Tanzania kupanda kuwa uchumi wa kati chini: Mkapa amechangia 194%; JK 96% na Magufuli 10%

Kwanini asilimia 10 tu,,huoni maendeleo?,tumefufua shirika la ndege,reli ,umeme sasa haukatiki,,reli ya umeme,,stand ya dodoma,soko kuu dodoma,,stand kuu ya mabasi dsm,daraja za salenda,,meli mv victory,,daraja la busisi,,mafanikio ni mengi mengi..
Mlevi wewe 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
GAZETI RAIA MWEMA,30/05/2012
Mohamedimtoi
WAZIRI WA VIWANDA NA KILIMO BILA KILIMO.
tangamano
tangamano
8 years ago

Advertisements

MACHI 2008, mshauri mmoja wa viwanda kutoka Japan aliletwa nchini na Rais Jakaya Kikwete kuishauri serikali yake namna inavyoweza kuleta “Mapinduzi ya Viwanda” hapa nchini.

Kitendo kile cha Rais Kikwete kuleta mshauri huyo kutoka Japan kulinifanya, wakati ule, nijenge imani kuwa rais wetu alikuwa amepania kweli kweli kuifanya Tanzania kuwa tena nchi ya viwanda na kilimo.
Miaka minne na nusu sasa imeshapita tangu mshauri yule wa viwanda kutoka Japan amalize kazi yake ya kumshauri Rais Kikwete juu ya suala hilo, na bado hakuna dalili yoyote ya kujengwa viwanda vipya hapa nchini; achilia mbali kufufua vile vilivyokuwa vya umma vilivyouzwa kwa wawekezaji binafsi, na kisha vikatelekezwa au vikageuzwa maghala.

Sina hakika na hili, lakini naamini ya kuwa tangu Rais Kikwete aingie madarakani, karibu miaka saba iliyopita, hakuna kiwanda kipya chochote kikubwa kilichojengwa nchini, na hapa naamanisha kiwanda kikubwa
(heavy industry), na si hivi vya kusindika matunda au nafaka vya Bakhressa na Mohamed Enterprises.
Miaka saba ya utawala wa Rais Kikwete bila kujengwa viwanda vipya vikubwa nchini kumenikumbusha kauli iliyotolewa na mshauri yule wa viwanda wa Japan kabla hajaondoka nchini.

Mshauri yule, Yoshiyasu Mizuno, alinukuliwa na gazeti la Serikali la
Daily News, toleo la Machi 6, 2008, akisema kwamba kuyafikia Mapinduzi ya Viwanda si lelemama.
Alisema ya kuwa, ili Tanzania iweze kufikia malengo ya maendeleo iliyojiwekea katika
Visheni 2025 (ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda), ni lazima uchumi ukue kwa asilimia 15.6 kwa mwaka na iendelee kwa kiwango hicho hicho kwa miaka 18 mfululizo!

Lakini wiki iliyopita tuliambiwa na Gavana wa Benki Kuu (BOT), Profesa Benno Ndulu, kwamba uchumi wa Tanzania, kwa mwaka jana, ulikua kwa kiwango cha asilimia 6.5 tu. Sasa, asilimia 6.5 na asilimia 15.6 za Mjapani huyo ni wapi kwa wapi?!

Mimi si mchumi, lakini kwa kiwango changu kidogo cha elimu bado natambua kwamba si lelemama uchumi wetu kukua haraka kutoka kiwango chake cha sasa cha takriban asilimia saba na kufikia asilimia 15.6 alichokitaja Mjapani huyo; achilia mbali lile sharti jingine la uchumi kusimama katika kiwango hicho hicho cha asilimia 15.6 kwa miaka 18 mfululizo.

Ukizingatia nidhamu yetu mbovu ya uchapaji kazi, na ukizingatia hali ya kushamiri kwa ufisadi katika karibu kila sekta serikalini, na bila kusahau kuwa sekta ya viwanda ni kama vile haipo hapa nchini, na ukizingatia ukweli pia kwamba mawaziri wengi na ma-DC hujishughulisha zaidi na kusaka utajiri kuliko kulichapia kazi taifa, utaelewa ni kwa nini si rahisi kwa Tanzania hii, chini ya chama tawala CCM, kufikia kiwango cha kukua kwa uchumi cha asilimia 15.6 katika miaka ya karibuni.

Na ndiyo maana miaka karibu minne na ushee hivi imeshakatika tangu Mjapani yule aishauri Serikali ya Kikwete namna ya kufikia Mapinduzi ya Viwanda hapa nchini, lakini mpaka sasa bado hakuna viwanda vyovyote vikubwa ambavyo vimeanza kujengwa.

Sana sana tunachokisikia ni majuto au tuseme ni kujikosha kwa watawala wetu na dhambi ile kubwa waliyoifanya inayoendelea kuwatafuna ya kuuza na kuua viwanda vilivyoanzishwa enzi za utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Mwanzoni mwa mwaka huu, kwa mfano, tulimsikia aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akikiri kwamba kama kuna kitu alichokisahau wakati wa utawala wake ni kuendeleza kilimo! Huyo huyo Mkapa, baadaye, akanukuliwa tena akisema ya kuwa haiwezekani Tanzania kumaliza tatizo la ajira bila kujenga viwanda.

Hebu fikiria: Rais wa nchi anawezaje kukisahau kilimo; ilhali asilimia 85 ya wananchi wake wanajishughulisha nacho? Hebu fikiria: Mkapa atasemaje kuwa hatuwezi kumaliza tatizo la ajira bila kujenga viwanda wakati ndiye aliyesimamia kuviuza, kwa bei poa, tulivyokuwanavyo kwa wawekezaji wababaishaji ambao wamevitelekeza?

Ndiyo maana huwa najiuliza: Hivi Rais Kikwete alifikiria nini kumleta Mjapani yule mwaka 2008 kuishauri Serikali yake namna ya kufikia Mapinduzi ya Viwanda wakati tulikuwanavyo tukaviua?

Nina shaka kwamba hata chuma kilichovumbuliwa kule Liganga kitaishia Beijing kwenye viwanda vya Wachina badala ya kitusaidie kuyafikia haraka Mapinduzi ya Viwanda.

Ingekuwa ni enzi zile za utawala wa Mwalimu Nyerere ambapo tayari tulikuwa na viwanda kemkem, vikiwemo vilivyotumia mazao ya wakulima kama vile Mwatex, Sunguratex na Mutex, ni dhahiri chuma cha Liganga kingeharakisha zaidi safari yetu ya kuwa nchi ya viwanda vikubwa. Nasema hivyo; maana tulikuwa na pa kuanzia.

Lakini kwamba sasa watawala wanayatamani Mapinduzi ya Viwanda baada ya kuwa wameua viwanda vyote, ni kitu ambacho, kwa hakika, kinakaribisha maswali mengi hadi sasa juu ya umakini wetu na uwezo wetu wa kufikiri.

Na ndio maana, binafsi, sishangai kwamba miaka minne na nusu imepita tangu aletwe mshauri yule wa viwanda kutoka Japan, na bado hakuna kiwanda kikubwa hata kimoja ambacho kimejengwa nchini.

Kwa hakika, kuna wakati huwa najiuliza kama bado kuna umuhimu wowote, kwa sasa, kuwa na wizara ya viwanda yenye mawaziri wawili. Wizara ya viwanda inayosimamia viwanda vipi hasa?

Hivi kazi ya kila siku ya waziri wetu wa viwanda ni ipi? Vyovyote vile; waziri anayeisimamia wizara hiyo kwa sasa namshauri atembelee Kiwanda cha Nguo cha Urafiki cha Dar es Salaam ajionee kinavyogeuzwa, kidogo kidogo, kuwa yadi ya kuuzia magari!

Aidha, katika hali ya kawaida, mtu angetaraji kwamba baada ya Serikali ya CCM kusambaratisha viwanda na ndoto ya Mapinduzi ya Viwanda kuyeyuka licha ya ujio wa mshauri huyo kutoka Japan, sasa nguvu zote zingeelekezwa katika kampeni ya kufikia Mapinduzi ya Kilimo
(Green Revolution), lakini wapi!
Licha ya kwamba asilimia 85 ya Watanzania ni wakulima wadogo wadogo wanaoishi vijijini, serikali bado imewatelekeza ingawa ina programu yake maarufu ya kinadharia zaidi inayoitwa Kilimo Kwanza.

Rais Kikwete aliibuka na hicho kinachoitwa Kilimo Kwanza, lakini matunda yake mpaka sasa hayaridhishi. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kila nilipopata bahati ya kutembelea vijiji vya mikoa kadhaa nchini nimekuwa nikijitahidi kutafuta ushahidi wa mabadiliko ya kilimo chetu yanayotokana na ujio huo wa Kilimo Kwanza. Nikiri kuwa sikuyaona.

Na hata watawala wenyewe ni mara chache mno utawasikia wakienda vijijini kuhimiza Kilimo Kwanza au angalau kwenda kufanya tathmini zao wenyewe za papo kwa papo za mafanikio ya huo ujio wa Kilimo Kwanza. Lakini sivyo wanavyofanya; kwani wanapapatikia zaidi safari za Ughaibuni kuliko za vijijini, na hasa Rais Kikwete.

Hivi ni mara ngapi umepata kuwasikia watawala wetu wakitembelea vijiji vyetu kuhimiza kilimo kama alivyokuwa akifanya Mwalimu Nyerere enzi zake? Hivi ni mara ngapi umepata kuziona juhudi za wazi wazi za watawala wetu za kuwaelemisha wakulima wetu vijijini kuhusu kilimo bora?

Ndugu zangu, ninachosema ni kwamba, chini ya Serikali ya CCM, ni ndoto kwa Tanzania kufikia Mapinduzi ya Kilimo, na ni ndoto zaidi kufikia Mapinduzi ya Viwanda.
Ni kweli tunao mawaziri wa kusimamia sekta hizo mbili, lakini ukweli ni kwamba wapo kama hawapo! Mambo yakienda hivi hivi, kuna hatari huko mbele ya safari tukawa na Waziri wa Kilimo asiyesimamia kilimo chochote, na tukawa pia na Waziri wa Viwanda asiyesimamia viwanda vyovyote!
Hayo, ndugu zangu, ndiyo mavuno ya hadaa za ushauri wa mabeberu wa dunia.

Tulihadaiwa na asasi za
Bretton Woods za Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) tukauza viwanda vyetu na kuiua sekta ya viwanda. Tena watawala walifanya hivyo kwa ukaidi mkubwa; huku wakiwakejeli wale waliowapinga akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Tukumbushane: Akihutubia kwenye sherehe za Mei mosi, 1995, mjini Mbeya, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hivi kuhusu uuaji huo wa sekta ya viwanda nchini:
“Nchi haiwezi kuendelea hata kidogo kwa kupuuza viwanda. Nchi tajiri duniani zenye viwanda huvibana vinchi vidogo viache mambo ya viwanda. Taabu yetu ni kwamba wala viongozi wetu hawakatai.

Wanakubali tu. Lakini sisi ni madodoki?”Lakini walimsikiliza Mwalimu Nyerere, wakampuuza. Wakaendelea kuviuza viwanda vyetu kwa wawekezaji wababaishaji. Baada ya kumaliza kuviuza na kuviua na nchi kugeuka kuwa dampo la bidhaa hafifu za nje, eti sasa ndo wanayatamani Mapinduzi ya Viwanda! Eti sasa ndo wanazinduka na kutambua kuwa bila kujenga viwanda hatuwezi kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu nchini!

Lakini jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba bado wanaendelea kuuamini ushauri wa mabeberu kuhusu sekta yetu nyingine – sekta ya kilimo. Majuzi hapa Rais Kikwete aliitwa Marekani na Rais Obama ili kupewa “mwongozo” wa namna ya kuendesha sekta ya kilimo nchini.

Kina Obama walimwambia kwamba eti mkombozi wetu ni kilimo cha wawekezaji wakubwa kutoka nje, na kwamba hilo ndilo tulipe kipaumbele badala ya kung’ang’ania kuwaendeleza wakulima wetu wadogo wadogo nchini!

Kwa ushauri huo wa Washington ambao tayari watawala wetu wameshaukubali, miaka si mingi sehemu kubwa ya ardhi yetu yenye rutuba nchini itaangukia mikononi mwa umiliki wa wawekezaji hao wa kigeni – mambo yale yale ya zama za ukoloni!

Na japo tunapozwa hivi sasa na watawala wetu kwa kupigiwa kibwagizo cha wimbo wa
land for equity, yaani kwamba tutabaki na asilimia 25 ya hisa katika kila mradi wa kilimo kikubwa cha biashara kitakachoanzishwa na wawekezaji wa kigeni, shaka yetu iko pale pale.

Na shaka yenyewe ni kwamba, mwisho wa yote, sehemu kubwa ya ardhi yetu yenye rutuba itamilikiwa na Wazungu (mwenye asilimia 75 ya hisa ndiye mmiliki), na kwamba wazawa wengi watakuwa manamba (vibarua) tu katika mashamba hayo makubwa yatakayomilikiwa na Wazungu.

Hilo likihitimishwa, je sisi kama taifa tutakuwa tumeshika wapi? Nauliza hivyo; maana kwenye viwanda tulifuata ushauri wao tukaviuza vyote na kuiua sekta hiyo, na kisha tukageuka kuwa soko la bidhaa za viwanda vyao.

Na sasa hao hao wanataka tuachane na kukiendeleza kilimo cha wakulima wadogo wadogo ambao ndio wengi Tanzania, na badala yake tutegemee kilimo kikubwa kitakachoendeshwa na Wazungu kutoka Ughaibuni!
Hebu niambieni: Hayo yakihitimishwa, je, hatma ya uchumi na usalama wa taifa letu bado utakuwa mikononi mwetu wenyewe?
Tafakari.

Makala kwa hisani kubwa ya gazeti la :

GAZETI RAIA MWEMA,30/05/2012

Source : WAZIRI WA VIWANDA NA KILIMO BILA KILIMO.:
 
Huu ndio ukweli ambao baadhi ya watu wanauchukia. Utakisikia, "Toka 2015, shule zimejengwa kadhaa, hospitali zimejengwa...., viwanda...., nk". Hautasikia, "Toka 1961 hadi 1885 (Nyerere), 1985-1995 (Mwinyi), 1995-2005 (Mkapa) na 2005-2015 (Kikwete) kulijengwa viwanda..." Hautasikia hilo. Ukisikia sana, itakuwa "Viwanda vimejengwa ktk miaka 5 kuliko awamu zote". Hautapewa idadi ya awamu zote ikilinganishwa na awamu hii.

Watu tulivyowekewa woga, uzi huu unaweza hata kufutwa. Siyo kwa sababu umeongopa ila kwa sababu umesema ukweli ambayo baadhi ya watu hawapendi kusikia. Sijui kuna faida gani kuongopa. Awamu hii imefanya yake mazuri pia, lakini unaweza kumpandisha mtu bila kuwashusha wengine. Tanzania ni nyumba ambayo ujenzi wake hauna mwisho. Kila anayekuja anaweka matofali yake. Muda wake ukipita, anamwachia mwingine bila ya kumdharau aliyepita.

Wewe ni mchochezi tutakupima mkojo
 
Kumbe nyie mna kisa na magufuli,zile ngonjera za kua ccm inaturudisha nyuma ni uongo.
Hivi sasa umasikini limeongezeka, bahati mbaya yote hayo yanafanyika bila hata kujua idadi halisi ya watu waliomo Tanzania, ni makisio tu. Tanzania ilifanya sensa iliyotoa idadi angalau yenye uhakika ni ya mwaka 1967 lakini zilizofuata ni za kugushi tu na sijui kama sensa bado ipo.
 
Kuna watu waliotumbuliwa,vyeti feki,na wale walio zibiwa mianya ya wizi, kutwa kucha wako mitandaoni wakishirikiana na wanasiasa wenye uchu wa kwenda Ikulu kuponda Rais na serikali yake kujaribu kuaminisha uma kua hafai,wananchi wenye akili tunajua A-Z ya kwamba JPM ni jembe kuliko kiongozi yoyote wa juu hapa Africa. Hivyo tu

Mkuu naomba unisaidie maana Mimi sielewi. Inamaana hizo data alizotoa hapo juu siyo za kweli? Naomba unisaidie kunipa data za ukweli ndugu maana wanatuchanganya Hawa watu.
 
CHADEMA wamekuwa wapiga kampeni wa CCM!

Hayo yote ni mafanikio ya CCM kupitia serikali zake!

Tanzania hatuna vyama vya upinzani bali tuna wanaharakati!
Hizi sasa ndio akili za pure mwafrika!!! Nchi ni zaidi ya vyama, na sio kwamba maendeleo yanaletwa na wana ccm tu!! Kodi inalipwa na kila mwananchi,kama hakuna vyama vya upinzani bali ni wanaharakati, mbona sasa hamjiamini?? Mnatumia nguvu nyingi tena kwa kusaidiwa na polisi?!! Kwa mazuri anayofanya meko nilijua tu kuwa vyama vya upinzani vingekufa natural death!! Sio kwa mabomu!!! Upinzani ni itikadi hata kibaki chama kimoja bado upinzani utakuwepo tu mioyoni mwa watu!!
 
Kumbe nyie mna kisa na magufuli,zile ngonjera za kua ccm inaturudisha nyuma ni uongo.
Ccm na magufuli kwa pamoja vimechangia kuturudisha nyuma.
kumbuka wakati tunapata uhuru tulikua sawa na Singapore, Malaysia lakini leo zaidi ya nusu karne tunazungumzia GDP ya $ 1093 huku viongozi wanalazimisha tushangilie tumefika uchumi wa kati.
 
Asante Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati

Tukikuongezea miaka kumi tutaipiku USA

Sasa nadhani ugonjwa umeshafika kwenye ubongo. Kilichobaki ni kushindwa kuvuka barabara!! Sasa unaelekea kuwa mropokaji tu.

Hata mwaka 1776, USA ilikuwa mbali sana kuliko ilivyo Tanzania mwaka 2020. Leo bado unazungumzia maji safi na salama, elimu bure, miundombinu. Walishatoka huko!!
 
Kuna watu waliotumbuliwa,vyeti feki,na wale walio zibiwa mianya ya wizi, kutwa kucha wako mitandaoni wakishirikiana na wanasiasa wenye uchu wa kwenda Ikulu kuponda Rais na serikali yake kujaribu kuaminisha uma kua hafai,wananchi wenye akili tunajua A-Z ya kwamba JPM ni jembe kuliko kiongozi yoyote wa juu hapa Africa. Hivyo tu
Mataga unajuwa kuna chi za Kiafrika wazungu wananyimwa visa kwa kuwa wanaweza kuzamia?
 
Hapa chini ni historical trend (source ni World Bank) ya ongezeko la per capita income kwa Tanzania kuanzia awamu ya 3 (Mkapa), halafu ya 4 (JK ) hadi ya sasa ya 5 (Magufuli).

Ni wazi kuwa kila rais katika awamu hizo 3 amechangia kwa kiasi kikubwa kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati chini.

Mkapa: ongezeko la 194% (sawasawa na $ 330)

JK: ongezeko la 96% (sawasawa na $ 480)

Magufuli: ongezeko la 10% (sawasawa na $ 100)

In terms of %, aliyeongoza ni Mkapa na mwisho ni Magufuli.

In terms of absolute figures, aliyeongoza ni JK na wa mwisho ni Magufuli.


Nawaomba Watanzania tuwatambue vinara (walioongoza yaani Mkapa & JK) waliotufikisha hatua hii. Mungu awabariki sana hawa wazee wetu marais wastaafu.

View attachment 1496609
Pamoja na hayo yote uliyoyaweka.Jambo moja ni lazima tujiulize.
-WHY NOW just before General Election this middle income subject has just emerged?
-Kwa NINI JAMBO HILI la "UCHUMI wa KATI" ndo LIMETOKEA kabla ya UCHAGUZI MKUU?
Jibu ni kuwa TAYARI jamii ya KIMATAIFA imemkubali rais Magufuli na hiII ni kutoa "INDIRECT ENDORSEMENT"
kwamba huyu ANAIFAA Tanzania.

Na Wangependa kufanya kazi naye maana wameiona juhudi zake.
Kama wewe ni pundits/Mchambuzi wa mambo ya kimataifa unielewa. Na kama sivyo itakuwa hutanielewa kuwa ninasema nini.

IMPORTANT/LA NUHIMU sana:
Hapa si mambo ya KUWADHARIRISHA, Mwal.NYERERE, MKAPA, MWINYI wa KIKWETE, maana nao pia walitoa MCHANGO mkubwa katika taifa hili . ISIPOKIWA hii ni kuwa international community/Jamii ya Kimataifa IMEMKUBALI JPM
Na hili limekuja kabla ya uchaguzi likiwaambia Watanzania
"MAGUFULI NDO SULUHISHO LA NCHI YENU MCHAGUENI TENA."
 
Back
Top Bottom