Makaimati
JF-Expert Member
- Apr 4, 2011
- 462
- 87
acheni kutumia tumbo katika kufikiri, Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni zalio la Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. na zilipoungana nchi hizi mbili zilikuwa huru na kama nchi hatuangalii idadi ya watu katika kuungana
na katiba ya mwanzo ya mwaka 77 pia iliundwa kwa idadi sawa ambayo kamati yake iliongozwa na Marehemu Thabit Kombo(kama sijakosoa kuhusu Mwenyekiti au katibu) mbona huko hakujapigiwa kelele iweje leo kurejea tu mfumo ambao tumetumia iwe z
mnataka kusema kwa vile Tanganyika kubwa mara nyingi kuliko Rwanda au Burundi, kwenye EAC watanganyika wapewe wajumbe zaidi au wataporeview katiba ya EAC watanganyika wawe na wawakilishi wengi kwa kuwa wao wana eneo kubwa na wana watu wengi?
jamani tuacheni kupenda dhuluma na kufikiri zanzibar ni kama Mbagala ati kwa kuwa wana eneo dogo na watu kidogo (maana watu ingekuwa ni hoja UN wangewapa CHINA viti zaidi ya kimoja)
Ahsante Mtu wa Pwani kwa kutujibia wengi
Hawa ndugu zetu wanatumia jazba zaidi katika kujadili kuliko busara.
Majibu yako ni murua kabisa.
Kwani ukubwa wa pua ndio wingi wa makamasi?
Zanzibar iliungana na Tanganyika kama Nchi huru kama Tanganyika.
Ni lazima hawa jamaa waelewe kuwa Tanzania haiwezi kuwepo bila ya Zanzibar lakini Zanzibar itakuwepo bila ya Tanzania.