Tanzania excluded from EAC joint communique

Tanzania excluded from EAC joint communique

Hii biashara ya kututenga inaweza kuwa " a blessing in disguise" kama wanavyosema wenzetu. Kama tutatekeleza mawazo ya akina Prof. Wangwe, sina shaka tutasonga mbele kwa kasi zaidi kuliko ambavyo ingekuwa ndani ya EAC.
Nadhani tusichukulie huo mpango wa jirani zetu on a negative side pekee. Tuangalie jinsi inavyoweza kutunufaisha zaidi.
 
Hiyo ni mipango inayoambatana na mihemuko ya Kagame, waacheni tu sisi tushikamane kama nchi na tuwe tayari kupingana na njama zozote za kutaka kutuhujumu.

Kabla ya kumlaumu Kagame au Kenyatta au M7 je tumejiridhisha kuwa Mhe Dkt JK hakuletewa mwaliko? Tumemuuliza Salva Rweyemamu ili atupe habari za uhakika? Je ukijaambiwa kuwa Mhe Daktari JK aliletewa mwaliko lakini kwa sababu zo zote zile hakuweza kuhudhuria utasema nini? au basi kwa vile Kagame amekuwa Kagame waTZ hatimaye tumepatiwa wimbo mpya wa Taifa. Sitashangaa sasa hivi kusikia matatizo yetu ya miaka 50 huo mzigo anatwishwa Kagame. Kurugenzi la Mawasiliano la Ikulu tafadhali tusaidieni, je mwaliko haukuja? Jibu lenu litatusaidia kuwa na mwelekeo sahihi wa mjadala huu.
 
kwa sasa nguvu kubwa ni kuikomboa congo na ukoloni wa kagame hawa wengine tutawaangalia baadaye tuwafanye nini.

Tatizo ni kwamba kwa swala la Congo DRC,Tanzania imepanda meli ambayo haijui inakoenda.Ninachojiuliza ni kwamba hivi tunaelewa kinachoendelea Congo kweli.Wenzetu wa nchi za Magharibi na Israel wako Congo kupora utajiri wa Congo wakishirikiana na Kabila.Kagame naye yuko DRC kupora.Sasa sisi tumekwenda kuwasaidia wazungu kupora au vipi.Si afadhali tungemsaidia mweusi mwenzetu.Inasikitisha kuona wezi wakigombana.Tanzania ngoma hii huwezi kuicheza ondoka!
 
Kumekucha! TZ yatengwa EAC

Hii siyo EAC Joint Communique- ni ya nchi tu zilizokutana, ndiyo maana hakuna sehemu yoyote EAC inatajwa. Pili South Sudan si mwananchama wa EAC. Tatu ingekuwa EAC Secretariat akiwemo Katibu Mkuu wake wangekuwepo. Sijui mnaotoa hizi habari mnataka kuchonganisha au mnapotosha kwa madhumuni gani?
 
This was not an East African Community (EAC) event as many people would like to believe. This meeting had much to do with increasing the efficiency of Mombasa port on which Uganda, Rwanda, Burundi and South Sudan depend for their imports and exports. This explains the attendance of those three countries' heads of state along with Kenyan President Uhuru Kenyatta.
 
Just like that? Kwa ile statement ya JK tu kuhusu M23? Labda kulikuwa na mengine tusoyajua.

JK hakwenda Mombasa kwenye uzindizi wa bandari.
Huyu jamaa yetu (JK) ni mwepesi sana 'kudandia' mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kutoa 'ushauri'.
 
Mimi naona ni nafuu wacha waitenge lakini moto wake watauona. Kwani tukibaki peke yetu shida ipo wapi EAC ni mzigo mwingine rudisha wabunge wote makao makuu Arusha ni mali yetu maana ipo ndani ya Tz... waendelee na umoja wao ambao hautakuwa na muda mrefu maana wote wakorofi.. Kila la heri New East Africa uchwara...Ziara ya Obama inawauma sana hawa watu sasa ndio wanapalia makaa watashangaa.
 
Tutasema sana tu, lakini kuumia ndio huko. Kutengwa na jirani yako kuna madhara makubwa tusijifariji. Tutafute sababu na kujisafisha. Tumebweteka kwa kulewa misifa kwa kukalia raslimali na kuwauzia wazungu. Ni laana tuliyoitafuta siku zote. CCM hoyeeeeeee! utuzike salama, maana unaendelea kutujaza ujinga ati bora tule nyasi na kubeba msalaba wake. Tunashikishwa adabu, ina maana hata misimamo ya nchi hii haingwi mkono na majirani zake wote.


Na bandari yenyewe malalamiko kibao! mikataba ya kinyonyaji ya Ticks!
 
Hapo ni urafiki wa mashaka,hawana muda mrefu hao watakwaruzana vibaya vibaya Kagame atakapoanza kuwapelekesha

Ni hivi wote wakorofi...weka huyu kaguta,hako kagame wa sudan ndio usiseme hao hawaendi mbaali...
 
This was not an East African Community (EAC) event as many people would like to believe. This meeting had much to do with increasing the efficiency of Mombasa port on which Uganda, Rwanda, Burundi and South Sudan depend for their imports and exports. This explains the attendance of those three countries' heads of state along with Kenyan President Uhuru Kenyatta.


This is not the first incidence that Tanzania has not been invited and it seems those three leaders have reached an agreement to exclude Tanzania. In fact, they see Tanzania not as partner state but an impediment for EAC federations' dream. It is sad that EAC doesn't have cool heads momentarily. Leaders have allowed their emotions to control their decisions as a result they are not looking at the big picture. Please, read the below article and you will figure out why many Tanzanians feel like they are being alienated. And even Kikwete's spokeman, Rweyemamu, has confirmed that Tanzania was not invited.


Burundi and South Sudan join new EAC partnership - News - nation.co.ke
 
This was not an East African Community (EAC) event as many people would like to believe. This meeting had much to do with increasing the efficiency of Mombasa port on which Uganda, Rwanda, Burundi and South Sudan depend for their imports and exports. This explains the attendance of those three countries' heads of state along with Kenyan President Uhuru Kenyatta.

Na hii inamaanisha nini?
FAST TRACKING POLITICAL FEDERATION

• Ministers responsible to meet in Kampala from 10th -12th September, 2013 and report on the roadmap by 15th September, 2013 as well as prepare a zero draft of the federal constitution by 15th October, 2013.
 
Tatizo ni kwamba inachukua zaidi Ya mwezi kuikomboa container hapo dsm wakati mombasi hachukui mda mrefu, na pia gharama kubwa ya kuikomboa container kwa ajili ya rushwa. Hapo bandarini kulichafuka sana
 
...watanzania tuache porojo....lazima foreign affairs waje hapa watoe tamko kama walialikwa Mombasa ama la??...maana naona hata rais wa sudan na burundi wametuma wawakilishi wao.........siamini kuwa kweli tz hawakualikwa....maana tunaweza kuwa tunapiga kelele kuwa tz wametengwa...wakati labda wamealikwa wakasepa.......We need to hear from the TZ foreign ministry....kuhusu huu mkutano......maana hata kama JK alikua na udhuru.....TZ walishindwa kumtuma representative(kama sudan na burundi)???.....maana itashangaza wabongo wamekaa dodoma wanajadili urais wa 2015 ...na kupongezana...wakati wenzao wanapitisha joint communiques za maendeleo kwa wananchi wao......tuache ushabiki kwenye haya mambo wabongo.....


Angalizo: Hawa jamaa wamezungumzia mambo kama: EAC single tourist visa.....pia single customs territory...na pia ku fast track political federation...haya yote wameyazungumzia kwenye context ya EAC.....kwa hiyo TZ tusijidanganye kuwa haya mambo hayatuhusu......Swali la msingi ni je...kwanini TZ haikutuma mtu???????????na next summit wamesema itafanyia Kigali in October 2013.....tuone kama JK hatohudhuria...maana hii itakua mara ya tatu kwake(kama hatohudhuria)......Kwanini watu wanasema TZ inatengwa...na sio TZ inajitenga(tukumbuke kuwa huko nyuma kumewahi kuwa na malalamiko toka EAC member states kuwa TZ wamekuwa kikwazo kwenye baadhi ya mambo)....mbona tunang'ang'ania kutengwa??????
 
Hii siyo EAC Joint Communique- ni ya nchi tu zilizokutana, ndiyo maana hakuna sehemu yoyote EAC inatajwa. Pili South Sudan si mwananchama wa EAC. Tatu ingekuwa EAC Secretariat akiwemo Katibu Mkuu wake wangekuwepo. Sijui mnaotoa hizi habari mnataka kuchonganisha au mnapotosha kwa madhumuni gani?

umeeleweka mkuu - hivyo kikao kijacho rasmi cha wakuu wa nchi EAC ni lini mkuu au vikao havina ratiba maalum. ni muda sasa.
 
Waende zao na vi-nchi vyao vidogo vidogo! Na wakumbuke kuwa, watakuja Presidents wengine wa nchi zao watakaotaka kushirikiana na Tanzania.

Shame on Uhuru na Kagame, it seems these two presidents are the mastermind behind this saga.
 
Hapa wa kuangalia (na pengine kulaumu kuvuruga EAC) ni Kenyatta na siyo Kagame. Naona anaendeleza sera za baba yake (RIP). Maana hata miradi hiyo ilivyokaa ni kuifaidisha Kenya kwa kiasi kikubwa ..
 
umeeleweka mkuu - hivyo kikao kijacho rasmi cha wakuu wa nchi EAC ni lini mkuu au vikao havina ratiba maalum. ni muda sasa.

Vina muda na ni mara moja kwa mwaka - Novemba mwisho (kiako rasimi). Mara nyingi wanakuwa na kikao kimoja kingine (extra ordinary).
 
Hawa wakenya ni wajanja sana, hebu fikiri hadi kufikia 2018 wao watakua wapi kimaendeleo ya hiyo miundombinu ambayo yooote inaanzia kwao, na jee wakiamua kuvunja mahusiano baadae kama walivyofanya mara ya kwanza wakabakia na viwanda vyote na sasa wanatuuuzia bidhaa kwa hela ya juu sana, nawaonea huruma hao mburula wengine!! Pia kwa wivu wao wa kuikosa Tanzania, wameamua eti kuishirikisha Burundi (huu ni ujinga) hata maendeleo yafike huko hii sayari haipo tena!! Kama haitoshi wananyemelea South Sudan, wanategemea mafuta na pengine ardhi sasa wasije waka-mess up na hawa jamaa TZ haitawasaidia!! Mimi naishauri TZ iondoshe majeshi yake kule Sudan ya kusini hatuna tija nako!!!!
 
Back
Top Bottom