Tanzania inayonifanya niwaombe msamaha wana JF

Masaka

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
437
1
Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi, kufuatilia comments za watu nikakuta link kwenda youtube kuona documentary kuhusu maisha ya uwanja wa fisi - inaitwa hyena square.

Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Inaumiza kuwa wengine tunaishi maisha ya kula na kusaza huku wenzetu wakipitia maisha kama ya dada Eliza aliyotajwa kwenye hiyo movie.

Kama haya yanatokea Tanzania na mimi sikuyajua, sijui ni mengi kiasi gani ambayo siyajui. Hapana, hii imepita kipimo, kama hii haivunji moyo basi sijui nini tena kitabadili mwelekeo. Siwezi sasa kuendelea kuishi maisha mazuri wakati wengine wakiishi jehanam kama haya. Kama haya yanatokea Tandale ambako ni KM chache tu toka magogoni, sijui yanayotokea Iringa ni makubwa kiasi gani.

Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.

Hebu one mwenyewe hii clip ya youtube..

http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM

[media]http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM[/media]

http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc
 
Hiyo clip ni kama dk 30, jipe muda wa kutosha kabla ya kuifungua. Kuna link mbili lakini zote zinaongelea kitu kimoja.
 
Masaka kwani wee unaishi wapi hayo ya uwanja wa fisi usiyajue hadi leo hii, tena kwa kupitia blogs? Au ndio 'wazee wa inji' wamekupiga kata funua kuhusu malipo yako? Mi nilikua nakuangalia tu......Kitakachokusafisha hapa ni kuzikana threads zako zote za pumba ulizozimwaga hapa kama utitiri na kuweka posts mpya zenye mtazamo wa mzalendo halisi mwenye kuijua nchi yake na yale yanayojiri ndani yake. Kauli zako ndizo zitakazo kusafisha, am afraid- just saying 'sorry' wont be good enough.
 
Masaka... sikujua unaguswa na matatizo ya Tanzania. Ulipojitokeza kutetea CCM miye nilikuwa nahesabu muda tu kabla "mwanga wa ukweli" haujakuzukia. Inasikitisha kuona CCM inapoteza mtetezi mzuri kama wewe. Nina uhakika watakumiss.

Ila nakuomba usikate tamaa, jaribu kutetea unayoweza kwani mchango wako ni muhimu sana na ulileta balance ya pekee humu. Chonde chonde usiache kukitetea chama chako.
 
Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi, kufuatilia comments za watu nikakuta link kwenda youtube kuona documentary kuhusu maisha ya uwanja wa fisi - inaitwa hyena square.

Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Inaumiza kuwa wengine tunaishi maisha ya kula na kusaza huku wenzetu wakipitia maisha kama ya dada Eliza aliyotajwa kwenye hiyo movie.

Kama haya yanatokea Tanzania na mimi sikuyajua, sijui ni mengi kiasi gani ambayo siyajui. Hapana, hii imepita kipimo, kama hii haivunji moyo basi sijui nini tena kitabadili mwelekeo. Siwezi sasa kuendelea kuishi maisha mazuri wakati wengine wakiishi jehanam kama haya. Kama haya yanatokea Tandale ambako ni KM chache tu toka magogoni, sijui yanayotokea Iringa ni makubwa kiasi gani.

Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.

Hebu one mwenyewe hii clip ya youtube..

[media]http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM[/media]

[media]http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc[/media]

Masaka umenivunja mbavu ile mbaya. Kwani wewe mwenzetu unaishi tanzania ipi???
 
For the scripture versed, this is a Saul- Paul seeing the light moment.

I trust you will sincerely learn the burning issues and carry the enlightened ideals presented by esteemed members of these fora.
 
Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi, kufuatilia comments za watu nikakuta link kwenda youtube kuona documentary kuhusu maisha ya uwanja wa fisi - inaitwa hyena square.

Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Inaumiza kuwa wengine tunaishi maisha ya kula na kusaza huku wenzetu wakipitia maisha kama ya dada Eliza aliyotajwa kwenye hiyo movie.

Kama haya yanatokea Tanzania na mimi sikuyajua, sijui ni mengi kiasi gani ambayo siyajui. Hapana, hii imepita kipimo, kama hii haivunji moyo basi sijui nini tena kitabadili mwelekeo. Siwezi sasa kuendelea kuishi maisha mazuri wakati wengine wakiishi jehanam kama haya. Kama haya yanatokea Tandale ambako ni KM chache tu toka magogoni, sijui yanayotokea Iringa ni makubwa kiasi gani.

Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.

Hebu one mwenyewe hii clip ya youtube..

http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM

http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc

Machozi yalikutoka wewe baada ya Kelly Rowland kutokwa na machozi?
Mbona wengine yalishatutoka sana tu na sasa tumeamua IWE MBAYA?
Watu tunakwenda BONGO tunaona hali za maisha ya watu machozi yanatutoka wewe unasubiri mpaka Yamtoke mmarekani ndio uamini?
 
Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Nashukuru kuwa umekubali makosa yako,kitu ambacho kinahitaji uajsiri sana,haswa kwa sisi watanzania.

Naamini kuwa Chama si tatizo, bali ni wale viongozi na vibweka vyao ndio wametumia chama kama mwanvuli wa kufanya uharamia wao.....hawa mimi nina waita ni majambazi ni maharamia ambao wameteka chama.

Kilichobaki, wewe ni kusaidia wanachama wenzako ambao bado ni wengi wasafi mkiokoe chama chenu.

BRAVO MASAKA.....hii ndio tunaita Utaifa kwanza and then Chama au Mke.
 
Unajua Tz sio maskini kama watu wa mataifa wanavyozani ila ni umaskini wa kujitakia na hasa unaosababishwa na mafisadi wachache ambao wamehodhi kila kitu cha nchi hii kiasi cha kutowatendea haki watz!

Sasa umeona ya Uwanja wa fisi ndo umeamini sasa ukionyeshwa yanayojiri uko vijijini watu wanafungwa kisa hawajatoa michango ya kujenga zahanati ya kijiji mbaya zaidi msimu wa kupanda na sio wa mavuno!

Now you have seen the right then stand up for the rights of the many Tanzanians ambao hawana wa kuwatetea!
 
...usisahau kuwanyima kura sio maneno tuu.

duh watu mmekua wakali!!!
well masaka hongera sana kwa kufunguka macho na sie twasema twashukuru mmoja amerudi kundini maana ulikua umepotea kijana!!!karibu sana
 
...Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia Kosa....welcome back againa masaka tumkome Nyani..
 
Usikate tamaa mapema namna hiyo.. Bado una nafasi kubwa ya kukikosoa chama chako ukiwa ndani ya chama hicho
 
Masaka kwani wee unaishi wapi hayo ya uwanja wa fisi usiyajue hadi leo hii, tena kwa kupitia blogs? Au ndio 'wazee wa inji' wamekupiga kata funua kuhusu malipo yako? Mi nilikua nakuangalia tu......Kitakachokusafisha hapa ni kuzikana threads zako zote za pumba ulizozimwaga hapa kama utitiri na kuweka posts mpya zenye mtazamo wa mzalendo halisi mwenye kuijua nchi yake na yale yanayojiri ndani yake. Kauli zako ndizo zitakazo kusafisha, am afraid- just saying 'sorry' wont be good enough.

Uwanja wa Fisi umebadilika kidogo, tofauti na miaka michache nyuma. Nilizunguka huko mwaka 2005, nimepita tena 2008. Mradi wa Benki ya Dunia umesaidia kidogo kubadili hali ya manzese. Lakini kinachosikitisha ni kuwa mabilioni mengi yametumika lakini mabadiliko yaliyofanyika hayalingani kabisa na fedha zilizotumika. Lakini mbaya kinachoumiza ni kuwa, mikakati yoyote ya kubadili miundo mbinu bila kubadili hali za maisha ya watu inasababisha a mere beautiful city of the beggars! Kinachotokea manzese ni kuwa sasa hawa wahanga wanasukumwa pembezoni na kuanzisha viwanja vingine vingi zaidi vya fisi maeneo mengine. Tembelea tandale, makurumla ndani ndani na vitongoji vingine utabaini matabaka tuliyonayo katika nchi yetu. Ndani ya Jimbo moja la Ubungo, mkazi wa Sinza na wale wa viwanja vya fisi ni kama mbingu na ardhi! Tanzania inahitaji ukombozi, kuwa na taifa lenye fursa kwa raia walio wengi. Pale uwanja wa fisi kuna wakina dada wenye vipaji vingi sana, laiti wangepata fursa

JJ
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom