomueleza mwenzako halijui, si unalieleza wewe sasa kuliweka sawa?
Au na wewe unabishi tu huku haulewi chochote?
Kwanza eleza, Wanajeshi wa Tz, walikuweko Congo Drc ama hawakuwako?

yaan wabongo
 
Kupitia Umoja wa Mataifa( MONUSCO) Tanzania ina kikosi Congo cha Maaskari walinda amani. Toka mwaka 2013 hivi, ambapo nchi zinazochangia MONUSCO ni Tanzania askari kama 2,000, Malawi askari kama 300, South Africa askari kama 600, na Ukraine askari kama 800 (Ukraine kikosi chao kilijitoa MONUSCO mwaka jana kurudi nyumbani kuisaidia nchi yao kwa vita vyao na Urusi na waliondoka na vifaa vyao vya kijeshi). Kwahiyo Tanzania inachelewa kupeleka kikosi kwa njia ya Africa Mashariki kwa sababu ya kuepusha mgongano wa kimaslahi, kwamba haiwezekani ikawa na Kikosi cha kulinda amani cha MONUSCO alafu ikawa na kikosi pia cha kuondoa na kunyang'anya siraha waasi. Kofia mbili azitakiwi.
 
Back
Top Bottom