Tanzania inataka vita ili ijulikane-kujitangaza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania inataka vita ili ijulikane-kujitangaza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hasara, Oct 17, 2007.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. H

  Hasara Senior Member

  #1
  Oct 17, 2007
  Joined: Dec 29, 2006
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MSINIELEWE VIBAYA KWA MANENO HAYA YA KUTAKA ''VITA''
  Tanzania inataka vita ili ijulikane-tuache kujitangaza nchi za nje kwa kutumia mamilion ya wavuja jasho huko CNN wakati somalia ,liberi,kongo, sudan,iraq,iran,afghastam. n.k zina pata matangazo ya bure kwa CNN, kwa sababu ya Amani na Utulivu inatumika kama kimvuli cha mafisadi, na kuomba omba kila siku na na safari za NJE kila siku, zarau, kiburi cha madaraka, kwani watatufanya nini?

  sasa watanzania wamechoka kauli za viongozi wetu, muda wakwenda chaka unakaribia,

  haya ni maoni yangu sijatumwa na mtu yeyote.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 17, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  ni maoni ya kipuuzi ambayo siyo tu ni ya hatari bali ambayo yanabidi kupingwa!! Hizo nchi ulizozitaja baada ya kujitangaza bure CNN zimepata manufaa gani zaidi.. kama ukijitangaza kwa vita ndio unapata Iraq, Afghanistan, Somalia, Kongo n.k miye nachagua amani!! Mafanikio hayaletwi na vita yanaletwa na amani!
   
 3. green29

  green29 JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Ni mawazo ya ajabu kutamani sauti ya mtutu na harufu ya damu zisizo na hatia kwa nia tu ya kujitangaza... itakuwa ni kujitangaza kwa maslahi ya nani kama si wauaji... haya ni mawazo ya kichawi..yashindwe na yalegee!! Vita tunayotakiwa kupigana ni ile ya kujisafisha nafsi na kuisafisha nchi ili tuondokane na ufisadi na wizi wa haki za msingi za watanzania. Na silaha ni kuelimisha watanzania ili wawe waangalifu wakati wa kuchagua Viongozi. Uchaguzi ni nafasi ya kipekee kuisafisha nchi; ni nafasi ya kuchagua njaa au shibe kwa kila mtanzania.

  Watanzania wanatakiwa kuacha kuchukulia uchaguzi kijuu juu... uchaguzi ni zaidi ya ngoma za mganda na flana za rangi mbali mbali.

  Umakini unatakiwa kuanzia kwenye uchaguzi wa vyama vyote hadi wa serikali. Hatupaswi kuangalia upande mmoja. Viongozi wa vyama vya upinzani wakiwa ni wasafi watakuwa na ujasiri kukoromea udhalimu wa chama tawala(haijalishi chama gani kitakuwa tawala 2010 kuendelea)
  Hii ndio vita tunayotakiwa kupigana.
   
 4. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2007
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hasara:
  Ni maneno ya ibilisi hayo. Mfukuzie mbali, hustahili hata kidogo kuwa 'agent' wa ujumbe mbovu kama huo.

  Tunazo njia nyingi tu, na tena nzuri sana za kuwashinda na kuwalegeza hawa mafisadi wetu.
   
 5. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2007
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Mmmmhhhhhhhhhhhhhhhh Kutangazwa kwa gharama ya Uhai wa Binaadamu!
   
 6. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2007
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Aisee tumezoea AMANI. Ushindwe na ulegee kwa nguvu za MOLA!
   
 7. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  hatuwezi kufika huko tho tumechoka,kuna hatua nyingi unaweza kuschukua na zisilete hasara,tafakari na cha kufanya hakikisha kura yako unampa kiongozi ambaye si Fisadi na mwenye nia njema ya kuongoza watanzania,mwenye moyo wa ushujaa wa kulinda na kutetea maslahi ya taifa,asiyewakumbatia wafanyabiashara sababu hata mwalimu alishwahi kuhoji ni lini tanzania imeacha kuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi?

  ni hayo tu,
  TANZANIA INATAKA MAENDELEO ILI IJULIKANE-KUJITANGAZA
   
 8. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  kumbe unajua hili ! mbona hedikopta ilivyopingwa mawe ntu nlikuwa nnafurahia na nkasema ndio kwanza mwanzo wa mapambano ( sio ya kifikra in that case ). jibu in short bana usiandike kama mnyika hadi anasahau anachoongea !
   
 9. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2007
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kweli kama lilivyo jina lake Hasara ni hasara sana kwa ndugu zake hawana ndugu ila mzimu. Watanzania hatuwezi kuhubiri masuala kama haya tafadhali haya yasipate nafasi kamwe. Wachache watakao soma colum hii hawatakubaliana na wewe, nadhani lengo lako ni kujulikana katika JF kwa kutoa mada kama hii. Majambazi tu yakitikisa mtaa wote tunalala roho juu sembuse vita ambayo itatumia kila aina ya vifaa vya kivita silaha kubwa na ndogo, wewe hujawahi kuziona. Tafadhali Hasara shetani wa hasara na akutoke na kama utaendeleza mada hii na ulegee na "upararaizi" kabisa
   
 10. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2007
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  I know kwamba in JF there is freedom of speech, however lazima mfahamu kwamba hiki ni chombo ambacho wasio penda maendeleo ya Tanzania wanakiangalia kwa karibu sana, sasa kama Mtaanzisha mada za kishenzi na kipumbavu ili kuvutia watu wachangie it will not make sense, na wote hapa tutaonekana kama wajinga au wendawazimu.

  Kujulikana sio point ya maendeleo, na decision ya JK kutuweka kwenye CCN sio decision ya watanzania wote, however we elected him to make decisions for us, some of the decisions will be good some will be bad. Zipo nchi nyingi zinazo julikana na hazijamwaga damu, its all about strategy son. Look at Fiji, small ireland with high GDP, have you ever see them on TV?

  So, please dont judge the whole country because of decion made by one Tanzania who happen to be president by luck.
   
 11. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  i co- sign you 10,000,000,000% !!

  Ndio mambo watu kuwa na mitazamo kama yako ! Keep it up MUFTI !
   
 12. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2007
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  M7, Zenawi na wengineo waliyatumia na wakafika walipo (swala kama wao ni bora kuliko sisi kila mtu ana fikra zake, mi sidhani kama wako bora kuliko sisi). lakini kwa Tanzania hatujafika huko, bado tuna njia mbadala ya kutumia kuleta mabadiliko bila kulipa ghrama kubwa ya uhai wa wale tunaowatetea.

  Lakini unafikiri huko Iraq, Afghanistan, Liberia hali ilianzaje? yanayofanyika kwetu ndo yalipelekea watu kuchukua maamuzi waliyoyachukua ambayo gharama zake ndo tunaziona. Unafikri waliberia au hao wengine walikuwa hawapendi AMANI? walikuwa wanapenda kuona raia wao wakifurika ugenini kama wakimbizi, wakipanga foleni WFP kuomba chakula?? HAPANA! Kwamba tutalinda amani katika mazingira tuliyo nayo nadhani tunapoteza mwelekeo, Amani hailindwi kwa "uzuri" na "porojo", kwani ingekuwa hivyo JK hizi sifa anazo! Na wengi tunaogopa kuyajadili haya kwa sababu tunaogopwa kusutwa na wenzetu lakini reality on the ground ni tofauti.

  Wote mnaoongelea hii AMANI naomba mzisute nafsi zenu muangalie kama unaweza kuwadanganya raia million 40 kwa hili neno moja tuu kila siku wakati wewe unateketeza hazina ya taifa. ni swali gumu na gharama ni kubwa, lakini if thats what it will take for our leaders to listen, hata kama sio kizazi chetu, kizazi kijacho kinaweza badilika kikawa hakina tena ule ukarimu tulio nao sisi (kama bado upo anyway).

  Kumbuka after ten to fifteen years from now wapiga kura wengi watakuwa hawamjui mtu anayeitwa Nyerere na what he stood for. Amabe wengi tunamassociate na hili neno AMANI...Guys lets think big and far! Viongozi wetu lazima wabadilike, hulka ya binadamu ni kwamba subira ni kitu adimu sana. We jiulize Mpalestine au Muiraq anayejilipua unafikiri anapenda kufa vile? ni kwamba anaona hana haja tena ya kuishi kwa hiyo anaona mara mia aondoke na watu wengine hamsini. MWOGOPE MTU ALIYEKATA TAMAA!

  vita ni mbaya na gharama zake ni kubwa lakini if thats the only option then what else? Our leaders must know we can take it no more. huwezi pata allowance ya laki tano kwa siku (bila kodi), UNATEMBELEA vx YA ML. 100, you leave in paradise, wakati mtanzania mwenzako hata kwa mwaka haipati hiyo hela, hana ukhakika wa aspirini nk na bado unaimba amani na utulivu! You must be kidding!
   
 13. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkuu MM hizi nchi hazijitangazi Bure hizi nchi zinajitangaza kwa gharama ya maisha ya raia wake na cha kusikitisha zaid ni kujitangaza kwa kumwaga damu ya kina mama na watoto na wasio kuwa na hatia. Huyu jamaa anataka vita ili iweje? kweli huku ni kufilisika kimawazo na kihoja. Vita ni kitu cha kupinga siku zote.:confused:
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Oct 17, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  We kada usinchulie dhambi.. hakuna hata mara moja ninaposhabikia matumizi ya nguvu kupata mafanikio ya kisiasa! na ukiangalia sikuchangia kabisa mada hiyo.. you should know me by now.
   
 15. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  sasa washika dau wako unadhani hawakukuwakilisha walipochangia mada na kuandika mambo ya fujo as always !

  naenda kulala mie !
   
 16. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Bunduki ( kura)zipigazo risasi moja ya uhakika tunazo nyingi sana zaidi ya milioni 20.

  Fisadi ameanza kuingia hofu,
  anazungukunga kila kona macho yamemtoka pima mekundu kama pilipili kichaa,
  domo kalipanua kaa chewa na kulonga ovyo huku akijipinga mwenyewe.

  Wananchi Bunduki zao wamekumbatia kwa makini wanasubiri muda mwafaka wa kumlipua Fisadi na kumtupilia mbali akashiriki karamu haramu na mabwana zake ughaibuni.

  Kila dalili inaonyesha ushindi ni wetu.
  Fisadi anajitahidi kuminya na kutawala majira ili wakati usikate mwendo na saa yake ikafika.
  Kiburi na majivuno yake yamegeuka kuwa nyenzo madhubuti ya kuumaliza uhai wake ulo salia.
  Kiti chake cha enzi kinatoa fukuto kali la uoza wake kama moto wa jua.
  Nyayo zake laini zakanyaga mbili mwitu.
  Kilio cha maumivu ya moto wa uoza na mbigili za kulewa madaraka ni kikali, chalindima kama radi za masika.

  Apita akijificha sura na umbo lake majiani kuogopa kuzomewa na wananchi.
  Atamani kujigeuza sura kuwa binadamu tena lakini mkia wamwumbua.


  Kila mtu anajua wakati wake umekwisha na kiama chake ki kinywani mwake
  kila alisemalo lampeleka mautini maana kuzimu yamlilia.

  Kiubinafsi Bunduki zetu ni hafifu kwa umoja ni silaha madhubuti ya kumkatilia mbali Fisadi.
   
 17. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2007
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,609
  Likes Received: 6,774
  Trophy Points: 280
  MADELA.

  Nimekubali Mkuu, Tamathali za Semi ulizotumia katika thread hii zimekwenda shule, Nimefurahi jinsi ulivyotumia ufundi wa lugha hapo mzee , kwa hiyo kula Tano za haraka haraka!!

  By the way, ili tuweze kuendelea tunahitaji, watu ,ardhi, siasa safi, uongozi bora, amani,mtaji, elimu na maarifa,

  kwa hiyo kupigana vita na kuzing'oa serikali madarakani kwa kudhani hapo ndo tutaendelea mimi ninaona huo ni upotofu.

  kwa sababu vita huondoa amani yenye kuhitajika , ambayo nayo ni msingi wa maendeleo.

  kwa kuwa tunakubariana kwamba Tanzania tuna amani, kwa nini tusirekebishe misingi mingine ya maendeleo?

  Mathalani kama hatuna uongozi bora kwa nini tusifanye namna ya kuubadili au kuurekebisha bila kuvunja amani? kwa sababu hatuwezi kuvunja msingi mmoja wa maendeleo kwa ajili ya kusimika mwingine.

  au kama ardhi ni msingi wa maendeleo , je tumeitumiaje hiyo ardhi kwa ajili ya maendeleo? maswali yanaendelea na kuendelea

  Principles huwa hazikubali kuvunjwa , huwa zinajiadjust kuhakikisha zinasimama, kumbuka ukivunja amani leo, amani itataka Isimame, matokeo yake atakuja mtawala mmoja dhalimu mwenye nguvu atakaye hakikisha amani inarejea ili awatawale vizuri, na hiyo itakuwa gharama kubwa ya damu, mali ,uhuru n.k
  ndivyo principles zifanyavyo kazi.
   
 18. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  wewe Hasara sasa nini kitafuatia baada ya kuonekana CNN/BBC/SKY? wakishauza habari zao watatafuta another hot spot wanaendelea kuingiza mamilioni. Huu ni upuuzi wa hali ya juu hayo mataifa yaliyojitangaza kwa damu za raia wasio na hatia yamefika wapi?
   
 19. J

  Judy Senior Member

  #19
  Oct 17, 2007
  Joined: Aug 13, 2007
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani msameheni bure, si unaona hajajitokeza kujibu tuhuma? Inaonekana kajutia alichosema, may be katumwa na wauza silaha a-introduce hiyo ishu wapate soko.Au ni ushabiki tu wa kuonekana kapost mada. mmh
   
 20. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #20
  Oct 17, 2007
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Samahani, I have to close this topic. Anzisheni mada zenye mguso kwa jamii pls, soma alama za nyakati!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...