UbungoUbungo,
Unaandika maneno amengi pasipo hata kujifunza toka kwa wenzako. Nimekwambia toka nyuma kwamba hakuna sheria inayoruhusu Blockade ndani ya International water - HAKUNA na ulikubali sasa unakuja kwa nukuu ya Myahudi mwingine anavyofikiria yeye kwa utetezi kama wako pasipo kutumia vifungu vya sheria.
Pengine labda pitia
wikipedia utaelewa kwamba hizo blockade haitambuliki na vyombo vya kimataifa na hata hivyo kuwepo kwake haikugusa International water kwa sababu sheria hairuhusu. The fact is Hamas walishinda Uchaguzi na nchi za magharibi hawakupenda kwa sababu demokrasia yao haikuweza kufanya kazi. Wao wanamtaka Mahmood Abas ambaye ni kibaraka wao, na kumpa hadi wadhifa wa rais wa Palestine japokuwa alishindwa Uchaguzi. Palestine is the only country dunia hii ikiongozwa na rais aliyeshindwa Uchaguzi, yet bado wanadai ndio demokrasia.
Mwisho unatakiwa kusoma zaidi ufahamu kwamba kuna tofauti kubwa sana baina ya JEWS na ZIONISM. Wapo viongozi wengi wa Kiyahudi (Rabba) na wafuasi wa dini wanapinga harakati za Zionist ambazo ni sawa kabisa na Apartheid..Hata sisi hatukuwachukia Makaburu kwa sababu walikuwa wazungu laa hasha isipokuwa in Kisiasa waliweka sheria za kibaguzi na sheria hizo hazikutambulika kimataifa lakini bado walizitumia dhidi ya weusi.
Mkuu wangu, imani yangu nitaendelea kuamini kwamba JEWS ni wafuasi wa dini ya Judea na Moses sii kizazi kinachotokana na mwanamke Myahudi. Kwa sababu wapo wengi tu mfano wa kina Natanyahu ambao mama zao walikuwa convert ktk Judaism, wakaolewa na baba mrusi, MPolish au Muingereza kisha watoto zao wanaitwa Wayahudi hata kama hawaifuati dini ati kwa sababu mama yao alikuwa Myahudi.. F...that.
Dini ni imani ya mtu sio uzawa wake, na sisi sote Waislaam, Wakristu, Wayahudi, Hindu na kadhalika tumeanza kufuata Gosple ya shetani (binadamu) kuamini kwamba unaweza kuwa Muislaam au Mkristu kwa kuzaliwa sii lazima kuwa muumini wa dini au Mungu..Ati mtu akiona jina la mtu tu Mohammed au Joseph tayari tumekwisha mpachika dini pasipo hata kuangalia iabada zake. Mungu aliwaita Wayahudi kwa sababu ilikuwa dini na walifuata mafundisho yake,hakuwa na maana wana wa Israel wote walikuwa Wayahudi, walikuwepo Wana Israel ambao hawakuamini kama tulivyo sisi ktk dini zetu..