Tanzania hatuhitaji bandika bandua, tunahitaji kuimarisha Taasisi. Hata Mama yetu akitoka madarakani tutakuwa na stori hizi hizi tu

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
23,410
36,560
Wakati nyimbo za maombolezo zikiendelea kupigwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mashada ya maua hata hayajanyauka katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Tz, JPM. Kuna mengi yameanza kuibuliwa ambayo ni mapungufu katika Uongozi wake. Hasara ya Shirika la Ndege, Ubadhilifu mkubwa katika mamlaka ya Bandari pia inaonyesha kuna upotevu wa Pesa nyingi katika Benki kuu yetu kiasi cha Madam President kuamrisha kuwepo kwa uchunguzi kati ya Jan, 2021-March, 2021.

Haya yote yanatokea na yataendelea kutokea milele kama kutakuwa hakujajengwa taasisi imara zenye kuwa na meno makali na uwezo wa kunusa harufu ya wizi na ufisadi na siyo kama sasa hivi Jeshi la mtu mmoja. Kwasababu hata JPM alipoingia alitumbua tumbua sana na kuwaamini hawahawa wanaotumbuliwa leo, inaonyesha mtu akijua ameaminiwa ni rahisi kukwapua na kutumia mamlaka yake vibaya kwa maslahi yake kwasababu anajua ameaminiwa na mkuu wa nchi na ndiyo maana hata PM wetu ndugu Majaliwa alipotembelea mamlaka hii ya Bandari waliosimamishwa kazi ni dagaa tu na inasemekana ndugu yetu Kakoko alikuwa huwezi kumgusa.

Binafsi nashauri tuimarishe zaidi taasisi zetu hasa wale watch dogs wanaoweza kunusa harufu ya wizi wa mali za umma (Usalama wa taifa), pamoja na kuzifanya taasisi zenyewe kuweza kujiendesha na kuacha haya maisha ya kuangalia upepo. Mama nayeye akija na tumbua replesi, tumbua replesi haisaidii nayeye anaowaamini watapiga tu maana wanajua amewaamini hata mtu akifanya wizi anajua tu hata akifukuzwa ana mzigo wa kutosha.

Kuna mengi yanatokea ila hata yakipelekwa Mahakamani hayajawahi kumpata mtu na akafungwa kwa wizi na kupukutishwa (kufirisiwa) kwasababu ushahidi either kwa makusudi unakuwa haunanguvu ama zile zile hela alizokwapua zinavuruga ushahidi.

Mama akitaka aache legasi yake vizuri atusaidie kujenga taasisi imara, kurekebisha baadhi ya sheria ziwe na majuto zaidi kwa mtu anayekutwa na makosa ya wizi na siyo kutumbuliwa tu na kuendelea kunywa kahawa home na ikimpendeza zaidi anaweza kutupa Katiba mpya kwasababu ni yeye alikuwa naibu Spika wa Bunge lile, vinginevyo itabaki wimbo uleule tu milele na milele.

Ni maoni yangu tu na samahani kwa mwandiko mbaya, ila daah kusikiliza hizi nyimbo na hotuba na nyimbo za kumbukizi ya mpendwa wetu JPM zimekuwa chungu sana baada ya jana Mama yetu kupokea zile taarifa na kuanza kuzifanyia kazi.

Tuendelee kuomboleza na kumkumbuka mpendwa wetu kwa yale mazuri JPM, kwa mema yake tu maana hakuna aliyemkamilifu bali tukitenga taasisi imara zitasaidia kutuweka salama zaidi.

FB_IMG_1617000073596.jpg
 
Back
Top Bottom