Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi, kufuatilia comments za watu nikakuta link kwenda youtube kuona documentary kuhusu maisha ya uwanja wa fisi - inaitwa hyena square.
Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Inaumiza kuwa wengine tunaishi maisha ya kula na kusaza huku wenzetu wakipitia maisha kama ya dada Eliza aliyotajwa kwenye hiyo movie.
Kama haya yanatokea Tanzania na mimi sikuyajua, sijui ni mengi kiasi gani ambayo siyajui. Hapana, hii imepita kipimo, kama hii haivunji moyo basi sijui nini tena kitabadili mwelekeo. Siwezi sasa kuendelea kuishi maisha mazuri wakati wengine wakiishi jehanam kama haya. Kama haya yanatokea Tandale ambako ni KM chache tu toka magogoni, sijui yanayotokea Iringa ni makubwa kiasi gani.
Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.
Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.
Hebu one mwenyewe hii clip ya youtube..
[media]http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM[/media]
[media]http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc[/media]

http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM
http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc
Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.
Hivi hadi mtu uishi au uende Marekani ndo ujue kwamba sisi tuna maisha mabaya?
mzee hadi uishi kwenye usafi ndio utajua uchafu ulivyo mbaya... na kama mtu hajawahi kuona mwanga, atachukiaje giza...?
...usisahau kuwanyima kura sio maneno tuu.
Masaka kwani wee unaishi wapi hayo ya uwanja wa fisi usiyajue hadi leo hii, tena kwa kupitia blogs? Au ndio 'wazee wa inji' wamekupiga kata funua kuhusu malipo yako? Mi nilikua nakuangalia tu......Kitakachokusafisha hapa ni kuzikana threads zako zote za pumba ulizozimwaga hapa kama utitiri na kuweka posts mpya zenye mtazamo wa mzalendo halisi mwenye kuijua nchi yake na yale yanayojiri ndani yake. Kauli zako ndizo zitakazo kusafisha, am afraid- just saying 'sorry' wont be good enough.