Tanzania ina mambo ya ajabu sana; Uhamiaji inanyima watu wanaotusaidia uchumi work permits, wanapofunga ofisi na kuaga Serikali inawaomba wasiondoke!

Niliwahi kusema humu JF kwamba Tanzania ina mambo ya ajabu sana kuhusiana na utoaji wa work na residence permits hata kwa watu ambao ni wawekezaji, japo kila siku tunapiga kelele eti kuvutia wawekezaji.

Wawekezaji wanapokuja wanapata shida sana kupewa work au residence permits. Kuna wawekezaji Tanzania wamekaa zaidi ya miaka kumi nchini na wengine hata kuoa au kuolewa na Watanzania lakini bado wananyimwa permanent residence permits.

Kuna wageni toka nje wenye utaalamu wengi sana Tanzania ambao wameoa au kuoelwa na Watanzania na kuwa na familia, lakini hata hawa hawaruhusiwi kufanya kazi nchini kwa ajili ya kutunza familia zao, wananyimwa work permits japo ni wake au waume wa Watanzania na serikali inasema haiwatambui kama wakazi wa kudumu nchini!

Hivi kweli kweli kuna watu na akili zao serikalini na huko Uhamiaji na hawaoni kuna tatizo hapa?

Kichekesho cha mwaka ni hili la hii NGO ya WUSC kutoka Canada. Wao walikuwa na ofisi nchini kusaidia na kutoa mafunzo kwa watu na taasisi mbalimbali nchini na hata za serikali. Wamekuwa na mchango mkubwa sana taasisi kama Chamber of Commerce (Women), Umoja wa Wakulima wadogodogo nchini (MVIWATA), Umoja wa Wajasiliamali wa Wahitimu wa Chuo Cha Sokoine (SUGECO) nk,

Lakini cha ajabu ni kwamba kila WUSC walipokuwa wanaomba vibali vya kazi kwa ajili ya wataalamu wao, Uhamiaji walikuwa wakiwakatalia na kuwakwamisha kwa sababu za kijinga kabisa. Ilifikia mahali uamuzi ukatolewa kwamba kwa sababu ya kukataliwa kupewa vibali basi ofisi ya WUSC nchini ifungwe.

Sasa siku ya kufunga rasmi ofisi ya WUSC, mgeni rasmi akawa Ofisa kutoka Wizara ya KIlimo. Hapo ndipo akawa anamwaga sifa kwa kazi iliyofanywa nchhini na WUSC na kuwaomba eti wasifunge ofisi na kuondoka!

Hivi Tanzania tuna watendaji wa namna gani lakinini? Kwa nini tunafanya mambo haya ya kijinga na kipumbavu kabisa - kama anavyosema Magufuli!

Hebu angalia ujumbe toka serikalini wakati WUSC wanafunga ofisi kwa kunyimwa work permits

View attachment 1390930View attachment 1390934

Ujumbe huu nataka uwafikie Raisi Magufuli na Waziri wa Mambo ya Ndani Simbachawene, kwamba kama kweli tunataka kuipeleka mbele Tanzania, tuache kabisa utendaji kama huu ambao ni mambo ya kijinga na kipumbavu ambayo hayawezi kufanywa na watu wenye akili timamu.

Source: IPPMedia
Govt simplifies issuance of work permits to attract more investments

Tafuta kuna uzi humu ndani wa hao jamaa zako baadhi waneoana wanaume kwa wanaume. Ilikuwa ni aibu kubwa kwa Taifa.

Queen Esther
 
Unaweza kuwa right kwamba Wizara ya Kazi ndio kikwazo kwa work permits. Lakini ninachojua ni kwamba work permit ni aina ya residence permit. Ukishakuwa na work permit huhitaji tena kuomba residence permit.

Lakini suala la residence permit kwa watu waliokaa sana Tanzania au kuoa na kuolewa halina uhusiano na wizara ya Kazi

Uko sahihi mkuu. Hili swala zima likipaswa kuwa la uhamiaji kwa nje lakini ndani wizara ya kazi ikawa na rights katika mchakato. Au likawa swala la wizara ya kazi na idara ya uhamiani ikawa na rights katika mchakato. Haileti mantiki mtu aliyepata work permit akakosa resident status wakati kazi zinafanyika ndani ya nchi. Na ndio maana nchi nyingine work permit inatolewa kwa pamoja na resident permit katika idara moja ya kazi!! Ila ukiomba resident permit, wewe ni wa idara ya uhamiaji. Kenya ni mfano!!

Ukiritimba ndio vyanzo vya haya yote!!
 
Ndio maana watu wanasistiza Magufuli ajikite kwenye mifumo. Ku-deal na hizi issues kama isolated cases haitatupeleka popote. Anaweza kusikia hili akaamrisha hawa watu wapewe work permits mara moja na kuwatukana hata kuwatumbua watendaji waliowakwamisha. Lakini hilo halitatui tatizo lililopo.
 
Wamefanya mambo mazuri sana nchini. KUna wakati nilidhani wanakuwa wanamsoma Magufuli kujua nchi inahitaji nini. Leo nasikia eti wanafunga ofisi kwa kuwa Uhamiaji wamekuwa wakiwanyima work permits! Sikuamini nilichoona. Tuna watu wapumbavu na wajinga sana kama watendaji serikalini.
Walikujakujaje hapa nchini? Wanachojishughulisha nayo imesaidia nini nchi hii so far toka wamekwepo hapa nchini? Bila wao kuwepo nini kitatokea?. Kuna mahali wanaita Yaedachini wilayani Karatu ambapo kuna NGOs zaidi ya 50 ambayo yote yanajifanya kuhangaika na ukombozi wa jamii ya Hadzabe na Barbaig lakini hakuna aliyekombolewa, badala NGOs hizo zinajistawisha tu. Ngorongoro the samw. Achana na hizo biashara, let them go.
 
Hapa lazima kuna jambo ambalo mleta mada hulielewi. Tafuta kufahamu undani wa sababu za kukataliwa work permit. Hawa watu usiwachezee wengine huingia kwenye nchi zetu na malengo marefu na ya hatari sana kwa Taifa. Usiharakishe kuilaumu serikali.
 
Niliwahi kusema humu JF kwamba Tanzania ina mambo ya ajabu sana kuhusiana na utoaji wa work na residence permits hata kwa watu ambao ni wawekezaji, japo kila siku tunapiga kelele eti kuvutia wawekezaji.

Wawekezaji wanapokuja wanapata shida sana kupewa work au residence permits. Kuna wawekezaji Tanzania wamekaa zaidi ya miaka kumi nchini na wengine hata kuoa au kuolewa na Watanzania lakini bado wananyimwa permanent residence permits.

Kuna wageni toka nje wenye utaalamu wengi sana Tanzania ambao wameoa au kuoelwa na Watanzania na kuwa na familia, lakini hata hawa hawaruhusiwi kufanya kazi nchini kwa ajili ya kutunza familia zao, wananyimwa work permits japo ni wake au waume wa Watanzania na serikali inasema haiwatambui kama wakazi wa kudumu nchini!

Hivi kweli kweli kuna watu na akili zao serikalini na huko Uhamiaji na hawaoni kuna tatizo hapa?

Kichekesho cha mwaka ni hili la hii NGO ya WUSC kutoka Canada. Wao walikuwa na ofisi nchini kusaidia na kutoa mafunzo kwa watu na taasisi mbalimbali nchini na hata za serikali. Wamekuwa na mchango mkubwa sana taasisi kama Chamber of Commerce (Women), Umoja wa Wakulima wadogodogo nchini (MVIWATA), Umoja wa Wajasiliamali wa Wahitimu wa Chuo Cha Sokoine (SUGECO) nk,

Lakini cha ajabu ni kwamba kila WUSC walipokuwa wanaomba vibali vya kazi kwa ajili ya wataalamu wao, Uhamiaji walikuwa wakiwakatalia na kuwakwamisha kwa sababu za kijinga kabisa. Ilifikia mahali uamuzi ukatolewa kwamba kwa sababu ya kukataliwa kupewa vibali basi ofisi ya WUSC nchini ifungwe.

Sasa siku ya kufunga rasmi ofisi ya WUSC, mgeni rasmi akawa Ofisa kutoka Wizara ya KIlimo. Hapo ndipo akawa anamwaga sifa kwa kazi iliyofanywa nchhini na WUSC na kuwaomba eti wasifunge ofisi na kuondoka!

Hivi Tanzania tuna watendaji wa namna gani lakinini? Kwa nini tunafanya mambo haya ya kijinga na kipumbavu kabisa - kama anavyosema Magufuli!

Hebu angalia ujumbe toka serikalini wakati WUSC wanafunga ofisi kwa kunyimwa work permits

View attachment 1390930View attachment 1390934

Ujumbe huu nataka uwafikie Raisi Magufuli na Waziri wa Mambo ya Ndani Simbachawene, kwamba kama kweli tunataka kuipeleka mbele Tanzania, tuache kabisa utendaji kama huu ambao ni mambo ya kijinga na kipumbavu ambayo hayawezi kufanywa na watu wenye akili timamu.

Source: IPPMedia
Govt simplifies issuance of work permits to attract more investments
Kila nchi Ina utaratibu wake ndugu, siyo suala la kuwekeza au kuoa na kuzalisha, permanent resident permit Ina mambo mengi, unaweza kuwa mwizi,jasusi, illegal immigrants,
Hutaki kufuata Sheria za nchi . Hapo permanent residency sahau kabisa. Hata nchi za dunia ya Kwanza unaweza kukaa miaka 50 lakini kila ukiomba unapigwa chini, kama unajiusisha na mambo kinyume na sheria za nchi hiyo. Mfano USA, Japan, Australia etc.
 
Kufunga ofisi kwasababu ya kukosa work permit inamaanisha ni idadi kubwa ya wafanyakazi wamekosa permit kiasi cha kuathiri utendaji. Ina maana hizi NGOs zimejaa wageni kiasi hicho? Mbona kuna kampuni nyingi tu zina wafanyakazi wananyimwa permit na kampuni hazifungwi?
Huyu jamaa inawezekana ana bwana wake kanyimwa resident permit
 
Back
Top Bottom