Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Ni kweli tupo kwenye ulimwengu wa kidigital, hivyo huwezi kuwakwepa watumiaji wa mitandao. Maana mitandao kama JF huku watu wanatiririka ukweli tofauti na kwenye magazeti.
Lakini hii sio sababu ya kusema kuwa serikali iwe na watumishi amabo inawalipa mishahara alafu hawajui masuala ya kitaalamu na kiutawala. Matokeo yake eti likitokea kosa wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii ndio wapost juu ya hilo kosa na kisha serikali kujirekebisha.
Mfano alipofariki hayati rais JPM, rais wa sasa alitangaza maobolezo kinyume na sheria ya mazishi ya viongozi, na alisema maombolezo ni siku kumi na nne. Ni aibu ofisi nyeti ya ikulu ambayo inawatalaamu wa kila namna wakiwemo wanasheria kumuingiza chaka aliyekuwa mtoa taarifa. Lakini kosa hili lilibainishwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa JF na baadae wakajirekebusha.
Hii ya kuteua kada wa Ccm awe mkurugenzi wa TPDC ni doa baya sana kwa ofisi ya rais hasa ukizingatia sifa za huyo kada ukilinganisha na unyeti wa shirika alilokuwa anapaswa kuliongoza. Nalo ni watumiaji wa mitandao ndio waliliibua na baada ya masaa 12 ndio akatenguliwa.
Hii inatupa picha mbaya sana juu ya watu ambao wanalipwa mishahara mikubwa kwa kutumia kodi za wananchi huku wakionyesha wazi kuwa hawana uwezo wa kutimiza wajibu wao.
Je, kama kungekuwa hakuna mitandoa ya kijamii ingekuwaje?