Tanzania ina watu milioni 43, Zanzibar hawazidi milioni 5 kwa nini tugawane kwa kulingana?

acheni kutumia tumbo katika kufikiri, Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni zalio la Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. na zilipoungana nchi hizi mbili zilikuwa huru na kama nchi hatuangalii idadi ya watu katika kuungana

na katiba ya mwanzo ya mwaka 77 pia iliundwa kwa idadi sawa ambayo kamati yake iliongozwa na Marehemu Thabit Kombo(kama sijakosoa kuhusu Mwenyekiti au katibu) mbona huko hakujapigiwa kelele iweje leo kurejea tu mfumo ambao tumetumia iwe z
mnataka kusema kwa vile Tanganyika kubwa mara nyingi kuliko Rwanda au Burundi, kwenye EAC watanganyika wapewe wajumbe zaidi au wataporeview katiba ya EAC watanganyika wawe na wawakilishi wengi kwa kuwa wao wana eneo kubwa na wana watu wengi?

jamani tuacheni kupenda dhuluma na kufikiri zanzibar ni kama Mbagala ati kwa kuwa wana eneo dogo na watu kidogo (maana watu ingekuwa ni hoja UN wangewapa CHINA viti zaidi ya kimoja)

Ahsante Mtu wa Pwani kwa kutujibia wengi

Hawa ndugu zetu wanatumia jazba zaidi katika kujadili kuliko busara.

Majibu yako ni murua kabisa.

Kwani ukubwa wa pua ndio wingi wa makamasi?

Zanzibar iliungana na Tanganyika kama Nchi huru kama Tanganyika.

Ni lazima hawa jamaa waelewe kuwa Tanzania haiwezi kuwepo bila ya Zanzibar lakini Zanzibar itakuwepo bila ya Tanzania.
 
Ahsante Mtu wa Pwani kwa kutujibia wengi

Hawa ndugu zetu wanatumia jazba zaidi katika kujadili kuliko busara.

Majibu yako ni murua kabisa.

Kwani ukubwa wa pua ndio wingi wa makamasi?

Zanzibar iliungana na Tanganyika kama Nchi huru kama Tanganyika.

Ni lazima hawa jamaa waelewe kuwa Tanzania haiwezi kuwepo bila ya Zanzibar lakini Zanzibar itakuwepo bila ya Tanzania

Makaimati
Life Goes On
 
Nadhani wakati mwingine kusafiri nchi mbali mbali ni elimu tosha kabisa, kama kung'ang'ania muungano basi wangeanza wenzetu wa nchi hizi Botswana, Namibia, Swaziland, Lesotho, na South Africa. hawa ni jamii moja na makabira yao yapo kwenye hizo nchi zote, jambo hambalo huna uelewa nalo ni busara ukakaa kimya. Hatuhitaji muungano wa kisanii Period.

Bora umpe mifano rahisi ataelewa, maana huyu nonda-mpemba anaejifanya mtanganyika huwa simuelewi ktk post zake, naona kama mpayukaji anayeongozwa na hisia akidhani hapa ni mzalendo.com-Jukwa la kashfa na matusi dhidi ya watanganyika.
 
Hapa unaongelea nchi tofauti tofauti (sovereign states) lakini baada ya huo Muungano nchi mbili zilikufa ila kakaundwa kainchi ambako siyo sovereign state (Zanzibar) na kukawa na Sovereignty state yaani Tanzania. Ndio maana hakuna Tanganyika, sasa idadi sawa inatoka wapi wakati tuna Tanzania ambayo ni yetu sote? Huu muungano utata mtupu na chokochoko zinaanzia hapo hapo kwenye idadi sawa!! KWA ZANZIBAR CHAO CHAO CHETU CHAO, alaaa, nani akubali?

La kuzingatia ni kuwa Tanganyika na Zanzibar mbele ya sheria au katiba ni wabia au wadau wenye haki sawa ktk Muungano huu bila kujali ukubwa wa eneo au wingi wa watu.

Pia Muungano huu wa kihistoria hauwezi kufa maana hata watu wa Malindi, Lamu, Mombasa wanajihesabu ni 'Watanzania' kutokana na kuwa pwani yote ya Afrika ya Mashariki ilikuwa chini ya utawala wa Sultani wa Zanzibar.

Kithibitisho ni kuwa Kiswahili cha pwani ya Kenya ni cha 'Ki-tanzania' na tusishangae 'call centre' za makampuni makubwa Kenya kinatambua muungano huu au mwingiliano huu kiasi ya kuwa tukiwa Tanzania maswali yetu kwa makampuni hayo hujibiwa na 'call-centre' zilizoajiri watu toka Pwani ya Kenya.

Ukienda Lamu, wakaazi wake hutaniwa si 'Wakenya' bali ni 'Watanzania'kutokana na tabia zao/misemo yao/hulka zao, hivyo hata kifanywe nini Muungano huu wa Tanganyika, Zanzibar na Pwani Ya Kenya hauwezi kufa mioyoni au midomoni mwa watu hawa wenye historia ndefu ya maingiliano ya karne na karne.

Udumu Muungano wa Kweli.

Hiyo Tanganyika unayoitaja iko wapi?
 
Suluhisho ni kuwa na serikali tatu,au moja
Tukiamua serikali moja itakuwa option nzuri na rahisi lakini ngumu kukubalika hasa kwa wazanzibari
Serikali tatu ni rahisi kukubalika kwa pande zote lakini itakuwa na sura ya kurudi nyuma au kupunguzia uzito muungano,hapo tungehitaji kuwa na serikali ya Tanganyika,Serikali ya Zanzibar na Serikali ya muungano ambayo inaweza kuwa ndogo tu kupunguza gharama za uendeshaji
Kwa hali ilipo sasa hivi sioni sababu ya kuwa na wawakilishi idadi sawa toka kwa watu ml 40 na watu ml 1.5
 
Wazenji wanatukana Muungano lakini wamejaa madukani Kariakoo, Ilala, Namanga. Nasikia Moshi hukuti Mpemba hata siku moja, Mchaga ain't taking no bullshit kuangalia mgeni anakuja ana take over economic base yako we uko pale pale, aking'ang'ania wanaweza kum sniper.

Tulikosea kuungana na haka ka kisiwa katika model ile ya Nyerere. Katiba mpya nategemea ivunjilie mbali hili li Muungano la kuibeba beba Zanzibar.

Labda wapemba, lakini Moshi najuwa wadosi, waarabu, wazungu kibaaaaaao. Wanafanya biashara.
 
Siku zote humu JF huwa nawaambia, na huo ndio ukweli, kuwa Zanzibar ndio wameimeza Tanganyika. Nyie mnaojidai kulalama humu, nchi yenu inayuoitwa Tanganyika iko wapi? Rais wake nani? Bendera yake ipi, Mwimbo wa Taifa upi? Bunge lenu lipi? Zanzibar wanavyo vyote hivyo, sasa nani alieolewa. Mie najuwa ukiolewa na jina unabadili (kwa wenzetu mnaofata uzungu) Sasa nai aliebadili jina?
 
Mkuu, unawalinganisha na milioni tano wakati idadi ya mwaka jana walikuwa 1,068,823? na sasa watakuwa wamepungua sana manake kila kukicha wavuvi wanazama baharini na kufa. Linaloniuma ni kwanini inaongelewa Zenji na tanzania na Tanganyika hakuna? Zenji wana bendera yao na ile bendera yatu ya tanzanyika iliishia wapi? Iko siku tutaachana na umwinyi. SIUTAMBUI MUUNGANO WA WAARABU NA WATANGANYIKA ninazifahamu nchi mbili Tanganyika na Zanzibar na si Tanzania. Kazi tulonayo ni kurudisha heshina ya nchi yetu ya Tanganyika!
 
Muungano tulio nao sasa hivi siyo sawa. Muungano utakuwa sawa tu tutakapokuwa na serikali tatu (3). Ambapo yarikali ya Tanganyika itahusika na Tanganyika na Serikali ya Zanzibar itawahusu wazanzibari. Halafu tuwe na serikali ya Jamhuri itakayo jihusisha na mambo yote yatakayohusu muungano kama itakavyo kubaliwa. Haiwezerkani wewe ukawa waziri wa Jamhuri ya Muungano halafu eti wizara yako haihusishi mambo ya muungano eti kuna waziri mwingine zanzibar mwenye majukumu kama yako. Kwa nini usiitwe waziri wa serikali ya Tanganyika.
 
Kama ishu ni idadi ya watu na sio utaifa basi china ilibidi iwe na viti kama 20 hivi ktk UN. Endeleeni kupiga pombe halafu muje muchangie ktk makongamano ambayo watu muhimu ka shivji nao wapo muone watakavyo waadhirisha.
 
Hapa unaongelea nchi tofauti tofauti (sovereign states) lakini baada ya huo Muungano nchi mbili zilikufa ila kakaundwa kainchi ambako siyo sovereign state (Zanzibar) na kukawa na Sovereignty state yaani Tanzania. Ndio maana hakuna Tanganyika, sasa idadi sawa inatoka wapi wakati tuna Tanzania ambayo ni yetu sote? Huu muungano utata mtupu na chokochoko zinaanzia hapo hapo kwenye idadi sawa!! KWA ZANZIBAR CHAO CHAO CHETU CHAO, alaaa, nani akubali?

Mkuu.
kwa jinsi muungano unavyoendeshwa uko sahihi katika hoja yako.

Lakini pia si kweli kuwa Tanganyika ilitoa mamlaka yake yote muungano ulipoanzishwa, Zanzibar pia haikutoa mamlaka yake yote kwa mamlaka mpya(Muungano au serikali ya Muungano)..pia mamlaka mpya haiwezi kujikwapulia madaraka ambayo haikupewa na Tanganyika na Zanzibar kama waanzilishi wa Muungano.

Au mkuu unabisha kuwa inatakiwa iwepo mamlaka ya Tanganyika, mamlaka ya zanzibar na mamlaka ya muungano?
kama umenisoma hapo juu kuna sehemu nimesema Mwalimu kwa "utaalamu" wake alichanganya mamlaka ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano pamoja. hali hii ndi iliyozaa, inayozaa hitimisho kuwa Tanganyika haipo au Zanzibar haina soverignty status.
mkuu kama mtu mwenye akili timamu niambie kuna nchi inayosalimisha mamlaka yake yote kwa nchi nyengine?

mkuu. tunawalaumu wazanzibari kwa makosa ya "viongozi" wetu wa Tanganyika.
Wapi umepata kusikia au kuona duniani jina la nchi huru linapotea katika ramani ya dunia au hata katika akili za watu?
Tanzania si nchi moja..Tanzania ni nchi mbili. Tanganyika na Zanzibar.

kwa ufupi ni hivi.
mambo ya Tanganyika..mamlaka ya Tanganyika, nchi ya Tanganyika...
mambo ya Zanzibar.....mamlaka ya Zanzibar, nchi ya Zanzibar.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar...mambo ya Muungano, kumi na moja..orodha leo imefika 22 au 32 inategemea uchambuzi. mamlaka ya Muungano, serikali ya Muungano inayofanya kazi kwa niaba ya nchi mbili.

Mkuu. kwa msimamo wangu ili kufanya Tanzania nchi moja ilibidi Karume auawe, vyama viunganishwe, TANU na ASP, kuchagua viongozi wa kuongoza Zanzibar huku Tanganyika. kuwafukuza katika uongozi wote wanaokosoa muungano...kuondoa madaraka ya rais wa zanzibar kuwa makamo rais wa muungano na hivyo kuipa serikali ya zanzibar status ya local gvt....still Tanzania haijawa nchi moja bado.
The only thing left ni kui-annex Zanzibar hilo litafanya Tanzania nchi moja.

Tatizo sisi wachangiaji hapa tunachangia mada kama hizi kinafiki na kiushabiki. Ukweli uko wazi kwa mwenye macho kuona na mwenye akili kufikiri.

Kwanza kabisa ni kwamba nina akili timamu. Na kwa akili zangu timamu nimeona kuwa Tanganyika haipo ila Zanzibar ipo ndio maana hakuna Mtanganyika anayeweza kupata ubunge/uwaziri Zanzibar ila kwa Tanzania Wizara za Ulinzi na Mambo ya Ndani ziko mikononi mwa Wazanzibar!! Soma Katiba hakuna kitu kinaitwa Tanganyika, ilijifia mwaka 1964 tukawa na Tanzania mara iitwe Tanzania Bara hata sielewi ni nini hiki. Nami siwalaumu Wazanzibar hata kidogo nalaumu mfumo tu wa Muungano. Nadhani tukipata sheria nzuri ya kuchakata katiba tutaweza kuuona Muungano huu kwa macho mawili na katiba itakayokuja natamani ishughulikie muundo wa Muungano. Nimefarijika kidogo kuona kwamba Tume ya Katiba itapitia pia Articles of Union miongoni mwa nyaraka itazopitia.
 
Kwa wale wanaopenda kusifu nyerere, hili pia ni kosa la nyerere. Alaumiwe yeye, kwa kutaka kuikurusedi Zanzibar kwa hila, akaona akiiuwa Tanganyika itakuwa rahsi kuimeza Zanzibar, kumbe ni "wrong calculation" kama ilivyo katika maamuzi yake yote.

Leo isingekuwa kiherehere cha nyerere watu msingekuwa mnalumbana humu, Nakumbuka nyerere mpaka aliwahi kusema kuwa hajui jina la Tanganyika limetokea wapi? Khaaa! Hajui kama hilo ni jina kiarabu typical? Na usomi wake wote? Kashindwa kujuwa Tanga = Tangier ?
 
Ukweli ni kwamba CCM ya bara ndiyo inayonufaika na huu muungano kila inapowadia uchaguzi mkuu. Maana huwa wanavuna kura nyingi sana za urais kutoka Zanzibar. So piga ua galagaza CCM wanaajenda ya siri kwenye thiz stupid muungano. Binafsi sitaki hata kusikia kitu kinachoitwa muungano
 
Inashangaza sana kuona jinsi serikali ya Muungano inavyoipendelea Zanzibar.. umeme hawana mgao na bado hawalipi ankara, nafasi za kazi kwenye serikali ya muungano kwa masuala ya muungano tuko pasu pasu, wao wanaweza kununua ardhi bara lakini wa bara hawezi kununua ardhi Zanzibar, wa bara hawezi kupiga kura Zanzibar (si raia) lakini wa Zanzibar kupiga kura Tanzania sawa kabisa.... na bado tume muhimu kama hizi za msitakabali wa nchi yetu tumewapa upendeleo usiokuwa wa kawaida

Tumieni nguvu ya umma ya CHADEMA kukataa huu muungano! Kinachojionyesha hapa ni kuwa ni wanafiki wa nafsi zenu. Kama hili linawakera kama upandaji wa hali ya maisha, Dowans, Ufisadi kuiondowa madarakani CCM basi jumuisheni hli la kuukataa Muungano.
 
Ukweli ni kwamba CCM ya bara ndiyo inayonufaika na huu muungano kila inapowadia uchaguzi mkuu. Maana huwa wanavuna kura nyingi sana za urais kutoka Zanzibar. So piga ua galagaza CCM wanaajenda ya siri kwenye thiz stupid muungano. Binafsi sitaki hata kusikia kitu kinachoitwa muungano
Wacha Bwana ! Hivyo kura 400,000 zinasaidia katika idadi ya kura zaidi ya milioni 10?
 
Wanouchukia sio Muungano wanachukia kuwa in spite ya hila za kikurusedi za nyerere (saint to be), zanzibar imeng'amua na sasa inajijuwa kuwa ilitaka kumezwa. Kitu kinachwaumiza sana ni utaifa wa Zanzibar, na chuki zimezidi baada ya wa bara wengi kunyimwa vitambulisho vua uzanzibari. Walikuwa wakipelekwa huko makundi kwa makundi, sasa hata wakae miaka 100, zanzibar imewastukia. Hapo sasa.
 
Kwanza kabisa ni kwamba nina akili timamu. Na kwa akili zangu timamu nimeona kuwa Tanganyika haipo ila Zanzibar ipo ndio maana hakuna Mtanganyika anayeweza kupata ubunge/uwaziri Zanzibar ila kwa Tanzania Wizara za Ulinzi na Mambo ya Ndani ziko mikononi mwa Wazanzibar!! Soma Katiba hakuna kitu kinaitwa Tanganyika, ilijifia mwaka 1964 tukawa na Tanzania mara iitwe Tanzania Bara hata sielewi ni nini hiki. Nami siwalaumu Wazanzibar hata kidogo nalaumu mfumo tu wa Muungano. Nadhani tukipata sheria nzuri ya kuchakata katiba tutaweza kuuona Muungano huu kwa macho mawili na katiba itakayokuja natamani ishughulikie muundo wa Muungano. Nimefarijika kidogo kuona kwamba Tume ya Katiba itapitia pia Articles of Union miongoni mwa nyaraka itazopitia.

Kwa manufaa ya kutaka kujua tu: Unakusudia ziko nchi mbili tu yaani Zanzibar na Tanzania? Sasa kama hivyo ndivyo mimi sioni tatizo kwani jina ni jina tu muuitwe Tanganyika au Tanzania.
Tatizo linaloliona mimi ni hili: jee hiyo Serikali ya Muungano iko wapi? kwa vile upande mmoja iko Zanzibar na upande mwengine iko Tanzania ambayo kwa maelezo yako (tena nakubaliana nawe kabisa) Ni hii hii Tanganyika ndiyo inayogeuzwa majina mara Bara mara Tanzania?
 
Muungano tulio nao sasa hivi siyo sawa. Muungano utakuwa sawa tu tutakapokuwa na serikali tatu (3). Ambapo yarikali ya Tanganyika itahusika na Tanganyika na Serikali ya Zanzibar itawahusu wazanzibari. Halafu tuwe na serikali ya Jamhuri itakayo jihusisha na mambo yote yatakayohusu muungano kama itakavyo kubaliwa. Haiwezerkani wewe ukawa waziri wa Jamhuri ya Muungano halafu eti wizara yako haihusishi mambo ya muungano eti kuna waziri mwingine zanzibar mwenye majukumu kama yako. Kwa nini usiitwe waziri wa serikali ya Tanganyika.

Nakubaliana nawe kabisa! Haiwezekani Magufuli aende akafunge mkataba wa kujega barabara ya Mwanza akitumia jina la Tanzania. Yeye sim Waziri wa Tanzania ni waziri wa Tanganyika!
 
Back
Top Bottom