Taasisi ya chawa wa mama imetofautiana nini na mama?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,640
697,940
Kwakuwa episodes ni nyingi mno kama mashairi ya mnanda, ukianza wimbo ni mwendo mdundo hakuna kupumua...
Kwakuwa tumeumbiw kusahau haraka sana na tumekuwa wabovu wa kutunza kumbukumbu kuna vingi vinatupita bila kuvipa marejeo stahiki...

Ni miezi mitano tu imepita (siku 150 hivi) tangu izinduliwe kwa mikogo na mbwembwe nyingi, taasisi iliyojiita CHAWA WA MAMA Hii taasisi isiyo na kichwa wala miguu ilijinasibu kumtetea mama toka kwa wapinzani wake kisiasa na wengine wote wanaoenda tofauti naye. Huku ikijivika jukumu la kuelezea mazuri yote yaliyofanywa na mama na kuyatolea ufafanuzi kila ilipobidi..

Mwezi ule wa tatu taasisi hiyo ya chawa wa mama ikaanza kuzindua na kufungua matawi mikoani huku ikitamba kuwa ina wanachama nchi nzima hivyo itafungua matawi yake kila kona ya nchi... Ikiwemo Tanzania visiwani

Sie twenye marejeo tukatunza kumbukumbu kwa wino mwekundu huku tukiandika na mada za kufafanua neno chawa na mabaya yake! Ili nyakati zikitimia tuyarejelee makabrasha!

Miezi mitatu tu baada ya taasisi tajwa kuzinduliwa kwa madaha na majigambo ya kila aina likaibuka suala zito la 'uuzwaji' wa bandari zetu zote..

Kwa miezi hii miwili, mama akapitishwa kwenye tanuru lenye fukuto kali sana kuhusiana na hilo sakata zima la bandari.. Na sasa kuna kesi mahakamani inaendelea
Kwa jinsi hali ilivyokuwa ngumu ilitarajiwa na wengi kwamba wa kwanza kabisa ambao wangejitokeza kumsaidia mama kwenye hili ingekuwa ni taasisi yenye nguvu na ushawishi mkubwa TAASISI YA CHAWA WA MAMA Lakini kwa mshangao wa wengi mpaka sasa hakuna hata mmoja kati yao aliyesimama na walau kukohoa tu ili uwepo wao ujulikane! Ama walau hata kutoa press release moja tuu...

Waliojitokeza kumtetea ama kusimama na mama ni watu wengine tofauti kabisa nje ya taasisi ya chawa wa mama!
Sasa ninini kimeisibu hii taasisi?
Ni mapunjo kwenye ulaji?
Ni kubaguliwa!?
Ni kudharauliwa?
Ni kutengwa?
Ni kunyimwa kabisa mgao?
Ni kugundua walitumika kama toilet paper na sasa hawana thamani tena?

Je mfadhili aliwaona ni vidampa tu wasio na mbele wala nyuma, wakionekana kama wachumia tumbo tu wasio na maana yoyote?
Vyovyote iwavyo kuna kitu cha kuumiza kimeipata hii taasisi ndio maana kwenye sakata zima la bandari haionekani popote!

Zaidi soma:

Thread 'Mama ana chawa wake?' Mama ana chawa wake?
maxresdefault%20(1).jpg
FpuD_OPWIAMqdvF.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matatizo ya siasa za Africa zinaangalia watu, badala ya kuangalia sera.

Mkapa alimwambia Magufuli asiseme serikali ya Magufuli, aseme serikali ya CCM.

Nyerere katika press conference ya Kilimanjaro Hotel alikataa kumjadili Mrema, akasema atajadili sifa za mtu atakayefaa kuwa rais.

Lakini bado hatujaelewa somo, tunang'ang'ania kuangalia watu.
 
Thread 'Mama ana chawa wake?' Mama ana chawa wake?View attachment 2700377View attachment 2700381

Sent using Jamii Forums mobile app
🙄 duh!
 
Back
Top Bottom