Tanzania kuondolewa orodha ya nchi maskini

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
912
Points
1,000

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
912 1,000
1574414014313.png

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Biashara (UNCTAD), limezindua ripoti ya mwaka 2019 kuhusu nchi maskini zaidi duniani.

Shirika hilo limebainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo katika hali chanya kwa kufanya vizuri, kuweza kuondoka katika orodha ya nchi maskini. Imebainisha kuwa Tanzania inafanya vizuri, ikiwa na taasisi imara, uongozi imara na mapambano dhidi ya rushwa.

Akiwasilisha ripoti hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mchumi kwa Nchi Zinazoendelea (LDC), Benjamin Banda alisema Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kuondoka katika kundi la nchi maskini. Alisema Tanzania ina uongozi imara, lakini pia ikielekeza usimamizi imara hata fedha za misaada kutoka nje ya nchi, zinaelekezwa sehemu zinazofaa, lengo likiwa ni kutoka kwenye kundi la nchi maskini.

Kuhusu ripoti, alisema nchi itastahili kuondoka kwenye kundi la nchi maskini, ikiwa itakidhi viwango vya juu vya kutoka, angalau kwa vigezo viwili kati ya vitatu na katika uhakiki. Alisema miongoni mwa vigezo ni ikiwa wastani wa pato la kila mtu la kitaifa la miaka mitatu la nchi maskini, limeongezeka kwa kiwango angalau mara mbili ya kiwango cha juu, yaani dola za Marekani 2,460.

“Hii ina maana kwamba mpaka mwaka 2018 kulikuwa na nchi 12 zinazostahili au kukaribia kuondoka kwenye kundi la nchi maskini,” alisema Banda.

Alisema kutoka na ripoti hiyo, UNCTAD inazitaka nchi maskini duniani, kuchukua jukumu kubwa la kuelekeza msaada wa nje katika maendeleo. Alisema mataifa yaliyo masikini zaidi duniani, yanapaswa kuhakikisha fedha kutoka vyanzo vyote vya nje, vinaelekezwa kwenye vipaumbele vya maendeleo ya taifa, mbinu hii ni njia bora ya kusimamia utegemezi wao wa msaada na hatimaye kuuepuka.

Alisema ili nchi hizo zifikie Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), lazima zichukue umiliki wa ajenda yao ya maendeleo na kusimamia mgawo wa fedha za maendeleo ya nje katika mpangilio na vipaumbele vyao vya maendeleo ya taifa.

“Jumuiya ya kimataifa pia inahitaji kutoa msaada wake kwenye lengo hilo la kawaida,” alisema.

Akitoa neno la shukrani, Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Michael Dunford alisema ripoti hiyo inatoa fursa kwa uchambuzi kijamii na kiuchumi na kupata data zitakazoboresha nchi.

Alisema ni ripoti inayotoa taarifa zinazotakiwa, ikitaka pia fedha kutoka nje kuelekezwa katika uwekezaji stahiki jambo litakalokuza uchumi. Alisema mashirika ya UN yaliyoko nchini Tanzania, yako mbele kusaidia serikali kufikia malengo enddlevu ya maendeleo na kutekeleza program mbalimbali za maendeleo. Nchi maskini zinahusisha nchi 15 kati ya 20, zinazotegemea zaidi msaada duniani kutokana na upungufu wa mara kwa mara katika akiba zao za nyumbani.

Chanzo: Habari Leo
 

stella1975

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Messages
460
Points
1,000

stella1975

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2018
460 1,000
Influenza, Hayo ni mambo ambayo yanafanyika Tanzania kuficha uchafu, nguvu nyingi sana inatumika kuficha uchafu kwenye nchi hii, watu wanaweza kumtuma hata kigogo anayekula nchi akatafutiwa nafasi kwa njia yoyote ile akaingia umoja wa mataifa akasema Tanzania ndio nchi ya kwanza duniani tajiri halafu ikatangazwa kuwa umesema umoja wa mataifa, yani kuna nguvu kubwa inafanyika kusifia tu eti rushwa imetibitishwa.

Wakati huo huo Waziri Mkuu anaunda tume ya kuchunguza rushwa ya bilioni 40 Wakati huo huo mkaguzi wa serikali anasema zimepigwa tilioni 1.5.

Wakati huo huo rushwa na upotefu wa hela unaripotiwa, ujue Hakuna awamu ambayo hela za umma zimepotea kama awamu hiii, na jiulize kuwa nchi inadai kuwa imevuka makusanyo ya mapato na kuvunja rekodi chukua hizo hela ongeza tilioni zaid ya 20 zilizokopwa halafu rudi tuambie kuwa hizo hela zimeenda wapi? Maana mtatuambia ndege na reli basi jumlisha hivyo vyote muone kuwa hata nusu haifiki hizo pesa zilizokopwa
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Messages
3,938
Points
2,000

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2007
3,938 2,000
Influenza,
Watuondoe au wasituondoe, sisi ni HAPA KAZI TU hakuna kingine! Hatufanyi maendeleo kwa lengo la kupata opinions za watu, tunafanya maendeleo kwa lengo la kuondoa umaskini wa wa-Tanzania.

Kwa mfano, tukifanya maendeleo halafu kukawa na opinions za wengine ambazo ni negative, INAKUWA NI BORA ZAIDI KWETU, kuliko kutokuwa na maendeleo halafu mkavimbishwa vichwa na watu wengine kwa opinions positive. What we are doing at the moment is what matters most than some other peoples' opinionsome other peoples' opinions
 

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Messages
462
Points
500

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined May 31, 2018
462 500
1574485726082.png


SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Biashara (UNCTAD), limezindua ripoti ya mwaka 2019 kuhusu nchi maskini zaidi duniani. Shirika hilo limebainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo katika hali chanya kwa kufanya vizuri, kuweza kuondoka katika orodha ya nchi maskini. Imebainisha kuwa Tanzania inafanya vizuri, ikiwa na taasisi imara, uongozi imara na mapambano dhidi ya rushwa.

Akiwasilisha ripoti hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mchumi kwa Nchi Zinazoendelea (LDC), Benjamin Banda alisema Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kuondoka katika kundi la nchi maskini. Alisema Tanzania ina uongozi imara, lakini pia ikielekeza usimamizi imara hata fedha za misaada kutoka nje ya nchi, zinaelekezwa sehemu zinazofaa, lengo likiwa ni kutoka kwenye kundi la nchi maskini.

Kuhusu ripoti, alisema nchi itastahili kuondoka kwenye kundi la nchi maskini, ikiwa itakidhi viwango vya juu vya kutoka, angalau kwa vigezo viwili kati ya vitatu na katika uhakiki. Alisema miongoni mwa vigezo ni ikiwa wastani wa pato la kila mtu la kitaifa la miaka mitatu la nchi maskini, limeongezeka kwa kiwango angalau mara mbili ya kiwango cha juu, yaani dola za Marekani 2,460.

“Hii ina maana kwamba mpaka mwaka 2018 kulikuwa na nchi 12 zinazostahili au kukaribia kuondoka kwenye kundi la nchi maskini,” alisema Banda. Alisema kutoka na ripoti hiyo, UNCTAD inazitaka nchi maskini duniani, kuchukua jukumu kubwa la kuelekeza msaada wa nje katika maendeleo.

Alisema mataifa yaliyo masikini zaidi duniani, yanapaswa kuhakikisha fedha kutoka vyanzo vyote vya nje, vinaelekezwa kwenye vipaumbele vya maendeleo ya taifa, mbinu hii ni njia bora ya kusimamia utegemezi wao wa msaada na hatimaye kuuepuka.

Alisema ili nchi hizo zifikie Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), lazima zichukue umiliki wa ajenda yao ya maendeleo na kusimamia mgawo wa fedha za maendeleo ya nje katika mpangilio na vipaumbele vyao vya maendeleo ya taifa. “Jumuiya ya kimataifa pia inahitaji kutoa msaada wake kwenye lengo hilo la kawaida,” alisema.

Akitoa neno la shukrani, Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Michael Dunford alisema ripoti hiyo inatoa fursa kwa uchambuzi kijamii na kiuchumi na kupata data zitakazoboresha nchi. Alisema ni ripoti inayotoa taarifa zinazotakiwa, ikitaka pia fedha kutoka nje kuelekezwa katika uwekezaji stahiki jambo litakalokuza uchumi.

Alisema mashirika ya UN yaliyoko nchini Tanzania, yako mbele kusaidia serikali kufikia malengo enddlevu ya maendeleo na kutekeleza program mbalimbali za maendeleo. Nchi maskini zinahusisha nchi 15 kati ya 20, zinazotegemea zaidi msaada duniani kutokana na upungufu wa mara kwa mara katika akiba zao za nyumbani.
 

Forum statistics

Threads 1,379,335
Members 525,398
Posts 33,744,320
Top