Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Mambo vp JamiiForums?

Ninashauri sana nchi yetu ya Tanzania isiwe na vazi moja tu la taifa. Tuwe na mavazi rasmi matano (5) kutoka katika makabila yetu yatakayorasimishwa na kupewa hadhi ya utaifa. Yaaani kama inawezekana mpangilio uwe hivi au hata kama kura ya maoni inaweza kupigwa itakuwa sawa tu.

Picha hapo chini ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne mzee Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwa wamependeza vizuri kabisa katika mavazi ya kabila ya Waha (baba) pamoja na Maasai (Mama)

images (3).jpg


(1) Kaskazini - Vazi la kimaasai (Mkoa Arusha)

(2) Kusini - Vazi la Kimakonde (Mkoa Mtwara)

(3) Mashariki - Vazi la Kisambaa (Mkoa Tanga)

(4) Magharibi - Vazi la Waha (Mkoa Kigoma)

(5) Kanda ya kati - Vazi la wagogo (Mkoa Dodoma)

Nchini Afrika ya kusini wamefanya hili kwa upande wa lugha rasmi za taifa, ila sisi tunaweza kufanya hivi hivi kwa upande wa vazi rasmi la taifa.

Kwa uhalisia tu ni kwamba, huko nchini Afrika ya Kusini kuna makabila mengi sana yaliyopo katika majimbo tofauti tofauti na matokeo yake lugha zinatawala katika majimbo yao husika ambayo inafanya kuwa lugha mahususi haswa kwa eneo/mkoa husika.

Takribani lugha thelathini na tano (35) zenye asili ya Afrika Kusini huzungumzwa katika nchi hiyo, kumi kati ya hizo ni lugha rasmi za taifa la Afrika Kusini: Ndebele, Pedi, Sotho, Swati, Tsonga, Tswana, Venda, Xhosa, Zulu na Afrikaans.

Lugha rasmi ya kumi na moja ni Kiingereza, ambayo ndiyo lugha ya msingi inayotumiwa katika mazungumzo ya kibunge na kiserikali, ingawa lugha zote rasmi zina uzito sawa katika hadhi ya kisheria na katika ya nchi hiyo.

Kama katika lugha 35 kutoka nchi nzima waliweza kuchagua lugha 11 tu kutambulika kama "official languages" na Tanzania yenye makabila takribani 120 pia inaweza kuchagua mavazi kutoka makabila 5 tu kuwa ndio mavazi rasmi ya taifa ili tumalizane na hili suala kwa maana tangia lianze kujadiliwa ni zaidi ya miaka 15 sasa na bado sijaona solution ya maana mpaka sasa.

Zamani ilikuwa ni Dar es Salaam kwa kabila la wazaramo ila sasa ni Dodoma kwa wagogo ndipo kumepewa hadhi ya makao makuu ya nchi na serikali. Kama mkoa wa Dodoma umeweza kupewa hadhi hiyo na kuacha mikoa mingine, kwanini makabila matano niliyoyaorodhesha hapo juu yasiwakilishe mavazi rasmi ya taifa?

Soma pia>>> Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu duniani isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Ni kama unafunga uhuru wa maoni. Na maoni yangu ni halina maana na haliwezi fanikiwa abadani maana vazi halitafutwi. Ni auto tu, ninyi mnadhan Nigeria walitaguta vazi lao, au Rwanda?
Sio lazima Tanzania ifanye kama Rwanda au Nigeria. Kwani Rwanda na Nigeria kuna makabila 120 kama kwetu? Acha kukariri maisha kijana wangu
 
Back
Top Bottom