Tanzania ina watu milioni 43, Zanzibar hawazidi milioni 5 kwa nini tugawane kwa kulingana?

Mkuu.
Huko kwa wachaga kuna hoteli imechukuliwa na serikali na kupewa mgeni au vipi?
Au aliyenyang'anywa sio Mchaga.?..still waiting to hear wana-msniper huyo mwekezaji mpya.
Halafu kuna mahoteli mingi tu Arusha ya wageni au?
Au tatizo ikiwa mgeni wenyewe ni mzenj?

Nani anachukua dhahabu zetu?
Nani anafaidi gesi yetu?
Wazenj unaowasema ni sawa na Mtanganyika yeyote yule, wanachumia tumbo tu. Wanaofaidi hutaki kuwataja au hujawagundua bado?

Kumradhi,Nilisahau mkuu ,kuwa bado...unapiga usingizi!
Kwanza Arusha sio Moshi, Arusha ilishauzwa zamani na kina Ally Hassan Mwinyi na Lowassa wasio na uchungu na nchi. Na hiyo hoteli aliyonyang'anywa Mchaga sidhani kama alipewa Mpemba, wangeshamfanya mbaya.

Dhahabu na gesi zinazokwapuliwa ziko uchagani? Mpemba "anaechumia tumbo" hawezi kutia mguu Moshi, Mchaga hataki ujinga. Labda uwe na mtaji mkuuubwa wa kuchimba madini ndio umshinde mangi na maduka yake, lakini sio kiduka ukaanzishe Moshi na Upemba wako. Mchaga atakuperemba. Mi si Mchaga lakini niliposikia hakuna Mpemba Moshi niliwapigia saluti wachaga.

Watanganyika wengine nao tunaanza kuamka, tutakuja kuwatimulia mbali, mkipona kwenye hii Katiba mpya sijui.
 
Kumbe hii katiba mpya inayotakiwa kwa nguvu zote ni kwa ajili ya kuwaKOMOA wazanzibar!!
 
Mimi akili yangu mbaya,kuondoa hayo matatizo zanzibar ningeifanya jimbo moja la tanganyika basi
 
Humu inawezekana kuna watu wanaandika comment zao wakiwa Bar, hivi wewe unafahamu maana ya ndugu wa damu? mke wako mwenyewe kama haujazaa nae hawezi kuwa ndugu wa damu, sasa undugu huo wa damu na hawa wapemba unatoka wapi? au wewe ni mwarabu wa ilala?
Mkuu.
Salmin Amour, alioa Mchaga wamezaa.....kuna Fatma said Ali ameolewa na mtanganyika mwenzetu...hao ni katika viongozi, pia kuna Zakia Megji......

Hafu kuna watu wengi tu wa makabila tofauti ya Tanganyika wameoa na kuolewa na Wazenj....mkuu kama huu uhusiano wewe huna haiwezi kuhalalisha kusema watu wa Tanganyika na Zanzibar hawana udugu wa damu,tena ulianza kwa miaka mingi, kabla ya Muungano.
kama una chuki binafsi nao ni kitu chengine. Chuki ni katika psychological disease! kapate tiba mkuu.

mimi si mwalabu wa ilala ni "mdanganyika" safi tu!
 
Ntemi Kazwile,

..nakubaliana na madai yako.

..mimi mapendekezo yako ni muungano wetu uvunjwe na tukashirikiane kupitia EAC.

..muungano wa serikali 3 hautabadilisha chochote, zaidi ya kuwapa wa-Tanganyika semi-autonomy status kama ile waliyonayo wa-Zenj kupitia SMZ. zaidi muungano wa serikali 3 utaongeza gharama za matumizi ya serikali kwa Tanganyika.

..kinachonisikitisha sasa hivi ni UWOGA wa wanasiasa wa Tanganyika kuzungumzia hatua za kuuvunja muungano huu usio na faida yoyote ile kwetu.
 
Kwanza Arusha sio Moshi, Arusha ilishauzwa zamani na kina Ally Hassan Mwinyi na Lowassa wasio na uchungu na nchi. Na hiyo hoteli aliyonyang'anywa Mchaga sidhani kama alipewa Mpemba, wangeshamfanya mbaya.

Dhahabu na gesi zinazokwapuliwa ziko uchagani? Mpemba "anaechumia tumbo" hawezi kutia mguu Moshi, Mchaga hataki ujinga. Labda uwe na mtaji mkuuubwa wa kuchimba madini ndio umshinde mangi na maduka yake, lakini sio kiduka ukaanzishe Moshi na Upemba wako. Mchaga atakuperemba. Mi si Mchaga lakini niliposikia hakuna Mpemba Moshi niliwapigia saluti wachaga.

Watanganyika wengine nao tunaanza kuamka, tutakuja kuwatimulia mbali, mkipona kwenye hii Katiba mpya sijui.

Mkuu,
Lowassa sio katika wachaga?
Mkipona....mkuu kwa sababu natatofautiana na wewe kimtazamo kwa hiyo na mimi nimekuwa katika wao?
That is Bush doctrine...either you are with them or you are with us!
It does not work that way, sir.

You hate what needs to be loved and you love what needs to be rejected!
kama umeridhika kugawiwa umasikini sawa!
 
Ntemi Kazwile,

..muungano wa serikali 3 hautabadilisha chochote, zaidi ya kuwapa wa-Tanganyika semi-autonomy status kama ile waliyonayo wa-Zenj kupitia SMZ. zaidi muungano wa serikali 3 utaongeza gharama za matumizi ya serikali kwa Tanganyika.

..kinachonisikitisha sasa hivi ni UWOGA wa wanasiasa wa Tanganyika kuzungumzia hatua za kuuvunja muungano huu usio na faida yoyote ile kwetu.

JokaKuu.
Unataka kusema kuwa muundo huu uliopo ulikuwa unajaribu kubana matumizi kwa iliyokuwa serikali ya Tanganyika?...anyway si lazima kujibu hili. nakusalimia tu,mkuu.

Huu "uwoga" hauko kwa viongozi tu...uko kwa kila anayejiita" mbara" au "mtanzania bara"....hatuko wengi tunaojiita watanganyika.
Pia hata tunaojiita watanganyika hatuutizami muungano huu kama third party...huwa tunaongozwa na ushabiki na hivyo kutaka kutupia lawama wazenj. We messed up and we should take that responsibility to correct the wrong.

Nani mwenye akili timamu haoni kuwa this "Muungano" is flawed!
It is just a big mess!
 
watanganyika wamejisahau wenyewe, maana wao ndio mainjinia wa muungano, na wao wenyewe kwa ujanja wao wakajisahau kistrategic kwa hio sio kweli wamejisahau, ila walitaka wafanye hivyo mtakavyo nyny muwe wengi kwa madai mna vipao mbele vingi na sisi tukubali kisha mtugeuze wageni kwenye nyumba tulioijenga kwa pamoja.

suluhisho ni serikali tatu, wazanzibar kama walivyofanya na serikali yao wamekaa na kupitia katiba yao na vipaumbele vyao peke yao na kwa muundo huo wamepata picha ya kujua kwenye katiba ya muuungano lipi na lipi libakie kwenye katiba ya muungano na lipi lirudi kwao, kama watanganyika wangekuwa ni watu wa haki wangekuwa na tanganyika yao, wakakaaa peke yao wakaangalia vipao mbele vyao na wakajua tunaenda kwenye katiba ya muungano ni lipi la muhimu kubakia kwenye katiba ya Jamhuri na lipi Libaki tanganyika

ila suluhisho waTanganyika ni wajanja na ujanja mwingi mwisho kiza

we kwani kuwa mtu wa pwani ndo unadhani unaruhusiwa kutumia matusi hapa ambako watu wanajenga hoja kwa maslahi yao binafsi? Watu wa zbar wameukataa muungano kwa kauli hata ktk website yao ya mzalendo.com,pia hapa watanganyika wameupinga kwa kauli mbali mbali hata hapa Jf,je we kwa nini usijenge kauli kuliko matusi? Mtu akikataa Uhuni huu,anakuwa na sababu yake hata iyo ya mlinganyo wa maeneo uko sahihi,ila towards the end we converge at the point kuwa muungano hautufai. Iweje utukane watu wazima ndugu?kumbuka wanaojadili muungano ni watu wazima,hapa hamna mtoto wa kutukanwa kuwa hatumii akili bali tumbo,ni ujinga na upumbavu. Hapa jamvini naona ID ninazoziona za PhD na masters'holders wanajadili,au raha yako tutoke humu,watoke wengine ili mubaki nyie mnaoandika jf kwa njozi kuliko milango ya fahamu? Ni hatari kuwa na wana matusi jamvini. Acheni watu wajadili wawezavyo na kuhitimisha,kama wamekuzidi hoja,kaa pembeni usikilize wachangiaji. Jirekebishe ndugu.
 
Ntemi Kazwile,

..nakubaliana na madai yako.

..mimi mapendekezo yako ni muungano wetu uvunjwe na tukashirikiane kupitia EAC.

..muungano wa serikali 3 hautabadilisha chochote, zaidi ya kuwapa wa-Tanganyika semi-autonomy status kama ile waliyonayo wa-Zenj kupitia SMZ. zaidi muungano wa serikali 3 utaongeza gharama za matumizi ya serikali kwa Tanganyika.

..kinachonisikitisha sasa hivi ni UWOGA wa wanasiasa wa Tanganyika kuzungumzia hatua za kuuvunja muungano huu usio na faida yoyote ile kwetu.

mkuu imeshawekwa wazi kuwa atayejaribu kuvunja muungano atachezea kamba/ktanz. Bora wajanja wapropose serikali3,hapa tnganyika watajitawala,zen Zenj,alafu wakutane kwenye govt.kuu ambayo automatically itakuwa haina power na kuwa week,towards the end serikali kuu itadisolve pole pole na kuiacha serikali ya Tnganyka na ile ya zbar. Watu wako so strategic usione wanadai serikali3 ukaona wanaigiza. Watawala wetu kwa kuwa ni wababe tutatumia akili wenyewe watumie nguvu mwishowe watasign for their destruction,upo apo mkuu?
 
Mimi mzawa wa TANGANYIKA na naipenda Tanganyika na c wa kuja.

Tuko pamoja mkuu.
Kama wewe ni mwenyeji wa mwambao usingotoa kauli kama uliyotoa.
Watu wa mwambao ni mchanganyiko.

Nimependa unataja tanganyika...mpaka kieleweke....au wewe ni "mtanzania bara"? au "mbara"?
Take it easy, bro....ni kiburudisho tu.
 
Mimi akili yangu mbaya,kuondoa hayo matatizo zanzibar ningeifanya jimbo moja la tanganyika basi

Kwa mamlaka yepi uliyonayo?
Ungetumia sheria ipi? Au ungetumia nguvu, ubabe na udikteta?

Mimi nilifikiri Muungano unafanywa kwa majadiliano.... kumbe ni jungle rules!
 
Nonda said:
JokaKuu.
Unataka kusema kuwa muundo huu uliopo ulikuwa unajaribu kubana matumizi kwa iliyokuwa serikali ya Tanganyika?...anyway si lazima kujibu hili. nakusalimia tu,mkuu.

Huu "uwoga" hauko kwa viongozi tu...uko kwa kila anayejiita" mbara" au "mtanzania bara"....hatuko wengi tunaojiita watanganyika.
Pia hata tunaojiita watanganyika hatuutizami muungano huu kama third party...huwa tunaongozwa na ushabiki na hivyo kutaka kutupia lawama wazenj. We messed up and we should take that responsibility to correct the wrong.

Nani mwenye akili timamu haoni kuwa this "Muungano" is flawed!
It is just a big mess!

Nonda,

..I dont have anything that indicates kwamba muungano wa serikali 2 ulilenga ktk kubana matumizi.

..ni mtizamo wangu tu kwamba, kuongeza serikali nyingine, juu ya hizi mbili zilizopo, kutaongeza matumizi, haswa kwa upande wa Tanganyika.

..pia Zanzibar inahitaji madaraka zaidi ya kujiamulia mambo yake, sasa sidhani kama mfumo wa serikali 3 utajibu kilio hicho cha wa-Zanzibari. nadhani wanaopendekeza serikali 3 hawajayatafakari kwa kina madai ya wa-Zanzibari.

NB:

..nadhani hata wanasiasa wa Zenj nao ni waoga kutamka kwamba muungano uvunjwe.

..CUF, chama cha Maalim Seif, sasa hivi wamependekeza serikali 3, na Zanzibar na Tanganyika ziongozwe na magavana.

..wanasiasa wa Zenj walikuwa na nafasi ya kuitisha kura ya maoni kuhusu muungano hawakufanya hivyo.

..kuhusu Zanzibar kujitawala kiuchumi, Maalim Seif aliulizwa kama anapendekeza Zanzibar iwe na sarafu na benki kuu yake akakanusha.
 
Mkuu.
Salmin Amour, alioa Mchaga wamezaa.....kuna Fatma said Ali ameolewa na mtanganyika mwenzetu...hao ni katika viongozi, pia kuna Zakia Megji......

Hafu kuna watu wengi tu wa makabila tofauti ya Tanganyika wameoa na kuolewa na Wazenj....mkuu kama huu uhusiano wewe huna haiwezi kuhalalisha kusema watu wa Tanganyika na Zanzibar hawana udugu wa damu,tena ulianza kwa miaka mingi, kabla ya Muungano.
kama una chuki binafsi nao ni kitu chengine. Chuki ni katika psychological disease! kapate tiba mkuu.

mimi si mwalabu wa ilala ni "mdanganyika" safi tu!

Nadhani wakati mwingine kusafiri nchi mbali mbali ni elimu tosha kabisa, kama kung'ang'ania muungano basi wangeanza wenzetu wa nchi hizi Botswana, Namibia, Swaziland, Lesotho, na South Africa. hawa ni jamii moja na makabira yao yapo kwenye hizo nchi zote, jambo hambalo huna uelewa nalo ni busara ukakaa kimya. Hatuhitaji muungano wa kisanii Period.
 
Kumbe hii katiba mpya inayotakiwa kwa nguvu zote ni kwa ajili ya kuwaKOMOA wazanzibar!!
Anhaaaa, kumbe mnaogopa niliposema Katiba mpya itawatimua, kumbe huko ni kuwakomoa eenh? Anhaa, mnaweweseka sasa eh?

Acheni kutingisha kiberiti, mnajua fika kwamba mnafaidika mno na Muungano lakini hamwishi kutokuwa na shukrani,
tutawatimulia baharini mkileta ngebe.
 
Muungano wetu unatakiwa tu ufanyiwe marekebisho, mimi sidhani kama idadi ya watu ni kigezo hapa tunaona kuna nchi mbili zimeungana Tanganyika na Zanzibar, mfano Italy wangefata idada ya watu nadhani Vatican City ingekuwa kitongoji sio nchi (Italy ina watu 61,016,804) na (Vatican City ina watu 832) na zote ni nchi
 
Si vema kuwaambia wachangia hoja kuwa wanatumia "tumbo kufikiri", hayo ni matusi kabisa na sidhani kama ni utu na inaonyesha wewe hujalelewa na values nzuri...sidhani kama kujibu hoja mpaka utukane, kwani ukitumia lugha proper hutasikilizwa? The fact that you start with insults doesn't show you use your head...and you are shaming yourself. Plus this issue is a very critical issue, huwezi kulinganisha na UN wala EAC...We are talking about justice within the union...in the use of our resources. Equitable distribution of governance and resources. How can you ignore such carnal issues? My friend, next time be civil...

Mpishe mpumbavu usije ukafanana naye, labda kwao hatumia zaidi tumbo!
 
Mkuu.
Salmin Amour, alioa Mchaga wamezaa.....kuna Fatma said Ali ameolewa na mtanganyika mwenzetu...hao ni katika viongozi, pia kuna Zakia Megji......

Hafu kuna watu wengi tu wa makabila tofauti ya Tanganyika wameoa na kuolewa na Wazenj....mkuu kama huu uhusiano wewe huna haiwezi kuhalalisha kusema watu wa Tanganyika na Zanzibar hawana udugu wa damu,tena ulianza kwa miaka mingi, kabla ya Muungano.
kama una chuki binafsi nao ni kitu chengine. Chuki ni katika psychological disease! kapate tiba mkuu.

mimi si mwalabu wa ilala ni "mdanganyika" safi tu!

Hapa Nonda umechemka, yaani tudumishe muungano tusioujua kisa mapezi ya wanasiasa?, kama wamaoana wao si wao. Hizi ndio faida wanazozidai za muungano?.

Muungano lazima uwe wa kimaslahi, sio maslahi ya wanasiasa.
 
Kwa mbali tunaweza kuulinganisha huu muungano wetu na ule wa Uingereza ambao jina kamili lingetakiwa liwe The United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland lakini inafupishwa na kuwa United Kingdom (UK).

Northern Ireland ina semi-autonomy kama ilivyo Zanzibar na baraza lake la uwakilishi kwa mambo yao. Pia kama Zanzibar Northern Ireland haina Sovereignty na ina uwakilishi kwenye bunge la United Kingdom.

Kama Zanzibar, Northern Island ni sehemu ya kisiwa na ina watu karibu milioni moja na nusu ambao ni asilimia 2.5% ya wakazi wa UK. Lakini huo ndio mwisho wa similarities na Jamhuri Muungano wa Tanganyika na Zanzibar au Tanzania.

Tofauti na Zanzibar, Northern Ireland ina wawakilishi 16 tu kwenye bunge la Uingereza lenye wabunge zaidi ya 600. Hii ni sawa na asilimia 2.5% tu kulingana na idadi yao ya watu.

Zanzibar yenye watu chini ya milioni moja ina wabunge 75 katika wabunge 357 wa Muungano ! Hii ni sawa na asilimia 17.5% huku watu wake wakiwa asilimia 2.5% tu ya Watanzania !

Kwa idadi ya wabunge 357, Zanzaibar ilitakiwa iwakilishwe na wabunge chini ya 10 period. Lakini kama ni usawa wa nchi unaliliwa basi tungegawana nusu kwa nusu kila upande ukiwa na wabunge 178 na nusu !

Tukimaliza hapo tunatakiwa Mawaziri tugawane sawa, wakuu wa mikoa tugawane sawa, wakuu wa wilaya tugawane sawa n.k. Mbona hapo Wazanzibar kila moja atakuwa afisa kuanzia vichanga, vikongwe hadi vichaa !

Mfano mwingine ni Marekani ambao wana United States of Amerika (USA) na ingawa kila jimbo lina mtawala anayechaguliwa na bunge lake, kwenye utaifa uwakilishi hutegemea wingi wa watu.

California (wawakilishi 55) kamwe haiwezi kuwa sawa na Alaska (wawakilishi 3) ! Tanzania hakika tukitaka kuendelea kuna mambo lazima tuache kuyafumbia macho. Yawezekana kulikuwa na umuhimu kwa wakati huo 1964 lakini siyo sasa.

Ni katiba mpya tu itakayotukwamua na kutuweka huru,
Mungu ibariki Tanzania.

Back
Top Bottom