Tanzania imetimiza hatua zote 4 kuwa nchi ya kidikteta

Safi sana. dikiteta wetu hana hata chembe ya "usomi" Ana PHD lakini utadhania Samaki. Samaki anaishi ndani ya maji lakini mchafu! Magu alipita tu kwenye mifumo ya elimu. utamjua kwa jinsi anavyojenga hoja zake. akiulizwa kwa nini hukutani na wapinzani, anasema wanataka kunikata kichwa!

Hapa anabomolea watu, kule anasema wasibomolewe ni wapiga kura wangu. hiyo ni dalili ya kukosa weledi na fikra.

mpaka hivi sasa anafanya mambo yanayoonekana wazi kwamba yatatugharimu, na kwa kweli tunagharimika. baadaye tutajifunza, baada ya kulipa gharama kubwa. Mkapa aliwakebehi waliohoji uwekezaji wa madini. leo kiko wapi? Magufuli naye kadhalika
 
1. kuongoza nchi kwa matamko badala ya utaratibu wa kawaida wa kiserikali. Ghafla tulitangaziwa kuhamia dodoma, tena kwenye podium ya uenyekiti wa ccm. hapa kuwa na michakato ya kiserikali ilivyo kawaida. tena bajeti ilikuwa imepita. wazo lenyewe lilishachina. yeye kaagiza tu.
2. Kutoa maagizo yanayovunja sheria na katiba. Ni rais wa kwanza kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa, tokea mfumo uliporejea mwaka 1992. Hata Nyerere aliporudisha nchi kwenye chama kimoja, alileta mchakato wa kubadili katiba kwanza.
3. Kusababisha vurugu kubwa katika ngazi za juu. Huu mtifuano wa kijinga kati ya CAG na Spika Ndugai umetokea bila comment kutoka Ikulu. confidence ya Ndugai inatuonesha JPM ndiyo alieendesha hilo zengwe.
Hayo ni machache tu mengine baadaye
 
kuna watu wanajua ukweli kabisa kuhusu utawala huu wa mabavu lakini ndio wamekuwa mstari wa mbele ktk kutetea,
 
Leo umeongea point kubwa sana. Adui wa watanzania ni CCM nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni kweli kwamba Urusi ilisambalatika kwasababu ya Mikhail Gorbachev kua "pandikizi la USA" au UJAMAA ndio ulishindikana? Kama alikua ni pandikizi wa USA, kwanini nchi zote (including China )UJAMAA/Ukominist ulianguka hata kwenye hizo nchi ambazo huyo pandikizi hakua mtawala!? Putin pamoja na kwamba anasifiwa hapa, nae hakuurudia UJAMAA, anaendesha nchi kibepari na sio UJAMAA aliokulia huko mwanzoni. But again, nambie kitu gani kipya walicho nacho Warusi leo kitecknolojia ambacho Putin kaleta kipya zaidi ya ile iliokua USSR? Technology ya silaha walio nayo leo Urusi ni kweli ipo advanced but ni mashindano yale yale yaliokuwepo Enzi za ile ilikua United Soviet wakishandana na USA!
 
Sasa kwa akili yako putin asingewekeza kwenye teknolojia na jeshi urusi ingeweza kushindana na Marekani?

USSR ilikuwa ni muunganiko wa nchi nyingi za kikomunisti huko Asia na Ulaya Mashariki na Hub kuu ilikuwa ni Urusi, baada ya kuingia Mikhail Gorbachev Urusi ilianguka na kuifanya USSR pia kuanguka.

Putin ni rais mwenye upeo mkubwa sana, na sijasema popote kuwa Putin anaendesha Urusi kwa misingi ya ukomunisti.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni lazima utakuwa Mchaga wale wa chini kabisa, kifua kimekujaa chuki hata huoni mbele.
Ukabila unatoka wapi hapa ......... kwa taarifa yako Mimi ni Msukuma, same as Nyani na Pascal Mayalla.

By the way, hivi kuna mtu ana roho mbaya na chuki humu JF zaidi yako ...!!?
 
Ambacho sikubaliani na wewe ni kuhusu eti huyu former USSR president kua ni pandikizi la USA, if that is true, kwanini UKOMINIST uanguke everywhere in the world na sio Urusi pekee yake? Still Putin, nasisitiza kaendeleza tu yale yaliokuwepo tokea Enzi za USSR ya ukominist kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama, remember Putin ni zao la KUG (hapa kwetu ni TISS) wakati wa huyo unae mwita "pandikizi la USA" so anajaribu kutembelea mule mule alimokulia but nyakati za aina ya siasa zile alizokulia ndio zimeshindikana, inabidi tu aimbe Kimarekani/Kimagharibi hata kama hataki.
 
Putin alikuwa agent wa KGB ( shirika la ujasusi USSR/Russia) na sio KUB,
Hebu weka sababu za kuanguka kwa ukomunisti duniani, naona una deny sababu kuu niliyoiweka mimi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa zitto aliongea ukweli mtupu,yule baba wa Chato hakuwa akijua mahali Dunia ilipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…