Tanzania kupanda kuwa uchumi wa kati chini: Mkapa amechangia 194%; JK 96% na Magufuli 10%

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,035
2,000
Hapa chini ni historical trend (source ni World Bank) ya ongezeko la per capita income kwa Tanzania kuanzia awamu ya 3 (Mkapa), halafu ya 4 (JK ) hadi ya sasa ya 5 (Magufuli).

Ni wazi kuwa kila rais katika awamu hizo 3 amechangia kwa kiasi kikubwa kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati chini.

Mkapa: ongezeko la 194% (sawasawa na $ 330)

JK: ongezeko la 96% (sawasawa na $ 480)

Magufuli: ongezeko la 10% (sawasawa na $ 100)

In terms of %, aliyeongoza ni Mkapa na mwisho ni Magufuli.

In terms of absolute figures, aliyeongoza ni JK na wa mwisho ni Magufuli.

Nawaomba Watanzania tuwatambue vinara (walioongoza yaani Mkapa & JK) waliotufikisha hatua hii. Mungu awabariki sana hawa wazee wetu marais wastaafu.

20200703_173955.jpg
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
3,090
2,000
Huu ndio ukweli ambao baadhi ya watu wanauchukia. Utakisikia, "Toka 2015, shule zimejengwa kadhaa, hospitali zimejengwa...., viwanda...., nk". Hautasikia, "Toka 1961 hadi 1885 (Nyerere), 1985-1995 (Mwinyi), 1995-2005 (Mkapa) na 2005-2015 (Kikwete) kulijengwa viwanda..." Hautasikia hilo. Ukisikia sana, itakuwa "Viwanda vimejengwa ktk miaka 5 kuliko awamu zote". Hautapewa idadi ya awamu zote ikilinganishwa na awamu hii.

Watu tulivyowekewa woga, uzi huu unaweza hata kufutwa. Siyo kwa sababu umeongopa ila kwa sababu umesema ukweli ambao baadhi ya watu hawapendi kusikia. Sijui kuna faida gani kuongopa. Awamu hii imefanya yake mazuri pia, lakini unaweza kumpandisha mtu bila kuwashusha wengine. Tanzania ni nyumba ambayo ujenzi wake hauna mwisho. Kila anayekuja anaweka matofali yake. Muda wake ukipita, anamwachia mwingine bila ya kumdharau aliyepita.
 
mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,233
2,000
Huu ndio ukweli ambao baadhi ya watu wanauchukia. Utakisikia, "Hadi 2015, shule zilikuwa kadhaa, hospitali zilikuwa...., viwanda...., nk". Hautasikia, "Toka 1961 hadi 1885 (Nyerere), 1985-1995 (Mwinyi), 1995-2005 (Mkapa) na 2005-2015 (Kikwete) kulijengwa viwanda..." Hautasikia hilo. Ukisikia sana, itakuwa "Viwanda vimejengwa ktk miaka 5 kuliko awamu zote". Hautapewa idadi ya awamu zote na awamu hii.
Kwa mnyonge anafaidika na nini hebu tuelimesheni
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,549
2,000
Kwanini asilimia 10 tu,,huoni maendeleo?,tumefufua shirika la ndege,reli ,umeme sasa haukatiki,,reli ya umeme,,stand ya dodoma,soko kuu dodoma,,stand kuu ya mabasi dsm,daraja za salenda,,meli mv victory,,daraja la busisi,,mafanikio ni mengi mengi..
 
siyo mimi ndugu, ni World Bank ambao sasa wanashangiliwa na MATAGA kwa kui upgrade nchi yetu!
 
RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
786
1,000
Hapa chini ni historical trend (source ni World Bank) ya ongezeko la per capita income kwa Tanzania kuanzia awamu ya 3 (Mkapa), halafu ya 4 (JK ) hadi ya sasa ya 5 (Magufuli).

Ni wazi kuwa kila rais katika awamu hizo 3 amechangia kwa kiasi kikubwa kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati chini.

Mkapa: ongezeko la 194% (sawasawa na $ 330)

JK: ongezeko la 96% (sawasawa na $ 480)

Magufuli: ongezeko la 10% (sawasawa na $ 100)

In terms of %, aliyeongoza ni Mkapa na mwisho ni Magufuli.

In terms of absolute figures, aliyeongoza ni JK na wa mwisho ni Magufuli.

Nawaomba Watanzania tuwatambue vinara (walioongoza yaani Mkapa & JK) waliotufikisha hatua hii. Mungu awabariki sana hawa wazee wetu marais wastaafu.

View attachment 1496609
Umetumwa na mabeberu kumchafua rais wetu mpendwa na taifa kwa ujumla!
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,166
2,000
Kuna watu waliotumbuliwa,vyeti feki,na wale walio zibiwa mianya ya wizi, kutwa kucha wako mitandaoni wakishirikiana na wanasiasa wenye uchu wa kwenda Ikulu kuponda Rais na serikali yake kujaribu kuaminisha uma kua hafai,wananchi wenye akili tunajua A-Z ya kwamba JPM ni jembe kuliko kiongozi yoyote wa juu hapa Africa. Hivyo tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom