Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Hisa inakua hisa kwahiyo unataka kusema siyo hisa tuiteje ambacho sijaelewa hapati mgao? au anapata dalaja kitu gani?mdaraja yote nimadaraja tu hadi f nidaraja hapo hoja hakuna kuna 16%swali lilikua wewe hujaona kitu kimefanyika?
Hisa daraja la ngapi?
Unajua maana ya hilo daraja?
Magufuli ameaibika pakubwa.
 
Nchi imepoteza mno kwenye sakata la Makanikia [ Fedha za kigeni $200M na TZS 430B Mapato ya Serikali]

  • mwaka 2016 Tanzania iliuza nje dhahabu iliyoingiza USD 1.8 bilioni
  • Mwaka wa Makanikia 2017 mauzo nje yalishuka mpaka USD 1.6 bilioni na;
  • Mwaka 2018, mwaka ambao athari ya Makanikia ilikuwa mwaka mzima mauzo nje yalikuwa USD 1.4 bilioni

Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%.

Katika kipindi hicho uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka tani 43 za dhahabu mwaka 2015 mpaka tani 39 mwaka 2018. Uzalishaji wa mwaka 2018 ulikuwa sawa na uzalishaji wa mwaka 2010.

Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka katika kipindi cha Makanikia. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ).

  • mwaka 2016/17 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 341 bilioni
  • Mwaka 2017/18 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 230 bilioni
  • Mwaka 2018/19 makusanyo yalikuwa TZS 220 bilioni.
Serikali imekadiria kukusanya TZS 350 bilioni mwaka 2019/2020.

Kwa mujibu wa Dkt. Genuine Martin kwenye mada yake kwa Policy Forum Breakfast Debate Julai, 2019 Mapato yote ya sekta ya Madini yameshuka kwa 32% katika zama za Makanikia.

  • mwaka 2016 Mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni
  • Mwaka 2018 Mapato yalikuwa TZS 867 bilioni.
Katika Miaka 2 Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni.

Tunapata nini kutoka Barrick Gold baada ya sakata la Makanikia?

Mapato ambayo Serikali ya Magufuli imepoteza kwenye sekta ya Madini kati ya mwaka 2017 - 2019 ni makubwa zaidi ya malipo* ambayo Serikali inasema tutalipwa na Barrick Gold Corporation ili kumaliza mgogoro baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali.

Tumeona hapo juu kuwa tumepoteza Mapato ya Fedha za kigeni $200M na Mapato ya Serikali kushuka kwa TZS 430 bilioni. Kutoka Barrick tunatarajiwa kupata $300M ambazo chache kulinganisha na kiasi tulichopeteza.

* Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ).

Kwa hiyo Tanzania imepoteza Mapato iliyokuwa yakusanywe kama mgogoro usingekuwepo [ $200M exports revenues and $170M tax revenues ] na imeishia kuilipa Barrick badala ya yenyewe kulipwa.

Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.


Tatizo la wawakilishi wa Tanzania hii hyo loss n tayar n hasara Sasa ili kucover hyo hasara unashaur tufanyaje?

Mie nadhan ungekuja na hoja tuongeze kufanya Kaz kwa juhudi, au uje na namna yoyote ile positive, Hapo huna tofauti na vijana wawili waliopotea msitun na kuanza kulumbana kuwa wewe ndo ulosema tupite njia hii namwenzie akimtuhumu hvyo hvyo jion itafika hamtotoka porin mtabaki humohumo.

Sema Nini kifanyike
 
Mkuu angalia hicho kipindi anachosema kuna hasara ni kipindi ambacho Serikali na Accacia/Barrick walikuwa kwenye mvutano. Na kama angalau umefika darasa la Saba ulipsawa kujua jaribio lolote la kutaka kuleta mabadliko kwenye sekita lazima lingeleta mvutano ambao kwa vyovyote vile ungeathiri sekita katik nyanya zote. Tunaweza kufikia hitimisho kama kilichofanya kimeleta hasara baada ya mvutano kuisha na kuangalia nini kimepatika. Kabla ya hapo kusema Kuna hasara huo ni Ushehe Yahya mkuu.
Muulize pia mzee wa MIGA vipi hawaendi tena hiyo safari?
 
Naomba sheria ya takwimu irudishwe watu wameanza kupotosha tena
Hivi dawa ya kudhibiti upotoshaji ni kuleta sheria za kibwege au kuja kutoka hadharani na kuclarify
 
Kivipi? Hizo data za Serikali sio zangu. Hizo za malipo ya Barrick zimetolewa na Barrick. Sasa Mimi nina kosa gani? Kuwaletea humu?
Kosa lako ni kuzileta kisiasa na kipropaganda wakati wewe kama Mchumi unaelewa wazi kabisa ilikuwa lazima iwe hivyo kutokana na kile kilichofanywa na Serikali na ambacho for years umekuwa ukitoa povu kifanyike!
 
Narudia tena hoja yako ni nini?? Hueleweki mkuu
Hoja yangu ni kwamba wewe kama msomi na mtu uliyejitanabaisha kama mtu uliyetaka yafanyike mageuzi katika sekita ya Madini unafahamau kabisa jaribio lolote la kufanya mageuzi hayo lazima lingeleta athari katika sekita. Sasa unapokuja kulalamika tena eti Kuna hasara kwangu mimi naona ni unafiki. Mchumi Kama wewe ulipaswa ujue hayo. And on this kwangu amefanikiwa, hajafanikiwa siyo issue. Issue ni kwamba amethubutu na wewe kwa hili ulipaswa uwe naye bega kwa bega lakini ndio kwanza ukaanza kupinga tena.
 
We ndo kichwa maji kabisa. Unajua maana ya Rais wewe.
Mkuu mwambie maana ya Rais,au maana ya rais ni kutestia hypothesis zako za kijima na kukosa exposure kwa expense ya nchi na watu wake
 
Mikataba yote anayo, Team ya Wataalam anayo anashindwaje kufanya Jambo kwa Uhakika mpaka aamue mwenyewe kwa atakavyoona inafaa !!?.

Nnadhani Mh Rais anayo nafasi kubwa sana ya kufanya Jambo kwa uhakika huku akifahamu Faida na Hasara zake.Haya haya Makinikia yuliambiwa tulikuwa tunaibiwa (Ref Ripoti ya Profesa Usoro) na tuliaminishwa hapa tunawadai hao Mabeberu Trillion mia nne na usheee kilicho fuatia tuliambiwa tutalipwa kishika Uchumba..

Tuombe uzima Mkuu ,tutakutafuta baadae wakati wa Matokeo ya haya yanayo fanywa na Mh Rais wetu Mtukufu na mpendwa sana.
Mkuu hawa ni wapumbavu hawawezi ona unachozungumzia hapa.
 
By the way, mbona watu wengine walikuwa wanapenda kuona Acacia inashinda na serikali inashitakiwa? Walikuwa wanapata nini?
Terrible. Israel ukifanya hivyo unabadilika jina immediately. Siasa yes, lakini sio suala la compromising them

..Barrick na Accacia hawakuigia nchini kwa kutumia mtutu wa bunduki.

..uwepo wao hapa nchini uliwezeshwa na sheria zilizopitishwa na wabunge.

..mikataba yao ya kinyonyaji iliidhinishwa na waTz wenzetu tuliowakabidhi madaraka.

..wizi ulifanyika kwa zaidi ya miaka 15 na kila aliyepinga sheria, mikataba, na wizi wa madini, aliingia ktk matatizo na wabunge wa ccm, serekali ya ccm, na vyombo vya dola.

..sasa tujiulize: Je, waliotetea barrick na accacia kwa miaka 15 walikuwa wakipata nini? Je, walikuwa na "udhu" wa kupigania rasilimali zetu sasa hivi?

..Kosa letu ni kuamini kwamba walioshirikiana na Accacia kutuibia wana uwezo wa kufanya mazungumzo na Barrick na kutupatia +ve results.
 
Nikweli kwanza anatakiwa atueleza kabla ya Makinikia (wakati wa shamba la bibi) zilizokuwa nizapotea ni shilingi ngapi na walidhibiti ngapi, na kwa sasa zinapotea ngapi na udhibiti ni ngapi halafu alinganishe na hoja yake. Maana kwa hoja yake anamaanisha bora tungeendelea vile vile kabla ya Makinikia.
Hasara tuliyopata Zito anasema inatokana na nini? au hukusoma,au hizo kodi anazozungumzia zimeanza kutozwa baada ya mkurupuko?Magufuli atawandanganya na kuburuza sana,na kwa akili hizi mtaitwa wapumbavu sana
 
Kivipi? Hizo data za Serikali sio zangu. Hizo za malipo ya Barrick zimetolewa na Barrick. Sasa Mimi nina kosa gani? Kuwaletea humu?

Unaposema kwa kutumia mifano ya kitu kimoja tu sidhani kama ni balanced information. Kwa mfano, inabidi uchambuzi wa kina ufanyike kuhusu aftermath ya maamuzi ya kutengeneza upya namna ya biashara ya uchimbaji na uuzaji wa madini kati ya serikali na Barrick utakavyofanywa.

Kama mtanzania, uamuzi wa kuwatingisha Barrick umebadili kabisa mwelekeo wa uchimbaji wa madini. hapa lilikuwa ni shamba la bibi, na kusema kweli ni kama tuliwachukulia wawekezaji ni miungu Fulani. Mambo yamebadilika sababu ya ujasiri wa kusema hapana. Kuwavuruga wale jamaa kumewapa funzo kuwa mambo huenda yakabadilika, Next time watakuja kwa akili na maarifa Zaidi. Na hawatakubali wajanja walio kwenye siasa kubadili mikataba ili iwanufaishe kama walivyofanya huko nyuma. Kigoda(RIP) aliweza kufanya hivyo,je kwanini asitokee Kigoda mwingine baadae?
 
..Barrick na Accacia hawakuigia nchini kwa kutumia mtutu wa bunduki.

..uwepo wao hapa nchini uliwezeshwa na sheria zilizopitishwa na wabunge.

..mikataba yao ya kinyonyaji iliidhinishwa na waTz wenzetu tuliowakabidhi madaraka.

..wizi ulifanyika kwa zaidi ya miaka 15 na kila aliyepinga sheria, mikataba, na wizi wa madini, aliingia ktk matatizo na wabunge wa ccm, serekali ya ccm, na vyombo vya dola.

..sasa tujiulize: Je, waliotetea barrick na accacia kwa miaka 15 walikuwa wakipata nini? Je, walikuwa na "udhu" wa kupigania rasilimali zetu sasa hivi?

..Kosa letu ni kuamini kwamba walioshirikiana na Accacia kutuibia wana uwezo wa kufanya mazungumzo na Barrick na kutupatia +ve results.
Na huyu msanii wao wa sasa amewafanya nini hao waliotuingiza mikataba mibovu,au hao waliotetea wizi for 15 years au amefanya nini hiyo mikataba zaidi ya kusababisha hasara zaidi
 
..Barrick na Accacia hawakuigia nchini kwa kutumia mtutu wa bunduki.

..uwepo wao hapa nchini uliwezeshwa na sheria zilizopitishwa na wabunge.

..mikataba yao ya kinyonyaji iliidhinishwa na waTz wenzetu tuliowakabidhi madaraka.

..wizi ulifanyika kwa zaidi ya miaka 15 na kila aliyepinga sheria, mikataba, na wizi wa madini, aliingia ktk matatizo na wabunge wa ccm, serekali ya ccm, na vyombo vya dola.

..sasa tujiulize: Je, waliotetea barrick na accacia kwa miaka 15 walikuwa wakipata nini? Je, walikuwa na "udhu" wa kupigania rasilimali zetu sasa hivi?

..Kosa letu ni kuamini kwamba walioshirikiana na Accacia kutuibia wana uwezo wa kufanya mazungumzo na Barrick na kutupatia +ve results.

I agree with you 100%. Ila watanzania hawa ambao wanatumia ujanja ujanja kutuuza wote kwa maslahi yao, lazima wakome. Namna walivyofanyiwa Barrick, next time, hawatafanya makossa waliyofanya huko nyuma. Unabadilisha mkataba mzima wa serikali halafu shares unampa individual (Kigoda)? How on earth could that be possible?
Mkuu, wana siasa ndio hao hao...wanabadilika kidogo sana.
 
Hata mimi namshangaaga huyu jamaa (Zitto)..ila kitu kimoja tunachofanana mimi na WEWE ni kwamba tunakosa FACTS za kujibu the so called LIES zake na hatimaye tunabakia kumshambulia na kumtuhumu ni KIBARAKA. Naomba tujitahidi kucounter facts zake ili tumuweke sawa aache the so called political stunts. Nakuomba saana nisaidie kutafuta facts tumuumbue la sivyo JF watatushambulia kwa PERSONALTY ATTACK and not FACTS.

Tafadhalii.
Huyo anayejiita kajekudya akikuletea hizo facts naomba uni-tag!! Kwanza mimi namuona ni kama kiroja! Zitto ametoa reference kwamba, taarifa alizoleta ni kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ). Lakini mtu kwa kukosa weledi, anadai ushahidi! Ndugu yangu kajekudya, ni ushahidi upi unaotaka wewe wakati umeambiwa source ya taarifa yake?! Ungekuwa smart wa kushindana kwa hoja, ungetafuta hicho kitabu halafu halafu ulete hapa kilichondikwa tofauti na alichoondika Zitto! Kinyume chake, unaonekana nawe ni wale wale tu; wapiga makofi msiojua what's exactly going on! Majuzi hapa kaleta makubaliano ya Barrick na GoT, tena mkawa mnataka ushahidi wakati full report inapatikana kwenye website ya Accacia, na gharama ni bundle yako tu kwa sababu ipo pale kwa matumizi ya umma!!

Tatizo lenu wengi wenu uelewa mdogo, na kama uelewa mnao basi mnajitia tu hamnazo kwa ajili ya maslahi ya chama au maslahi ya home boy!
 
Na huyu msanii wao wa sasa amewafanya nini hao waliotuingiza mikataba mibovu,au hao waliotetea wizi for 15 years au amefanya nini hiyo mikataba zaidi ya kusababisha hasara zaidi
Man, sio miaka 15, hawa jamaa wameanza kutuibia kwa zaidi ya miaka 20 sasa!!! Mikataba ya hovyo ilianza kuingiwa awamu ya role model wa Jiwe, namaanisha Mkapa! Na kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani angalau mkataba mmoja ulikuwa tangia wakati wa Mwinyi! So, in short ni tangia back 1990's sisi tumekuwa ni watu wa kupigwa tu!
 
Back
Top Bottom