Hata mimi hayo mawazonilikuwa nayo.sasa hivi nina akilinajua jeshi la polisini makanjanga tu.Ndugu wana bodi,wakati nikiwa mdogo enzi za mwalimu kuliwahi kuwa na uvumi kuwa Tanzania ilikuwa na idara nzuri sana ya TISS hata ikawa nchi ya Tatu kwa upelelezi duniani,kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya ezi hizi,nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chafu ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori,lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.
Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa
Zilikua ni story za utotoni tu!
Kuwa ya tatu inawezekana siyo kweli ila ni kweli kuwa ofisi ya usalama wa taifa ilikuwa ikijua sana kazi yake wakati huo. Kuna mtu alikuwa akiitwa Walingozi, yule bwana alikuwa siyo mchezo katika mambo ya usalama. Ni kutokana na usalama huo kuwa ingawa Nyerere alikuwa na maadui wengi matajiri, lakini walishindwa kabisa kumgusa. Kila wakijaribu mapinduzi wanakwapuliwa kabla hawajafika popote. Kwenye ile kesi ya akina Hans Pope, mmoja wa watuhumiwa (nadhani Badru Kajaja) katika testimnoy yake alionyesha kufadhaishwa sana kuwa plani zao zote zilipanguliwa na jamaa wa TISS katika muda ambapo ilikuwa zianze kutekelezwa kiasi kuwa wote wakachanganyikiwa wasijue namna ya kuendelea.
kwa hiyo.......wa zamani walikuwa hadi darasa la sabaPolisi siku hizi kaka wanachukuliwa hadi form 4 leaver 2 ht km ana div 4 pnts 32 anaenda depo unategemea nn?
Usalama unaongozwa na mgeni toka nchi ya zanzibar wategemea nini..miujiza hii ipo tanganyika tu!...na mimi nikipewa nchi hii nitamteua mhindi ili tuwalishe pilipili mpaka..
Hakuna chombo chochote kile duniani ambacho hufanya kaz ya kupima na kutoa remarks in ranks kwa vyombo vya upelelezi duniani (intelligence agencies) kutokana na utendaji wao kwasababu task nying za vyombo hivi huwa ni siri na haziwi published baada ya kufanyika na hta ikitokea izo task zikajulikana bas huwa baada ya muda mrefu mf. operation dhidi ya Lumumba imeichukua dunia miaka takriban 40 kuujua ukweli, task ya MI6 kubroke Enigma codes za wajeruman kweny WW II ilikuja kujulikna after yrs.
Hivyo hizo assesment hufanywa na watu personally lakini mapungufu yake ni makubwa. Binafsi napingana na hilo la TISS kua ya tatu! unless nalata vgezo dhidi taasisi nyingne.
Mr. .......007;
Hapo kwenye red panaonekana patamu mno, lakini sielewi chochote, and I'm not kidding. Unaweza ukadadavua kidogo stori zake kwenye red hizo hapo mbili?