Tanzania kuna fursa asilimia 98% ila hizi ndizo sababu kuonekana hakuna fursa

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,721
Nitashangaa mtanzania kukimbia nchi kubwa kutafuta fursa ila riziki ni popote.

Tanzania yetu kuna fursa nyingi ukijumlisha na ardhi yetu ambayo mpaka leo kuna nchi au watu wanatamani kupata hii nchi.

Fursa zilizopo kwangu naziweka asilimia 98% mpaka sasa azijatumika.

Ila kutokuonekana fursa hizi kuna sababishwa na haya:

Kukosekana kwa sera safi na utawala

hili suala linachangia asilimia kubwa hapa Tanzania na kusababisha mambo mengi kutupita huku dunia ikienda kasi.

Ubinafsi na watawala kujilimbikizia

ubinafsi umeshika kasi na hata wanaoshikilia fursa wanabaki nazo na kuzidi kuzichukua wao na wabaki wao kama wao kuanzia mtu mmoja, vikundi vya watu na n.k

Kukosekana kwa bajeti na mfumo mzuri wa kukopesheka
Kiukweli watu wengi wana fursa ya kufika mbali na kuweza kufanya mazuri lakini haya yanapelekea kushindwa.

Kama haya yatafuatwa basi kuna uwezo watu wakafungua vitu vingi na bila shida
 
Kijani ndio chanzo cha yote, kamekua ka kikundi ka wachache wezi na mafisadi.

Hawajali tena kuhusu wanachi kwa ujumla bali matumbo yao na familia zao.

Mission iwe kuiondoa madarakani CCM ili tu reset factory.

Sio mbaya kuanza upya kisiasa na uongozi hawa wamesha poteza dira..na hawawezi rekebishika tena.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nadhani ndo maana mtoa hoja amesema sera za nchi sio nzuri.

Na mimi niunge mkono kuwa sera sio nzuri kuhusu kilimo kabla hatujaanza kujadili hoja za mabenki kukopesha wakulima.

Kuna ardhi nyingi sana tanzania ambayo unakuta mtu anatumia nguvu zake kulima na mtaji kidogo kupata mbegu ya zao husika,lakini akishavuna mkono wa serikali kumpangia namna ya kuuza huu hapa bila kujali amepataje hayo mazao anayotaka kuyauza ili atoke kimaisha.

Nitoe mfano mdogo kuhusu zao la kahawa mkoani Kagera, wafuatiliaji wa vyombo vya habari watakumbuka hivi majuzi mkuu wa wilaya ya karagwe alitoa tamko juu ya kuwakamata watu wanaouza kahawa kimagendo.

Hiyo inayoitwa magendo ni kwamba watu kutoka uganda wanakuja na pesa nzuri mikoa ya kagera kununua kahawa tena nyumbani kwa mkulima na wanatoa pesa nzuri kulinganisha na fedha inayotolewa kwenye vyama vya ushirika ambao wananunua kwa bei ndogo
na wakati mwingine kwa mkopo.

Kufuatia usumbufu huo wanunuzi wanaondoka unakuta mtu unabaki na kahawa yako ukisubiria ikopwe tena kwa bei ndogo. Serikali ingeweka utaratibu mzuri,kila mtu atumie nguvu yake kihalali,na afaidi nguvu zake kama hao wanunuzi kutoka nje watatakiwa kulipa kodi kidogo,basi iwe hivyo ili mkulima apate soko na serikali ipate mapato yake.

Haiingii akilini ,kahawa iwe na bei nzuri uganda,na huku kwetu isiwe na bei kwani waganda wanauza wapi kahawa? au wao wana matumizi mengi ya kahawa kuliko sisi? Kama wana matumizi mengi basi ichukuliwe kuwa fursa mkulima anufaike.

Hapo sijazungumzia yule aliyekamatwa mkoani pwani na kiwanda cha kuchakata mawese akakamatwa na polisi kwamba ana kiwanda bubu,hadi aliponusuliwa na Zitto na waziri wa kilimo Bashe.

Kilimo kina fursa ya kuinua wengi tukiamua kutotumia sekta ya kilimo kama gereza la mateso.
 
Tatizo urasimu...

Wapo watanzania wengi tu wamewekeza nje na wanafanya vizuri

Ova
 
Back
Top Bottom