Tanzania kuijibu Marekani, Uingereza

Tanzania kuijibu Marekani, Uingereza

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema inalifanyia kazi tamko la pamoja la ubalozi wa Marekani na Uingereza linaloelezea wasiwasi wa kuzorota kwa haki za raia nchini.

Katika tamko hilo lililotoka leo Ijumaa Agosti 9, 2019 mabalozi hao wanaitaka Serikali kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kwa raia wake.

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Agustine Mahiga akizungumza na Mwananchi leo kuhusu tamko hilo amesema wameliona na wanalifanyia kazi.

Mwanadiplomasia huyo amesema wizara yake pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) watakutana kujadili tamko hilo na baada ya hapo Serikali itatoa msimamo.

“Baada ya kukaa kwa pamoja tutatoa taarifa ya Serikali kuhusu tamko hilo la pamoja,” amesema Balozi Mahiga aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Amesema anafahamu tamko hilo linatokana na tukio la hivi karibuni ambalo hakulitaja.
==========

My Take; Angalau Mahiga kajibu kidiplomasia angekuwa yule wangeambiwa Tanzania ni nchi huru wasituingilie.

Yule punguani anaetoa macho kama limjusi lililobanwa na mlango?

Jinga sana lile likizibo!
 
Hahahaha mamaa nimekubali kauli za Kagame kasema kweli.
Yani hawa wazungu hujifanya wanalinda haki za binadam ilhali hao ndio wa kwanza kuzivunja.
Wacha tu awachane ukweli inatakiwa ifike kipindi Waafrika tujitambue sisi ni kina nan na tunatakiwa tufanye nn tofauti na kuendeshwa na hawa majamaa.
Inatubid tuue superiority complex mama angu.
Kweli kabisa. Ndio maana Magufuli kuna baadhi ya watu hawamuelewi. Wanahisi wazungu Kila wanachofanya na hasa wanachotuelekeza ni formula na lazima tufuate. Magufuli kabadili mikataba ya accacia kwa kuwa wamekiri kuwa wanaiba na wameona msamaha. Wakati mwanzoni kuna mwanasheria mbobezi alitudanganya na kutisha watu kuwa tusijaribu kuzuia makinikia kwa kuwa tutafungwa na kuzuia wawekezaji nchini. Leo kimya anaona aibu huko aliko. Alituaminisha kuwa mikataba ikisainiwa ni mpaka mwisho, haivunjiki, sasa wanaona aibu.
 
Rais wa Rwanda alishawajibu vizuri sana hao jamaa kuhusu masuala ya haki za binadamu.
1. Kuwa Mwaafrika ndiye kinara wa haki hizo duniani.
2. Kuwa hao jamaa hawana moral authority ya kumfundisha Mwaafrika kuhusu haki hizo ambazo zinatawaliwa na mila na desturi.
3. Kuwa haki za binadamu za hao jamaa na ushoga, kutukana wakubwa zao na mambo mengine ambayo hayavumiliki kwa Mwaafrika. Mzungu anapaswa kujifunza kwetu katika masuala.ya haki za binadamu and not vice versa!
4. Kabendera kutumiwa na gazeti la Uingereza la Economist kuandika habari za kuleta machafuko kwa nchi yetu kwa malipo ya kampuni ya Uingereza ya Acasia, kamwe haliwezi kuvumiliwa na wala haliwezi kuwa kwenye haki za binadamu wa Kiafrika. Acasia wamekuwa wakimlipa Kabendera mabilioni ya pesa kwa shughuli hii baada ya kubanwa kwenye wizi wao wa makenikia. Lengo lao likiwa kuikomesha serikali ya Tanzania. Huu ni uhaini unaopaswa kuzimwa kabla haujaleta madhara. Hichi ndicho serikali ilichofanya kwa kumkamata Kabendera na kumfikisha mahakamani. Pesa hizo za kigeni alizokuwa akilipwa Kabendera hazikulipiwa kodi ya serikali - alikuwa akilipwa kinyemela kama wanavyolipwa wanaotumikia vikundi vya kigaidi hususani Al Akaida. Hii kama siyo money laundering ni nini?

Suala la Kabendera liko mahakamani na hakuna mwenye haki ya kuingilia suala ambalo liko mahakamani, including hao mabalozi wa Uingereza na Marekani. It is a contept of court. Waache sheria zetu zichukue mkondo wake.Wasitake kuifanyia Tanzania kama walivyozifanyia nchi kama Libya.
Hii nchi inatakiwa ifanywe kama Libya ndo tuheshimisne.
 
Haki za binadam ni Kabendera wengine nani sio binadam?
 
Kila siku kujibizana ni dalili za uoga, tuwafukuze nchini wakasemee huko kwao.
Sijui ccm wao wanaaemaje?!
Hivi inawezekana UAMSHO ikawa ni magaidi kweli, mbona uongereza na Marekani haziwatetei?!
 
Mkuu kuna uwajibishaji wa kiongozi akienda kinyume na katiba kulingana na UN treaties km alivyofanyiwa Uhuru Kenyatta.
Ila kusema ukweli hawa jamaa huingilia internal sovereignty za watu kuliko kuwajibisha viongozi wanapoenda kinyume.
Na kwann iwe Africa tuu???
Kuna mataifa yana violate human rights kindaki ndaki ikiwemo Myanmar ila husikii kiongozi wake akishurutishwa.
Kwann iwe Africa tuu ??!!
Tena akumbuke. Saudi Arabia hakuna vyama vingi hakuna demokrasia wanayotaka wazungu. Ushoga hauruhusiwi, uzinzi hauruhusiwi, ukikamatwa na makosa hayo ni kifo. Juzi tu ndo wameruhusu wanawake kupiga kura, kuendesha magari, lakini Hao ndo mabest wa marekani na ulaya. Usijidanganye kuwa wapo kwa ajili ya human rights. Watakuchukia tu endapo utakua free from their dependance na ukibana makampuni yao kuendelea kuiba. Obama alikiri hadharani kuwa walifanya makosa kuivamia Libya. Mpaka leo nchi ile haitawaliki. Kutoka nchi ya elimu bure mpaka kuwa nchi ya wakimbizi tena wakienda nchi hizo hizo wanazamishwa baharini.
 
Hapa watapiga kmya ... mzee jiwe si hataki kusikia ?? Wazr gan atanyanyuka na kukiri kisha kusimamia haki !!!? Wote watakaa kimya kulinda ugali wao
 
Tanzania Ni Pazuri Sana Nchi Ya Asali Na Maziwa
Kwasasa Mabeberu Hawana Nafasi
Yaani Tanzania Iko Salama Na Imara Kuliko Wakati Wowote Ule.
 
Mkuu namaanisha sana sana Africa labda nirekebishe kauli.
Mostly African countries bro.
Uko sahihi bado. Kwa ufupi nchi zote ambazo zitaathiri maslahi ya watu wa magharibi hasa maslahi ya kiuchumi, zitashughulikiwa. Ikiwemo venezuela ambayo best zao ni warusi ambao ni maadui wa marekani. Waafrika tunasahau haraka sana. Tunasahau kuwa mobutu seseseko alikuwa dikteta, muuaji na Kila aina ya ubaya alikuwa nao, lakini bado alikuwa kipenzi cha wazungu. Do you know why? Jibu ni simple tu, alikuwa akisaidia wazungu kuiibia Africa hasa Congo. Leo tumepata hasara kuwa na wasomi wasioamka kifikra wakisahau kuwa kutangulia sio kufika. Wazungu kututangulia haimaanishi wao watakuwa juu milele.
 
Sitarajii majibu yoyote ya maana bali kinyume chake.

Najua wataendelea kuharibu tu kupitia majibu yao.

na hayo majibu kwanza ni lazima hayapitishe kwa boss mkuu kabla hajaenda ya kutoa kihadhara. Na mantiki hii tusitegemee majibu ya maana kweli
 
Wewe huwa unaleta zipi, habari ni habari tu nzuri mbaya ni habari, za kupongeza za usaliti zote habari.
Kama ambavyo mke wako akichepuka mnayamaliza ndani kwa ndani, hivyo hivyo hata habari mbaya siwezi kuiandika na kuishabikia. Wewe kinara wa kushabikia mapungufu hasa ya Magufuli kiasi nina wasiwasi hata nkeo akikojoa kitandani Kwa bahati mbaya utautangazia ulikwengu. Jirekebishe
 
..wale hawakuuwawa na vyombo vya serekali.

..waliuawa na mwananchi wa kawaida aliyekuwa na silaha.

..na Wamarekani wanajadiliana kwa uwazi kuhusu masuala ya umiliki wa silaha usio na udhibiti.

..wako baadhi yao wanaamini unasababisha silaha ziangukie mikononi mwa wasiostahili.

..Na katika tukio lile vyombo vya serekali vilichukua hatua za haraka kurejesha usalama, na kumkamata mtuhumiwa.

..hapa kwetu wanaotuhumiwa kufanya ukatili ni vyombo vya serekali. Na kibaya zaidi serekali haionyeshi kukerwa na hali hiyo, na haichukui hatua.
Hapa nchini nani kauawa bila hatia na serikali. Mambosasa na liberatus wakiwa wanatoa taarifa za kuuawa majambazi ni kosa?
 
Akili zako kidogo kuna shida. Mwandishi anamuuliza maswali as mwandishi, PK yeye directly anaanza kumshambilia kwa maneno yasio ya kistaarabu.
Mwandishi ndo kaanza kutoongea kistaarabu kwa kusema Rwanda hakuna haki za binadamu. Angeuliza kistaarabu kuwa Hali ya haki za binadamu nchini kwako ikoje? Ukiishi kama mbwa, utakufa kama mbwa.
 
Back
Top Bottom