Hili limenilazimu kutoka pangoni.
..... Historia inaonesha mataifa na mwanadam kwa ujumla huwa mbunifu na pia uendelea kwa kasi pale mazingira yanapompa
changamoto nzito. Tushukuru mungu tumepata fursa ya pekee kujua jirani yako anamtazamo gani na wewe. Jambo hili huwa
ni adimu sana, matokeo yake hujikuta umezungukwa na watu wengi maishani lakin wachache ni wakweli.
..... Kijiografia Tanzania haina sababu yoyote ya kutishwa na maamuzi haya. Kwa ufupi dunia
ya leo commerce ndio inayotawala na kuendesha siasa. Trade volume kati ya Tanzania na nchi
hizi inaonesha kuwa athari za maamuzi aya ni ndogo sana kwa taifa letu. Inanishangaza kidogo
kuhusu Kenya maana hawa ni mojawapo ya wawekezeji wakubwa Tanzania kwa vyovyote vile nchi yetu
ikiamua kujibu mapigo wataumia sana na hili.
..... Kuna hili la chakula, asilimia kubwa ya chakula na nafaka katika ukanda huu inazalishwa na Tanzania
na hizi nchi huja hapa kununua. Nilifika Mufindi miaka ya nyuma na kukuta hawa majirani wakinunu kwa
wingi mbao na chai yetu. Nilirudi mwaka mwingine nikakuta biashara hii imeongezeka.
Nilipokuwa Arusha niligundua kuna bishara kubwa pale Namanga ya mboga mboga kutoka nchini kuelekea
kule ngambo ya mpaka.
..... Nishati, kwa ufupi hapa ndio pana utamu kweli! Katika hili tutazame The China scenario, leo hii
asilimia kubwa ya viwanda Ulaya na Marekani viwanda vinafungwa na kuamia China au kununua hizo
bidhaa china, sababu kuu ikiwa ni urahisi na unafuu wa bidhaa hizo. Kwa ufupi ukizalisha bidhaa
yenye ubora kwa bei nafuu, haijalishi upo wapi wanunuzi watakuja, nchi zote za kusini mwa bara la
Africa zinamahitaji makubwa ya nishati, na haya yanazidi uwezo wa vyanzo vyao na pili hawana njia
mbadala.
ENERGY & FOOD are the biggest global concerns right now. The world's eyes are all on us, recent visits
by key figures is sufficient testimony. Tanzanians, you have the largest gas and hydrocarbon deposits
along with the largest unutilised agricultural land on the planet.
You only need good accountable & responsible leadership, not a federation or quarrels.
Tanzania hiii ni FURSA KUBWA......
Tanzania sitetereke........
Tanzania wewe ni mzazi wa wote hawa ..... mwana hawezi mtisha mzazi.