....Criteria ya kutoa udhamini kwa mwanafunzi dunia nzima ni moja tu, kufaulu vizuri! Serikali itoe mikopo na udhamini kwa wanafunzi waliofaulu vizuri bila kujali mtoto wa mkulima au wa tajiri.
...
Serikali isomeshe wanafunzi kwa 100% kwa kuzingati viwango vyao vya kufaulu mpaka pale uwezo wake unapoishia!
Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly.
Kama umekuwa ukifuatilia mijadala yao (bodi ya mikopo na wanafunzi) kwa makini na kuwaelewa wanachosema ni kwamba "maskini wasaidiwe na matajiri wajilipie kulingana na hali yao". Hapo ni sawa kabisa.
Lakini wanafunzi wanachosema ni kwamba njia inayotumika kujua nani hana uwezo na nani ana uwezo iko 'flawed' na hivyo inasababisha baadhi ya watoto wa vigogo kusoma hiyo mikopo na wale wa wazazi wasio na uwezo kukosa na wakati huohuo serikali inadhani mambo yanaenda vizuri kabisa. Hili linawauma sana!
Kwa bahati mbaya kila wanafunzi wakitoa hoja zao tunashindwa kuelewa wanachokisema ni nini. Tunabaki tu kupotosha wanayosema na kuweka siasa kwa namna inayotupendeza. Lakini hatuoni kuwa tunaendelea kuharibu taifa letu sisi wenyewe.
Mkuu, iwapo wanafunzi wangekuwa na hata nusu ya uwezo wako kujielezea, hili suala wala lisingekuwa gumu. Mtu akisoma bandiko lako anapata mwanga zaidi kuliko vitisho vinavyotolewa na hao Daruso (au labda vyombo vya habari-ambavyo wengi ndimo tunapata taarifa, vinachagua cha kuandika).
Hoja unayoieleza hapa, kwamba mfumo upo flawed inaeleweka sana lakini hilo halihalalishi kuwa kila mwanafunzi apatiwe 100% loan.
Kama mfumo uko flawed, solution ni nu kufanya revision. Lakini kikubwa ambacho kinasikika kutoka kwa wanafunzi ni kutaka loan kwa asilimia zote. hatutafika kwa mtindo huo
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine
Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly.
Wakati USA, leo hii Obama anakuwa mtu atakayeifanya NDOTO ya Dr. King kuwa kweli na hivyo kuimaliza hizo ndoto, Tanzania tumeanzia kwa Obama na kwenda nyuma kwenye wenye nazo na wasio nazo. Matabaka yanazidi kutanda. Wengine wanafikiri matabaka kila sehemu yapo na Tanzania lazima yawepo. Ni kweli ila details ndiyo zinaleta shida siku zote. Wanasema "Demokrasia ni udikteta kwa walio wachache".
Nchi zilizoendelea, matajiri na watu wa hali ya kati ni wengi kuliko masikini. Tanzania ni kinyume chake. Hii inapeleka kuwa na Watusi (10%) kuwatawala Wahutu (90%). Amini usiamini, siku moja mapanga yatatembea. Na wala hutajua yalianza-anzaje. Ila kama masikini ni 10%, hawawezi kutembeza mapanga kwa watu 90%.
Haihitaji kuwa na akili sana au msomi sana ili kuelewa maneno ya kijana. Kama ni kijijini basi utasifiwa kuwa na wewe ni NABII kwani ulijua mapema kuwa hili litatokea. Ikumbukwe kuwa sisi hatupishani sana na Wakenya. Utalaani vyama vya upinzani weee lakini Mkenge umeutaka mwenyewe kuukalia.
Yes, serikali uwezo wake mdogo sana.
Mashangingi ya bei mbaya 700 kwa mwaka mmoja. Kukodisha ndege mbovu za ATCL, zilizopelekwa Kiwira kimya kimya, za safari, za vikao, washa, seminar, kongamano................ Kweli serikali uwezo wake mdogo, AMEN!!
Tujue kuwa serikali si kijiwe bali serikali ina dhamana kwa nyanja zote na tunalazimika kugawa tulichonacho katika nyaja hizo na ndio maana mashangingi yananunuliwa ili miongoni mwa hao wanaosoma sasa watakapoingia serikalini wayatumie. Warsha na semina pia wanaonufaika nazo ni haohao wanaotoka vyuoni . Fedha inazalishwa na mkulima lakini mkulima hanufaiki nayo lakini tunaziba midomo tunaposikia unyanyashaji wa wakulima. Serikali ni yetu na ni sisi wenyewe tunaotowa ubavu kwa viongozi watuchagulie namna ya kutumia fedha zetu. Hebu natuwatetee wakulima na sio hawa wanaogombania kupanda daraja la watawala.
Huyokijana kama angetabiri huo utabiri wake kwa kigezo cha wafanyakazi dhidi ya waajiri, wakulima dhidi ya serikali, chama tawala dhidi ya wapinzani, matajiri dhidi ya masikini basi hayo unayoyasema yangeleta maana lakini kuwa Tanzania isikalike kwa kikundi cha wanafunzi ambao nao wako katika harakati za kukwea kwenye tabaka la walionacho nafikiri Watanzania tuna akili ya kuchaguwa zuri na baya.
Ngekewa,
Unachosema ni sawa. Ila kwa mawazo yako, hayo Mashangingi, EPA, DEEP GREEN, Mwananchi Gold, Radar, Ndege ya Rais, Helcopiter za jeshi, Kiwira, Richmonduli, IPTL, ATCL, Meremeta na hizo zote Blingbling...... kwako wewe ni SERIKALI au KIJIWE CHA MAFISADI? Ngoja tusubiri na sisi Yesu wetu aje na kuwafukuza watu wote walioifanya Tanzania kuwa PANGO LA WANYANGANYI. Vibaka wakubwa. Hawana hata aibu kutaka kuifufua ATCL tena bila woga ila wanafunzi ambao kesho watalipa madeni na kulipa kodi wanaambiwa kwa kimyakimya YOU CAN GO TO HELL.
Naona mwenzetu una NGEKEWA zako. Haya hayakuhusu na wewe kila kitu ni NGEKEWA. Wengine kila kitu lazima tukaze misuli ....
Wangelikuwa wako makini, hi;i lisingelitokea. Wangelionyesha mfano kuwa tukaze mikanda, mie ningelikuwa wa kwanza kuwalaani wanafunzi. Ila wao ndiyo kwanza Pinda kasema ananunua Mashangingi ya mwisho 700, juzi wanatangaza tenda ya mashangingi mapya..... Eti serikali si KIJIWE!!!
Yaleyale.... kuwadharau vijana. Nyie Vigogo siku zote mnahau historia. Wenzenu walisema hivyohivyo. Wakawaona vijana wanachemka. Vijana walivyoanza mavituz ikawa tayari too laite. Uliona juzijuzi wanafunzi wa shule ya msingi walivyoji-organise?? Angalia mabadiliko yaliyotokea Uholanzi, Ufaransa na Europe in general. Vijana wakaanza kuchoma na kubomoa nyumba huko Ufaransa. Wee kaa na kusubiri watabiri kwa wakulima. Ndiyo ubaya na uzuri wa vijana wa unga/bangi. Siku wakianza kudai haki zao, wala hawaogopi kitu. Watachoma na kubomoa hayo mahekalu ya MAFISADI na kibaya zaidi ni kuwa wanaweza kuwabeba hata waliochuma mali zao halali.
The day will come. Ngoja nimsikilze Obama.......
shy ndugu yangu hii ndiyo lugha ya kujidanganya.Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine
Hatuogopi vitisho, tuko tayari kufa, kufukuzwa chuo na hata kwenda jela, tutaendelea kutetea watoto wa masikini, kwani kinachoendelea sasa ni kutengenezwa kwa matabaka kati ya masikini na matajiri, tunaomba Serikali iwarudishe wanafunzi wote vyuoni, vinginevyo Tanzania haitakalika,
Hayo ni maneno ya Machibya, aliyekuwa Rais wa iliyokuwa DARUSO. Maneno yake yanafanya nijiulize, hivi Machibya anaelewa maana ya maneno anayoyasema? Tanzania haitakalika, kwa hiyo watanzania wataenda wapi??? na nini kitafanya isikalike? Nani anampa huyu mwanafunzi kiburi cha kutishia maisha ya watanzania? Hizi lugha zisizo na busara zinaonyesha aina ya uongozi uliokuwepo DARUSO. Na sasa watanzania hawawezi kushangazwa na uamuzi wa kuifuta DARUSO iwapo huu ndio upeo wa viongozi wake.
Mkuu, iwapo wanafunzi wangekuwa na hata nusu ya uwezo wako kujielezea, hili suala wala lisingekuwa gumu. Mtu akisoma bandiko lako anapata mwanga zaidi kuliko vitisho vinavyotolewa na hao Daruso (au labda vyombo vya habari-ambavyo wengi ndimo tunapata taarifa, vinachagua cha kuandika).
Hoja unayoieleza hapa, kwamba mfumo upo flawed inaeleweka sana lakini hilo halihalalishi kuwa kila mwanafunzi apatiwe 100% loan.
Kama mfumo uko flawed, solution ni nu kufanya revision. Lakini kikubwa ambacho kinasikika kutoka kwa wanafunzi ni kutaka loan kwa asilimia zote. hatutafika kwa mtindo huo