Tanzania iliwahi kuwa nchi ya tatu kwa upelelezi duniani

socratess

Member
Apr 22, 2012
37
22
Ndugu wana bodi,wakati nikiwa mdogo enzi za mwalimu kuliwahi kuwa na uvumi kuwa Tanzania ilikuwa na idara nzuri sana ya TISS hata ikawa nchi ya Tatu kwa upelelezi duniani.

Kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya ezi hizi,nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chafu ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori,lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.

Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa.

 
Ndugu wana bodi,wakati nikiwa mdogo enzi za mwalimu kuliwahi kuwa na uvumi kuwa Tanzania ilikuwa na idara nzuri sana ya TISS hata ikawa nchi ya Tatu kwa upelelezi duniani,kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya ezi hizi,nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chafu ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori,lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.
Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa
Hata mimi hayo mawazonilikuwa nayo.sasa hivi nina akilinajua jeshi la polisini makanjanga tu.
Nchi zilizo endelea wenzetu wako mbali sanaw
 
Zilikua ni story za utotoni tu!

Ulisikia MABOMU na Kulipuliwa kwa WATU kama Jirani zetu KENYA? Na Unajua tulikuwa tunaadua MAKABURU; Wakimtumia BANDA; WARENO; MOBUTU na CIA... Lakini TUlikuwa hatupigwi Mabumu nchini kwetu hata kidogo...

Na IDD AMIN Maeneo ya KAGERA na alitaka kweli kuilipua Hospitali ya BUGANDO

Au Unataka kutuambia ni AMANI TOKA kwa MABABU ZETU??
 
Usalama unaongozwa na mgeni toka nchi ya zanzibar wategemea nini..miujiza hii ipo tanganyika tu!...na mimi nikipewa nchi hii nitamteua mhindi ili tuwalishe pilipili mpaka..
 
Kuwa ya tatu inawezekana siyo kweli ila ni kweli kuwa ofisi ya usalama wa taifa ilikuwa ikijua sana kazi yake wakati huo. Kuna mtu alikuwa akiitwa Walingozi, yule bwana alikuwa siyo mchezo katika mambo ya usalama. Ni kutokana na usalama huo kuwa ingawa Nyerere alikuwa na maadui wengi matajiri, lakini walishindwa kabisa kumgusa. Kila wakijaribu mapinduzi wanakwapuliwa kabla hawajafika popote. Kwenye ile kesi ya akina Hans Pope, mmoja wa watuhumiwa (nadhani Badru Kajaja) katika testimony yake alionyesha kufadhaishwa sana kuwa plani zao zote zilipanguliwa na jamaa wa TISS katika muda ambapo ilikuwa zianze kutekelezwa kiasi kuwa wote wakachanganyikiwa wasijue namna ya kuendelea.
 
Huo ndi usalama wa Taifa ambao kamwe hauwezi kufananishwa na huu usalama wa mafisadi. Madudu chungu nzima kila kukicha lakini hakuna hata mmoja anayekamatwa!!! pia wameingia katika kundi la kutengeneza ushahidi fake ili waharibu maisha ya Watanzania katika juhudi zao za kukisaliti chama cha upinzani. Wako busy kuidhibiti CDM wakati nchi inawaka moto kwa matukio mbali mbali ya kutisha ambayo yanaongezeka siku hadi siku.

Kuwa ya tatu inawezekana siyo kweli ila ni kweli kuwa ofisi ya usalama wa taifa ilikuwa ikijua sana kazi yake wakati huo. Kuna mtu alikuwa akiitwa Walingozi, yule bwana alikuwa siyo mchezo katika mambo ya usalama. Ni kutokana na usalama huo kuwa ingawa Nyerere alikuwa na maadui wengi matajiri, lakini walishindwa kabisa kumgusa. Kila wakijaribu mapinduzi wanakwapuliwa kabla hawajafika popote. Kwenye ile kesi ya akina Hans Pope, mmoja wa watuhumiwa (nadhani Badru Kajaja) katika testimnoy yake alionyesha kufadhaishwa sana kuwa plani zao zote zilipanguliwa na jamaa wa TISS katika muda ambapo ilikuwa zianze kutekelezwa kiasi kuwa wote wakachanganyikiwa wasijue namna ya kuendelea.
 
Hakuna chombo chochote kile duniani ambacho hufanya kaz ya kupima na kutoa remarks in ranks kwa vyombo vya upelelezi duniani (intelligence agencies) kutokana na utendaji wao kwasababu task nying za vyombo hivi huwa ni siri na haziwi published baada ya kufanyika na hta ikitokea izo task zikajulikana bas huwa baada ya muda mrefu mf. operation dhidi ya Lumumba imeichukua dunia miaka takriban 40 kuujua ukweli, task ya MI6 kubroke Enigma codes za wajeruman kweny WW II ilikuja kujulikna after yrs.
Hivyo hizo assesment hufanywa na watu personally lakini mapungufu yake ni makubwa. Binafsi napingana na hilo la TISS kua ya tatu! unless nalata vgezo dhidi taasisi nyingne.
 
Ukiniambia Tanzania iliwahi kuwa nchi ya tatu kwa uzalishaji wa katani, utaniambia ni kwa tani, na mwaka. Na rekodi za World Trade Organization ambazo zipo na zinakubalika.

Of course kina Kiranga wanaweza kuzibishia, lakini Kiranga anaweza kubisha kwamba yeye mwenyewe ana exist, so that's entirely a different level of scrutiny.

Ukiniambia Tanzania iliwahi kuwa nchi ya tatu kwa upelelezi duniani, utanipa kigezo gani?
 
Ya tatu duniani? Hell no!

Ingawa hata mimi nilizisikia hizo simulizi na nilikuwaga nabishana sana na watoto wengine wa mtaani na shuleni lakini sikuamini hata kidogo.

Lingine nililokuwa nalisikia sana ni kuhusu makomandoo. Eti makomandoo wetu walikuwa wakali sana kiasi cha kuweza kuwachakaza makomandoo wa Marekani na Urusi.

Hata enzi hizo nilijua zilikuwa BS tu.
 
Hakuna chombo chochote kile duniani ambacho hufanya kaz ya kupima na kutoa remarks in ranks kwa vyombo vya upelelezi duniani (intelligence agencies) kutokana na utendaji wao kwasababu task nying za vyombo hivi huwa ni siri na haziwi published baada ya kufanyika na hta ikitokea izo task zikajulikana bas huwa baada ya muda mrefu mf. operation dhidi ya Lumumba imeichukua dunia miaka takriban 40 kuujua ukweli, task ya MI6 kubroke Enigma codes za wajeruman kweny WW II ilikuja kujulikna after yrs.
Hivyo hizo assesment hufanywa na watu personally lakini mapungufu yake ni makubwa. Binafsi napingana na hilo la TISS kua ya tatu! unless nalata vgezo dhidi taasisi nyingne.

Mr. .......007;
Hapo kwenye red panaonekana patamu mno, lakini sielewi chochote, and I'm not kidding. Unaweza ukadadavua kidogo stori zake kwenye red hizo hapo mbili?
 
Mbona kuna nchi zinafahamaika kwa majeshi zinaongoza duniani. Iweje intelligence agency tu ndo zisirankiwe? Wanazuoni niwaulize kwani ni lazima kila kitu kirankiwe kwa kuangalia quantitative data tu? Ina maana hatuwezi kujua kitu fulani ni cha ngapi kwa kuangalia qualitative data. Kama hatukuwahi kushambuliwa, na kama siri za usalama hazikuwahi kugunduliwa, na kama mbinu za majasusi ziligunduliwa mapema kabla madhara hayajatokea kwa nini tusijilinganishe na mataifa mengine na kujipa nafasi stahili? Mimi naweza kukubali kuwa huenda miaka hiyo intelligencia yetu ilikuwa ya tatu.
 
ilikuwa enzi za mwalimu enzi ya chama kimoja ila baada ya vyama vingi polisi,viwanja vya michezo,na open area,na majengo yaliyojengwa na wanainchi yakabakia ccm.hapo unategemea nini?
 
ilikuwa enzi za mwalimu enzi ya chama kimoja ila baada ya vyama vingi polisi,viwanja vya michezo,na open area,na majengo yaliyojengwa na wanainchi yakabakia ccm.hapo unategemea nini?
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom