Queen Esther
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 2,195
- 1,417
Niliwahi kusema humu JF kwamba Tanzania ina mambo ya ajabu sana kuhusiana na utoaji wa work na residence permits hata kwa watu ambao ni wawekezaji, japo kila siku tunapiga kelele eti kuvutia wawekezaji.
Wawekezaji wanapokuja wanapata shida sana kupewa work au residence permits. Kuna wawekezaji Tanzania wamekaa zaidi ya miaka kumi nchini na wengine hata kuoa au kuolewa na Watanzania lakini bado wananyimwa permanent residence permits.
Kuna wageni toka nje wenye utaalamu wengi sana Tanzania ambao wameoa au kuoelwa na Watanzania na kuwa na familia, lakini hata hawa hawaruhusiwi kufanya kazi nchini kwa ajili ya kutunza familia zao, wananyimwa work permits japo ni wake au waume wa Watanzania na serikali inasema haiwatambui kama wakazi wa kudumu nchini!
Hivi kweli kweli kuna watu na akili zao serikalini na huko Uhamiaji na hawaoni kuna tatizo hapa?
Kichekesho cha mwaka ni hili la hii NGO ya WUSC kutoka Canada. Wao walikuwa na ofisi nchini kusaidia na kutoa mafunzo kwa watu na taasisi mbalimbali nchini na hata za serikali. Wamekuwa na mchango mkubwa sana taasisi kama Chamber of Commerce (Women), Umoja wa Wakulima wadogodogo nchini (MVIWATA), Umoja wa Wajasiliamali wa Wahitimu wa Chuo Cha Sokoine (SUGECO) nk,
Lakini cha ajabu ni kwamba kila WUSC walipokuwa wanaomba vibali vya kazi kwa ajili ya wataalamu wao, Uhamiaji walikuwa wakiwakatalia na kuwakwamisha kwa sababu za kijinga kabisa. Ilifikia mahali uamuzi ukatolewa kwamba kwa sababu ya kukataliwa kupewa vibali basi ofisi ya WUSC nchini ifungwe.
Sasa siku ya kufunga rasmi ofisi ya WUSC, mgeni rasmi akawa Ofisa kutoka Wizara ya KIlimo. Hapo ndipo akawa anamwaga sifa kwa kazi iliyofanywa nchhini na WUSC na kuwaomba eti wasifunge ofisi na kuondoka!
Hivi Tanzania tuna watendaji wa namna gani lakinini? Kwa nini tunafanya mambo haya ya kijinga na kipumbavu kabisa - kama anavyosema Magufuli!
Hebu angalia ujumbe toka serikalini wakati WUSC wanafunga ofisi kwa kunyimwa work permits
View attachment 1390930View attachment 1390934
Ujumbe huu nataka uwafikie Raisi Magufuli na Waziri wa Mambo ya Ndani Simbachawene, kwamba kama kweli tunataka kuipeleka mbele Tanzania, tuache kabisa utendaji kama huu ambao ni mambo ya kijinga na kipumbavu ambayo hayawezi kufanywa na watu wenye akili timamu.
Source: IPPMedia
Govt simplifies issuance of work permits to attract more investments
Tafuta kuna uzi humu ndani wa hao jamaa zako baadhi waneoana wanaume kwa wanaume. Ilikuwa ni aibu kubwa kwa Taifa.
Queen Esther