WanaJF ningependa kuweka sawa kuwa kiasilia hakuna mtu au nchi iliyotutenga WaTz hapa. Labda ieleweke tu kuwa kila kiongozi wa nchi ana jukumu la kusimamia na kutetea maslahi ya nchi yake na wananchi wake ili kuboresha maisha yao. Na katika hili hakuna nchi nyingine itakayokupigania. Kinachofanywa na hawa viongozi wa nchi jirani ni hicho hicho.
Pia ikumbukwe kuwa lengo la kuwa na uchirikiano kama wa EAC ni kuweka pamoja rasilimali zetu kama watu (kwa maana ya soko) na miundombinu; taratibu za kodi nk ili kurahisisha biashara na kuleta economies of scale hasa katika uwekezaji.
Tanzania ina advantage ya kijiografia kwa sababu mbali na kuwa na habari, inapakana na nchi zote zingine nne za EAC (na kwa hivyo ina easy access ya masoko ya nchi zote hizi) na kwa ujumla inapakana na nchi sita (hinterland states) ambazo zingepaswa kutumia bandari zetu kikamilifu.
Mwanzoni mwa miaka ya 1980 Nyerere alijenga bandari ya nchi kavu (dry port) ya Isaka kwa ajili ya kushughulikia mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC. Mizigo ilikuwa inasafirishwa kwa reli mpaka Isaka na baada ya hapo kwa barabara ya lami kwenda kwenye nchi hizo. Pia kulikuwa na mpango wa muda mrefu wa kujenga reli kuunganisha Isaka na Rwanda na Burundi. Kadhalika, kulikuwa na mpango wa muda mrefu na ambao ulisisitizwa sana na Uganda baada ya Museveni kuingia madarakani wa kujenga njia ya reli kutoka Arusha hadi Musoma kwa ajili ya kuunganisha Uganda kiurahisi na bandari ya Tanga. Ikumbukwe miaka ya 1970 Nyerere alijenga reli ya Tazara ambayo iliunganisha Zambia (na DRC ya kusini) na bandari ya Dar.
Sasa tujiulize kilitokea nini mpaka tumefika hapa na kuanza kulalamika kuwa tumetengwa? Mabadiliko ya mfumo ya kisiasa na kiuchimi yaliyotokea hapa nchini mwanzoni mwa miaka ya 1990 na kutekelezwa na serikali ya CCM kihakisia yaliua kila kitu kilichokuwapo kwa manufaa ya watu wote na kukiweka mikononi mwa watu binafsi wa ndani na nje na wakati huo huo watawala wakiwa ni mawakala au wabia wao (kwa ujumla wao tunawaita mafisadi). Hivyo miondombinu ya reli ikaonekana haina tena manufaa kwao na hivyo ikatelekezwa kwa kutokunfanyiwa matengezezo na kutokununua injini na mabehewa mapya. Wakaanzisha makampuni yao binafsi ya kusafirisha mizigo kwa malori ili kuchukua nafasi ya reli. Pia hili tabaka la mafisadi ambalo sasa ndio liko madarakani likadhoofisha sana uendeshaji wa bandari nchini kiasi cha bandari zetu kuwa taabani kuitendaji. Ili bandari yoyote iendeshwe kifanisi lazima uinganishwe na reli inayofanya kazi viruzi (an efficient railway network).
Matokeo ya ufisadi huu ni kama ifuatavyo:
Inachukua wastani wa siku kumi kwa meli kusuniri kuingia bandarini kupakua mzigo katika bandari ya Dar (Mombasa inachukua siku moja!)
Kutokana na riport ya Bank ya Dunia Tanzania inapoteza UD Dollars 1.8 billion (TSh 2.88 trillion) kwa mwaka kutokana na utendaji mbovu wa Dar Port na mchi jirani zinazohudumiwa na hii bandari zinapoteza zaidi ya USD 800 million (Tsh 1.3 tr) kwa mwaka.
Gharama ya kupakua/kupakia mzigo katika bandari ya Dar ni 74% zaidi ya gharama katika bandari ya Mombasa. (Kuna waziri wa Kenya mwezi uliopita alisema bandari ya Mombasa ingedorora kama WaTz wasingekuwa usingizini!). Na ndio maana waagizji wengi wa magari (dealers) wa Dar wanapitishai mizigo yao bandari ya Mombasa.
Kusafirisha mzigo kwa lori tuseme kutoka Dar kwa barabara mpaka Rusumo (mpaka wa Rwanda) ni kizungumkuti. Kuna weigh bridges kibao na gari itasimamishwa na polisi (halali na feki) zaidi ya mara mia moja njiani na mara zote dereva atatakiwa atoe kitu kidogo!
Katika mazingira kama haya viongozi wa nchi jirani wangefanya nini na ukichukulia kuwa wananwajibika kwa wananchi wao? Halafu Kenya sasa wana rais ambaye kibiashara/kiuchumi ni mpambanaji (proactive) na hawezi kulaza damu na kuachia fursa zinazotokana na watawala wa Bongo kujikita tu kwenye ufisadi. Kama ile kauli mbiu ya Bill Clinton wakati wa kampeni za uraisi Marekani 1992 inavyosema, Its the economy stupid! Maana yake kiongozi yeyote makini siku zote ataweka mbele maslahi ya kiuchumi ya nchi yake.