Bunduki ( kura)zipigazo risasi moja ya uhakika tunazo nyingi sana zaidi ya milioni 20.
Fisadi ameanza kuingia hofu,
anazungukunga kila kona macho yamemtoka pima mekundu kama pilipili kichaa,
domo kalipanua kaa chewa na kulonga ovyo huku akijipinga mwenyewe.
Wananchi Bunduki zao wamekumbatia kwa makini wanasubiri muda mwafaka wa kumlipua Fisadi na kumtupilia mbali akashiriki karamu haramu na mabwana zake ughaibuni.
Kila dalili inaonyesha ushindi ni wetu.
Fisadi anajitahidi kuminya na kutawala majira ili wakati usikate mwendo na saa yake ikafika.
Kiburi na majivuno yake yamegeuka kuwa nyenzo madhubuti ya kuumaliza uhai wake ulo salia.
Kiti chake cha enzi kinatoa fukuto kali la uoza wake kama moto wa jua.
Nyayo zake laini zakanyaga mbili mwitu.
Kilio cha maumivu ya moto wa uoza na mbigili za kulewa madaraka ni kikali, chalindima kama radi za masika.
Apita akijificha sura na umbo lake majiani kuogopa kuzomewa na wananchi.
Atamani kujigeuza sura kuwa binadamu tena lakini mkia wamwumbua.
Kila mtu anajua wakati wake umekwisha na kiama chake ki kinywani mwake
kila alisemalo lampeleka mautini maana kuzimu yamlilia.
Kiubinafsi Bunduki zetu ni hafifu kwa umoja ni silaha madhubuti ya kumkatilia mbali Fisadi.
MADELA.
Nimekubali Mkuu, Tamathali za Semi ulizotumia katika thread hii zimekwenda shule, Nimefurahi jinsi ulivyotumia ufundi wa lugha hapo mzee , kwa hiyo kula Tano za haraka haraka!!
By the way, ili tuweze kuendelea tunahitaji, watu ,ardhi, siasa safi, uongozi bora, amani,mtaji, elimu na maarifa,
kwa hiyo kupigana vita na kuzing'oa serikali madarakani kwa kudhani hapo ndo tutaendelea mimi ninaona huo ni upotofu.
kwa sababu vita huondoa amani yenye kuhitajika , ambayo nayo ni msingi wa maendeleo.
kwa kuwa tunakubariana kwamba Tanzania tuna amani, kwa nini tusirekebishe misingi mingine ya maendeleo?
Mathalani kama hatuna uongozi bora kwa nini tusifanye namna ya kuubadili au kuurekebisha bila kuvunja amani? kwa sababu hatuwezi kuvunja msingi mmoja wa maendeleo kwa ajili ya kusimika mwingine.
au kama ardhi ni msingi wa maendeleo , je tumeitumiaje hiyo ardhi kwa ajili ya maendeleo? maswali yanaendelea na kuendelea
Principles huwa hazikubali kuvunjwa , huwa zinajiadjust kuhakikisha zinasimama, kumbuka ukivunja amani leo, amani itataka Isimame, matokeo yake atakuja mtawala mmoja dhalimu mwenye nguvu atakaye hakikisha amani inarejea ili awatawale vizuri, na hiyo itakuwa gharama kubwa ya damu, mali ,uhuru n.k
ndivyo principles zifanyavyo kazi.